Uchaguzi 2020 Bernard Membe anaongea lugha rahisi na anaeleweka kuliko Lissu

Uchaguzi 2020 Bernard Membe anaongea lugha rahisi na anaeleweka kuliko Lissu

Baada ya kuwasikiliza wagombea wa upinzani ambao tayari wameshaanza kampeni zao, nimejaribu kubainisha tofauti zao, ambapo kwa mtazamo wangu naona Bernard Membe ana uwezo Mkubwa Sana wa kuongelea mambo ya wananchi kwa lugha rahisi na inayoeleweka.

Aliongea kuhusu mazao ya kilimo na changamoto za masoko, wavuvi na changamoto zao, watumishi wa umma na kuporwa mishahara yao kwa lugha rahisi mno. Kwa upande wake Tundu Lissu, ana uwezo mzuri wa kuongea, lakini anaongea kwa jazba, anatumia muda mwingi kuongelea mambo ya haki za binadamu, kumuongelea Dkt. Magufuli na kuongelea jinsi wapinzani walivyofungwa kusumbuliwa na Polisi, alivyopigwa risasi.

Haya mambo hayana impact kubwa kwa wananchi wa kawaida walio wengi. Kwa maoni yangu ajikite kuelezea matatizo yanayogusa watu wote, na jinsi atakavyoyatatua.
Hayo ndio wanyonge walionyongeshwa wanapenda kuyasikia Mkuu. Wangekuwa wanapenda ya Membe na JPM basi Membe naye angepata wafuasi wengi kwenye mikutano wake au JPM asingehitaji Diamond, bendi ya TOT na Harmonize kumjazia watu kwenye mkutano.
 
Mzee wa " a fair coin" . Sio wewe kila ukirusha shilingi ni kichwa tu, kichwa tu, kichwa tu aaaa.
 
Jana aliwaambia wanamanyoni hao wanaowaambia ndege zisinunuliwe sababu nyie hampandi ndege wanawadanganya. Akawaambia madawa yanayotumika yanatoka nje ya nchi, sasa wanataka tutumie bodaboda kuyafata???
Wananchi wakashangilia sana baada kapata elimu ya umuhimu wa ndege
Wewe utakuwa haunatofauti na hao usikute ni illiterate
 
Kuwa CCM usijitoe Ufahamu, hata Mimi ni CCM lakin LISSU anatuumiza kichwa
Jamaa anaongea mambo ambayo wanasiasa wengi hawataki kuyagusia
Britannica
 
Baada ya kuwasikiliza wagombea wa upinzani ambao tayari wameshaanza kampeni zao, nimejaribu kubainisha tofauti zao, ambapo kwa mtazamo wangu naona Bernard Membe ana uwezo Mkubwa Sana wa kuongelea mambo ya wananchi kwa lugha rahisi na inayoeleweka.

Aliongea kuhusu mazao ya kilimo na changamoto za masoko, wavuvi na changamoto zao, watumishi wa umma na kuporwa mishahara yao kwa lugha rahisi mno. Kwa upande wake Tundu Lissu, ana uwezo mzuri wa kuongea, lakini anaongea kwa jazba, anatumia muda mwingi kuongelea mambo ya haki za binadamu, kumuongelea Dkt. Magufuli na kuongelea jinsi wapinzani walivyofungwa kusumbuliwa na Polisi, alivyopigwa risasi.

Haya mambo hayana impact kubwa kwa wananchi wa kawaida walio wengi. Kwa maoni yangu ajikite kuelezea matatizo yanayogusa watu wote, na jinsi atakavyoyatatua.
mwalimu akiwa darasani anafundisha lazima atoe mifano ili somo lake lieleweke. lissu yuko sawa, akisema tz hakuna demokrasia lazima atoe na mifano, akisema hakuna utawala bora lazima atoe mifano. sasa wewe unataka anadi tu sera bila ya kuelezea mapungufu yaliyokuwepo?

tulieni dawa iwaingie kwanza. sisi wananchi ndio tunapenda lissu anavyonadi sera zake
 
Hayo mambo anayoongelea Lissu ni mambo ya msingi kama we unaona haeleweki basi una shida wewe
Hotuba ya Mwanza Lissu kaongea mambo ya msingi sana. Yani kama wewe ni CCM au upinzani, bila kujali chama, ukitumia akili bila ushabiki utaona kwamba kuna vitu vya muhimu kaongea.

Nimeongea sana kuhusu manunuzi ya ndege bila tenda, Lissu kaongelea hilo.

Nimeongea sana kuhusu rekodi ya Magufuli kabla hajawa rais na ambavyo hakusimamia haki, Lissu kaongea hilo.

Kaongea mengi sana, sehemu ya hotuba hii hapa chini.

Kwa hiyo ndio irudiwe rudiwe mara elfu ndio akili ndogo ielewe... mbona Tanzania nzima inajua tu... na mbona tunakubali pia kwamba alichofanyiwa ni ukatili wa hali ya juu hata kabla yeye kurudi nchini... wanaombeza kutoka kwa moyoni mwao kwa alichofanyiwa, kama hakuna wakati wowote ile roho zao zimewa sumbua, hizo roho haziko hai tena...

Kampeni iendeshwe kama kampeni, mambo ya maendeleo yajadiliwe, na sera zimwagwe... sehemu serikali haijatekeleza ipasavyo, vyama vya upinzani zishikilie pale pale na kutueleza watatatua vipi kero husika za wananchi... na walete mbinu ambazo ni tofauti na za ccm ili hizo akili ndogo ziweze kutathmini njia mbadala za maendelo, kifupi nadharia tofauti... basi! Ndio kampeni yenyewe... kura za huruma usitegemee sana kwa watanzania... kwani wangapi waliingia barabarani wakati alishambuliwa kukemea ukatili huo??? Au tuseme kwamba wanao jazana kwenye mikutano ya Lissu wanakuja kumwona alivyo baada ya tukio lililomtokea?? Wanajua lililotokea, na amesha ongea ya kutosha kuhusu sakata lake hata kabla ya kampeni kuanza rasmi..sasa ni wakati wa kunadi sera na si vinginevyo!! Watanzania mpaka sasa hivi inajulikana wazi tu, asilimia kubwa si wajasiri sana, lakini pia akili yetu ndogo si ndogo kihivyo...
As long as hamjajibu nani alitaka kumwua Lissu hilo swali tutawauliza mpaka siku mnaingia kaburini, kama linawakera ni kwa sababu mnajua mnayo hatia
 
HAKUNA MTU ANAYEONGEA LUGHA RAHISI KAMA LISU HAPA DUNIANI KAMA HAUMUELEWI JIULIZE MARA 100% LISSU NI BINADAMU WENYE UZALENDO NA UPENDO MKUBWA SANA KWA TANZANIA (Ukombozi wa MTU au taifa huletwa na MUNGU kupitia mwanadamu ( Wenye akili takatifu tunauona ukombozi kupitia lisu na Amin ndugu nakwambia Huyu LISSU HATOSHINDWA KUKAMILISHA PUNJE NDOGO ILIYOSALIA. CCM MKO NJE YA WAKATI KUBALINI YAISHE😂😂😂😂😂
 
  • Nzuri
Reactions: BAK

Kwa hiyo unahalalisha ushoga na usagaji tanzania sababu babu sea ameachiwa huru au sababu lowasa amerudi CCM?

Sio nyie mlioshangilia 2015 mgombea urais chadema Lowasa aliposema atamwacha huru babu sea?

Au wakati ule ulipinga hilo wazo sababu ulikua CCM?
 
Back
Top Bottom