Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,317
- 1,320
N
Nani au mtanzania gani asiyejua Luna ujenzi wa Sgr, ununuzi wa ndege bwawa la umeme n.k mbona kila siku vinarudiwarudiwa na jiwe a.k.a kichaa tena kwa MDA wa miaka Mitano hamuoni! Ila lissu kusema alivyopigwa risasi ndani ya siku kadhaa imekuwa kurudiarudia? Ndio maana nakuambia kama haumwelewi lissu ni uamuzi wako tu wa kijanga ambao hautabadili chochote😁😁😁😁😂😂😂😂Kwa hiyo ndio irudiwe rudiwe mara elfu ndio akili ndogo ielewe... mbona Tanzania nzima inajua tu... na mbona tunakubali pia kwamba alichofanyiwa ni ukatili wa hali ya juu hata kabla yeye kurudi nchini... wanaombeza kutoka kwa moyoni mwao kwa alichofanyiwa, kama hakuna wakati wowote ile roho zao zimewa sumbua, hizo roho haziko hai tena...
Kampeni iendeshwe kama kampeni, mambo ya maendeleo yajadiliwe, na sera zimwagwe... sehemu serikali haijatekeleza ipasavyo, vyama vya upinzani zishikilie pale pale na kutueleza watatatua vipi kero husika za wananchi... na walete mbinu ambazo ni tofauti na za ccm ili hizo akili ndogo ziweze kutathmini njia mbadala za maendelo, kifupi nadharia tofauti... basi! Ndio kampeni yenyewe... kura za huruma usitegemee sana kwa watanzania... kwani wangapi waliingia barabarani wakati alishambuliwa kukemea ukatili huo??? Au tuseme kwamba wanao jazana kwenye mikutano ya Lissu wanakuja kumwona alivyo baada ya tukio lililomtokea?? Wanajua lililotokea, na amesha ongea ya kutosha kuhusu sakata lake hata kabla ya kampeni kuanza rasmi..sasa ni wakati wa kunadi sera na si vinginevyo!! Watanzania mpaka sasa hivi inajulikana wazi tu, asilimia kubwa si wajasiri sana, lakini pia akili yetu ndogo si ndogo kihivyo...