Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama CHADEMA ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!.

=======


Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:
1962 – 1968:
Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations with Hons, First class, University of Dar es salaam)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law, John Hopkins University Marekani)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia:
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu:
2006 – hadi 2015:
Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – 2015: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – 2015: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amekuwa mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.
Hizo mbwembwe tu za membe ila atambue kwamba Boss wa Dady isbcoming na phd ya maganda ya korosho.
Hajawahi kuwa fisadi
Hajawahi kuwaonea aibu mafisadi
Hajawahi kuwaogopa mafisafi
Hajawahi kuwaonea huruma mafisadi.
Hajawahi kuzurura nje ya nchi
Hajawahi kutoa ahadi sema ile ya Million 50 kila kijiji, mdomo wake uliteleza.
Hajawahi kulazimisha uongoz i.e ubunge kwa maana wapinzani wake walikuwa wanapotea in a thin air kabla hata ya uchaguzi.
Hajawahi kuruhusu wakosoaji wampotezee muda
Hajawahi kuruhusu akili ndogo impe ushauri
Hajawahi kufanya jambo la kufurahisha mahisimu wake kisiasa
Hajawahi kuacha kufanya kampeni za wazwaz
Hajawahi kuacha kugawa pesa mamilion kama peremende
 
Na kuondoa hiyo hofu yako, kama umemfatilia , amewahi kukiri yupo tayar kumuunga mgombea yoyote watakayekubaliana.

Anaweza kusimama, akasimama Lissu, lkn mwisho akaamua kumuunga Lissu... nani anajua???? .


Hapa nilazima wapinzani wakae vzuri wajadiliane.


Kama wasipoungana, CCM haitatikiswa hata kidogo.
Membe kila alicho nacho kwny maisha yake kuanzia kazi yake'ukipepeo',mali zake,kazi nzuri za watoto wake/ndg zake vyote amevipatia CCM na hawezi kwenda kinyume nao hata dakika 1 maana anaelewa 'consequences' zake.

Na Membe ataleta zile Kampeni za kina za kikondoo za kina Lowassa kuogopa kupiga mawe huko alikotoka na tutaishia tu kusema jamaa ana kampeni za kistaarabu.

Mkuu hivi kipindi Zitto anaanzisha ACT akawa anapokea pesa kutoka kwa kina Zoka mpk na a/c Zao na amount zikawa hadharani hukuwahi kufahamau?

Unajua Zoka&Membe hao ni wa kutoka 'ofisi' 1?
 
Usipomwelewa Membe unapata tabu... jamaa anakauli fulani ivi tata... 'Sisi' ... "wenzangu", " kisiki"...... n.k

Kisiki cha mpingo sio yeye tu, fuatilia mahojiano yake na Ulimwemgu, aliweka wazi, Wanaume anaowakubali ....Visiki vya mpingo.


Membe anajua hashindi akisimam, ila anachotaka ni kuwasaidia wapinzani na serikali ione uwezo wake.
Hayo ndio yanakupumbaza?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Dah.. Kweli upinzani una kazi
 
Nihvi sisi mgombea wetu ni lisu tu, huyu jamaa asitake kujikomba komba chadema
 
Mkuu kuungana Ni sawa na inadumisha nguvu Ila tatizo nikuungana na kuwapa watu ambao siyo sahihi kupeperusha bendera ya muungano.
Nikweli kabisa, nahapa ndipo linakuja hitaji lake lakusema ni muda mwafaka wakuzungumza .

Hapa kila upande uwe tayar kuunga juhudi.


LENGO LETU NI MOJAX CCM ITOKE MADARAKANI.

Binafsi hata CCM wafanye nn, natamani sana siku moja WATOKE MADARAKANI.



watanzania wajue, CCM ni adui mkubwa wa maisha yao.
 
Wapinzani ni lazima Tuungane
Waungane vipi wakati baadhi yao wanatembeza bakuli CCM,na wengine wapo upinzani kuvidhofisha?

Upinzani kuishinda CCM inahitajika kwanza CCM wao kwa wao wasambaratishane kikweli kweli.
Siku ukisikia kila mmoja ana amri yake ndio CCM kwishnei.
 
Hiv bila kuitaja chadema angepungukiwa nn?
Mbona bado wana washwa washwa sana na cdm?
Yan ujumbe wake anaona usingekamilika bila kuitaja chadema au ndio alichotumiwa toka huko lumumba?
 
Hayo ndio yanakupumbaza?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Dah.. Kweli upinzani una kazi
Nia ye Membe iko wazi , kwa bahat mbaya ukakasi anaoupata ni kukubalika sababu hamna aujuaye moyo.


Ila ukweli nikua, Membe ni hazina kubwa kwa Upinzani.

Hivi kama CCM lengo ni kuua upinzani ,wangehangaika na haya wanayoendelea nayo et mpaka wamtumie Membe??.


E.Lowassa?? Lowassa alirudi CCM kwa sababu ya Serikali kumuwinda ktk shuguli zake za kiuchumi, kuwindwa kwa waty wake wa karibu.

Nin angefanya??????? ...... kama lengo ilikua nikuua upinzani.. ..haya Lowassa alileta wabunge wangapi??? Kwann asingejitoa kwa kinyang'anyiro siku chache kabla ya uchaguzi???.
Mzee E.Lowassa aliamua kukubali yaishe sababu kwake aliguswa panapouma.



Upinzani usipoungana et kisa Membe... ni kosa kubwa watakalokua wamefanya .

Zanzibar Chadema haipo.. Seif yuko ACT... na wazinzibar siasa zao ni MVUTO WA MTU SIO CHAMA.

Chadema inanguvu Huku Bara.... aya , wasipoungana wanataka nn?????


Mchezo ulikua Lissu wa chadem, Seif wa ACT..

Sasa Kuja kwa Membe kusifanye upinzani utoke nje ya Reli... Nafasi bado ni kubwaa ya kukaaa, Hata Membe mwenyewe anajua .
 
Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!

@BenMembe

CHADEMA Watani zangu bado ' nawakubali ' sana tu na naona ' mkijipanga ' vyema mnaweza ' Kumng'oa ' JPM na CCM yake ila msiungane nao.
 
Sawa
Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!

@BenMembe

CHADEMA Watani zangu bado ' nawakubali ' sana tu na naona ' mkijipanga ' vyema mnaweza ' Kumng'oa ' JPM na CCM yake ila msiungane kabisa.

Tuko makini sisi chadema sidhani ushauri wa L7 una maana sana.
 
Kuungana kwa ajili ya membe hapana........2021 membe anaomba msamaha anarudi ccm wapinzani wanedelea kujipanga
 
Dahh, nina mengi ya kuongea kuhusu usanii huu ila bora niache, kwanini hii mijitu ikifika uchaguzi inakua inahamia upinzani thn lazima kutatokea chama cha upinzani kitakubali kirahisi tu bila ya kufikiria, kwanini siku za uchaguzi tu???????????????!
 
Kama mitandaoni tu Membe hana ushawishi, huko mtaani ataupata kwa nani? Zitto na Mbowe ni watu hatari sana, huenda jamaa nae kachukua mzigo kama Mbowe alivyofanya kwa mzee Lowassa. Hizi tricks katika siasa zinatajirisha sana watu.
 
Rais lazima awe anajua Uchumi!! Membe atosha! Tumeona Uchumi ulivyopiga mweleka kwasababu ya Lubuva kutuwekea MKEMIA.
 
Hahaha mimi sitapiga kura nitakuwa muangalizi wa ndani.
 
Back
Top Bottom