Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Tulisema Tz hakuna Upinzani kuna Ubinafsi ndio kama hivi
Endeleeni kugawana kura
 
Jiwe hapati kura yangu amemtoa bashite too late, ila membe naye hapana, kurudisha mikataba ya bagamoyo maana yake nini? ile si wachina walikua wanataka kuchukua nchi yetu hivi hivi? yupo serious kweli?

Hamna mtu mwenye uafadhali sasa hivi Tanzania kwa kweli, basi tutampa Lissu tu japo ye naye walewale ila angalau kwa mbali sana. Ningekua nimefikisha umri ningegombea mwenyewe

Ni Wachina na Sultan wa Oman walikuwa wachukue nchi kwa miaka 99, ukanda wote wa pwani ya Tanzania Bara kutoka Moa mpaka Mikindani Mtwara!!! Aibu tupu! Sasa huyo anataka kurudisha nchi kwa Sultan wa Oman chini ya ulinzi wa China!! Upinzani kuchukua nchi ni sawa na kuona mbalamwezi mchana.
 
Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama CHADEMA ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!.

=======


Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:
1962 – 1968:
Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations with Hons, First class, University of Dar es salaam)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law, John Hopkins University Marekani)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia:
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu:
2006 – hadi 2015:
Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – 2015: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amekuwa mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.
#Kazi na bata, tushachoka mikazi tu!
 
Nimecheka kwa sauti ,lol sasa mbona "ningegombea mwenyewe "
Jiwe hapati kura yangu amemtoa bashite too late, ila membe naye hapana, kurudisha mikataba ya bagamoyo maana yake nini? ile si wachina walikua wanataka kuchukua nchi yetu hivi hivi? yupo serious kweli?

Hamna mtu mwenye uafadhali sasa hivi Tanzania kwa kweli, basi tutampa Lissu tu japo ye naye walewale ila angalau kwa mbali sana. Ningekua nimefikisha umri ningegombea mwenyewe
 
Ni Wachina na Sultan wa Oman walikuwa wachukue nchi kwa miaka 99, ukanda wote wa pwani ya Tanzania Bara kutoka Moa mpaka Mikindani Mtwara!!! Aibu tupu! Sasa huyo anataka kurudisha nchi kwa Sultan wa Oman chini ya ulinzi wa China!! Upinzani kuchukua nchi ni sawa na kuona mbalamwezi mchana.
Mzee kajipiga kisu mwenyewe, hii hoja ccm watawekezamo vibayaaaaaa kumshambulia kama agent wa mabeberu
 
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje awamu ya 4, Bernard Kamilius Membe, leo Julai 17, 2020 amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo ambapo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu.
EdIEW6kWAAA4Ek-.jpg
 
1594989034780.png

Kama nilivyosema jana, anataka urais kisa cha kujiunga na ACT, pia nilisema anatamani vyama vyote viungane na kumchagua yeye kuwa mgombea urais, watu kama hawa unawaona ndani nje jinsi walivyo wehu na walafi wa madaraka. 😂😂😂 Alishindwa kupata nafasi CCM alipojaribu kubadilisha muongozo wake wa uteuzi wa wagombea, akaona wajinga wengine watamkubali. Atauza nchi kwa wachina na kujinufaisha yeye na wachache wenzake kama akipata urais.
 
Mhe. Membe chonde chonde usigawanye kura za upinzani wewe unga mkono wapinzani ila usigombee maana ukigombea utagawa kura za upinzani na Magufuli atashinda SAA 4 asubuhi, kuepuka hilo usigombee kabisa
 
Kumekucha
Acha Tuone
Tumchague John Pombe Joseph Magufuli
 
View attachment 1509428
Kama nilivyosema jana, anataka urais kisa cha kujiunga na ACT, pia nilisema anatamani vyama vyote viungane na kumchagua yeye kuwa mgombea urais, watu kama hawa unawaona ndani nje jinsi walivyo wehu na walafi wa madaraka. 😂😂😂 Alishindwa kupata nafasi CCM alipojaribu kubadilisha muongozo wake wa uteuzi wa wagombea, akaona wajinga wengine watamkubali. Atauza nchi kwa wachina na kujinufaisha yeye na wachache wenzake kama akipata urais.
Membe kama Membe peke yake hawezi kitu kwa vile hana wafuasi wowote ukiachilia wale wa kule village kwake.... akisimama peke yake hata yule mzee Rungwe anaweza kumzidi kwa kura.
sema kinakachompa jeuri ni support ya Maalim Seif ambaye ndiye amekwenda na wafuasi wake wengi sama pale ACT.
ACT ni Maalim Seif and Maalim Seif ni ACT. tunaita box office!

ninachokiona kwa upande wa Maalim Seif ni kama kuwapiga pressure Chadema kuharakisha mchakato wa maamuzi yao kwa ajili ya coalition - kwamba "mkiendelea kuchelewa chelewa, walahi tena tutamsimamisha Membe!".
leo hii ikitokea say mtu kama Tundu Lissu arejee nchini na asimame kugombea kupitia Chadema, am sure Maalim atampiga chini Membe fasta.
 
Na mimi mtizamo wangu ni huo huo mkuu,na ukijumlisha na kitendo alichokifanya Lowassa cha kurudi CCM hapo ndipo namna ya watu kumuani Membe inakua changamoto zaidi.
Halafu juu ya ukweli huo mliosema tobias na mng'ato, ni dhahiri kuwa Membe kwa sasa hana pesa ya kuweza "kuwashawishi" na "kuwalainisha viongozi wa CHADEMA au hata wa CUF au hata wa NCCR- Mageuzi eti waungane. Na kama mlimwangalia Membe jana pale ACT -Wananchi, ni wazi alicho kuwa akiwaambia wote ni kwamba - "unganeni na nichagueni mimi Membe nigombee URAIS". Hicho ndicho anachotaka Membe - no more no less! Akili zake zimegota kwenye URAIS ambao hawezi kuupata 2020 au hata 2025. Wekeni kumbukumbu na tutahojiana tena come 2025.
 
Nashauri chadema ikubali kukubaliana na membe ni nini hasa kimenishawishi,membe anajua mengi na mabaya zaidi ambayo serikali imefanya .

Lakini sasa chadema wakidhubutu kufanya hivyo inatakiwa wajipe up too 2035 ili kuwa na kujiimarisha upinzani sahihi .

Otherwise membe anaweza kuwa mtu bora wa kuhakikisha anapambana na ccm.

Binafsi sina chama.
 
Jana wakati anakaribishwa!Aliahidi kujali mishahara ya vyombo vya ulinzi!Nimejiuliza kwa kina kwani kwa sasa hv hali ikoje huko jeshini????Mbona kama hatupo salama???
 
Back
Top Bottom