Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Membe umefeli. Bila hao kuungana basi unatwanga maji kwenye kinu tu. Ila ninachojua baadae utarudi CCM na utachukua form ya urais kupitia CCM 2025.

Yaliyotokea kwa Lowassa 2015 ni somo tosha kwa wapinzani wa kweli. Sio kila siku ni Ijumaa. Sisi tunataka tume huru ya uchaguzi, mbwembwe za mazee ya ccm zimetuchosha. Tuna kampeni nzito ya kuhakikisha wapiga kura wanakuwa wachache kupita maelezo iwapo hakuna tume huru ya uchaguzi. Na kampeni hii vizuri na itatoa majibu chanya.
 

Ahaaaa ahaaaa nimecheka ile mbaya, halafu huyo mzee anakuja na swagga za Lowassa zile alizoleta 2015. Nikisikia hayo maneno ya kitapeli ya huyo mzee nakumbuka ya yule tapeli mwingine Lowassa. Huyo Membe ajue shida ni wakati wa kwenda, wakurudi anajua pabaya na pazuri. Aendelee na hiyo ACT kwa cdm hapana.
 
Membe hana msaada wowote ule,Membe ni Lowassa part 2.FULL STOP

Atagawa kura za upinzani,atashindwa kwny uchaguzi kama kawa na akimaliza kazi yake atarudi zake kwao Ccm kama kawa.

Membe ni Lowassa wa Lindi. Wapiga kura wengi wa upinzani tunajitambua, hata Mbowe alibahatika sana kumleta Lowassa na watu wakamkubali. Ila baada ya wanaccm waliokuja na mafuriko ya Lowassa kuanza kurudi ccm, sasa tutaonyesha kuwa tunajitambua vizuri sana.

Haturudii kosa, acha ACT arudie kosa maana wao ndio wanategemea siasa za kunyanyuka kwa umaarufu. Cdm walishavuka hatua hiyo kwa somo kali. Ni vyema tukajikita kwenye kudai tume huru ya uchaguzi, na sio kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kihuni.
 

Ni vyema zaidi kuungana kushinikiza kupata tume huru ya uchaguzi, kuliko kuungana ili kushiriki uchaguzi kwa kuwatumia makada wa ccm. Tukishusha idadi ya wapiga kura nchini, itakuwa na impact kubwa sana, kuliko kushiriki uchaguzi ambao tayari Magufuli ana matokeo yake mfukoni.
 

Mkuu kunywa utakacho nakuja kulipa. Hiyo ACT iliasisiwa na kina JK, Membe, Mwigulu nk. Na lengo ilikuwa ni kukabiliana na cdm kwa faida ya ccm. Huyo Membe ndio mmiliki halisi wa ACT, hivyo mmliki rasmi wa ACT ndio katua kwenye mali yake. Kwa sasa tumestuka. Cdm haina tatizo na wapiga kura, na wapiga kura wake wengi wanajitambua, na wanajua hizi siasa za kishamba za Magufuli zitaisha, na chama kweli cha upinzani kitaendelea kuwepo kwa kasi kubwa zaidi.
 
Sasa wapinzani watashinda vipi kama watu hawatojitokeza kupiga kura ?Pigeni kura lindeni kura hakuna wa kuwaibia. Ondoeni negativity. Mkicheza Bunge halitakuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani. Kama ni kosa mtafanya basi ni kuwaambia watu wasiende kupiga kura.
 
Safi sana lazima nimpigie kura MTU huyu mwerevu,muungwana anayejali UTU... Sasa Lissu,nyalandu etc wamuunge mkono hats tusiposhinda tumpe tumbojoto pengine atabadilika na kutuskiliza pale tunapomwambia jambo fulani hatulitaki...
 

Kitu ambacho hufahamu ni kuwa cdm ina wapiga kura wa kweli wa upinzani. Kilichotokea uchaguzi wa 2015 kisha Lowassa kuamua kurudi ccm na wale waliokuja naye hakijawaacha wasaka mabadiliko wa kweli na furaha. Leo hii anapotokea mtu wa aina hiyo hiyo, na maneno yale yale, na mtindo ule ule, tena kutoka kule kule, ni wajinga tu wanaweza kukubali hilo.

Kama Lowassa alibanwa akaamua kujisalimisha, huyu yeye ana ushujaa gani? Kama kweli ni shujaa kwanini hakuonyesha huo ushujaa akiwa huko huko ccm? Cdm haihitaji kura hata moja ya Zanzibar, ili kupata ushindi, au uwakilishi mkubwa bungeni. Hatuna muda wa kuokoteza tena mgombea, wakati tuna wagombea wetu. ACT ndio inahitaji mgombea wa aina hiyo lakini sio cdm. Sisi wapiga kura wengi wa cdm tunajua fika tatizo ni tume isiyo huru ya uchaguzi, na sio mgombea wa kuokoteza. Ni vyema kuungana kupigania tume huru ya uchaguzi, na sio kuungana kumpa tapeli nafasi ya kuongoza wapinzani.
 

Yaani suala la kuwa hatutaenda kupiga kura wengi tumeshafanya maamuzi, na impact yake utaiona kwenye huo ushenzi uitwao uchaguzi. Mtu pekee anayeweza kutufanya tujitokeze kwa shingo upande kupiga kura kwa tume hii ya kihuni, ni Tundu Lissu tu.

Wapinzani hatuna muda wa kuendelea kuumizwa, kufanyiwa ukatili, unyama na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi, au mpinzani akipita kwa watu kuumizwa hivyo, bado anunuliwe kwenda kuunga mkono juhudi. Kwa hilo hatuko tayari. Huo unyama, ukatili na uhayawani wa wazi tumeuona kwa macho yetu, tena umekuwa ukiratibiwa na jeshi la polisi na tume ya uchaguzi, kwa maagizo ya jiwe.

Yaani sio wapinzani kukosa hata mbunge mmoja wa upinzani, hata wabunge wa ccm wakiamua kwenda na wake/waume zao ni sawa tu, kwani hata hilo bunge halina chochote cha maana, zaidi ya kupitisha kila atakacho Magufuli. Hilo bunge tunalidharau kuliko uchafu mwingine wowote. Tutatafuta namna nyingine ya kupata viongozi nje ya box la kura lisiloheshimiwa.
 
Anafaa
 
Habari mbaya kwa Tundu Lisu plan B yakev akibwagwa na Chadema imeshazibwa na Membe hatalala Leo Lisu

Pole Lisu hizo ndio siasa.Tulikwambia humu jamii Forums don't overate yourself

Ni hivi, Tundu Lissu ndio chaguo letu wapiga kura wa ukweli wa upinzani. Yaani hata wajichanganye Mbowe, Nyalandu, Membe, Msigwa nk, bado wote kwa pamoja hawana mvuto kwetu wapiga kura wa kweli wa upinzani kama alivyo Lissu. Hivyo Lisu hana lolote la kuogopa maana ana watu wa ukweli nyuma yake. Sana sana Lisu asipopitishwa, ni ahueni kwa Magufuli maana yeye ndio hawezi siasa za ushindani.
 

Simtetei Membe kwa lolote, hebu tuambie Magufuli alijibia wapi zilipo zile 250b za wizara ya ujenzi mpaka akawa rais? Au hizi 1.5t ni wapi alizitolea majibu?
 
Tulisema Tz hakuna Upinzani kuna Ubinafsi ndio kama hivi
Endeleeni kugawana kura

Ubinafsi wa kuungana na Membe, yeye Membe hawezi kugawa hizo kura za ccm?
 
Simtetei Membe kwa lolote, hebu tuambie Magufuli alijibia wapi zilipo zile 250b za wizara ya ujenzi mpaka akawa rais? Au hizi 1.5t ni wapi alizitolea majibu?
Kwa kweli mimi nimeandika kitu mabacho kinajulikana na matokeo yake yako wazi- nenda Lindi ukatafute kiwanda cha sementi kilichokusudiwa na hiyo pesa ya Libya. Ukikiona tueleze. Mahoteli ya Membe huko Lindi na Mtwara ni mazao hiyo pesa za Libya na ile CHENJI YA RADAR ambayo ililengwa kunufaisha shule zetu. Tuonyeshe hayo madaftari na madawati yaliyokusudiwa na hizo pesa za CHENJI YA RADAR1 Hizo za unazozungumzia za Rais Magufuli hebu zitolee maelezo zaidi ili tujue details zake na tuone namna ya kuchangia.
 

Hayo macho uliyoonea wizi wa Membe, ungeyatumia hayo hayo kuona wizi wa Magufuli.
 
Hayo macho uliyoonea wizi wa Membe, ungeyatumia hayo hayo kuona wizi wa Magufuli.
Wewe uliyeuona TUELEZE. Wizi wa Membe una hizo data na facts au mapenzi yana pofusha? Halafu huo uoga wa Rais Magufuli uko wapi?Ni nani, ni Rais gani, ukimwacha Baba wa Taifa, J.K. Nyerere, aliyewakabiri wakoloni na wanyonyaji wa mali na uchumi wetu ANA KWA NA NA MACHO KWA MACHO na kuwaeleza ukweli wa mambo yalivyo.
 
nimependa kuona Membe alipata first class , Mlimani si pa kispoti spoti japo nasi tunazo honours zetu za pale ila first class kiboko!!big up Membe! salute!!

Membe Chukua sera ya ajira , njaa kali na hali ngumu , mikopo bila riba na udhamini, uhuru wa kujieleza na maandamano ukajiuze kwenye kampeni, zako
 
Akapumzike,ACT inafutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…