Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Ile imani ya kumpa uaminifu wetu kama tulivyofanya 2015 kwa Lowassa ndio mtihani.
ACT Wazalendo itabidi mumlaumu Ex wa upinzani aliyetuachia vidonda mpaka kuoenda tena inakuwa ngumu

Leo chama chetu kinampokea rasmi Ndugu Benard Membe ndani ya chama.

Kiongozi wa chama, Ndugu Zitto Kabwe; Mwenyekiti wa Chama Taifa, Ndugu Maalim Seif Sharifu Hamadi; na Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Ado Shaibu na viongozi wengine wa chama wa Bara na Zanzibar wote watawaongoza wanachama kumpokea Ndugu Membe.

Karibu Benard Membe ACT–Wazalendo.
View attachment 1508280
View attachment 1508274View attachment 1508275View attachment 1508276View attachment 1508281View attachment 1508278View attachment 1508279
 
Naona Membe kaamua kuanza kampeni mapema ..... Yohana nafikiri pressure itaanza kupanda....!!
 
Nguvu nilizopoteza kwa kununua kalamu yangu mpya ya "obama" dukani maana tuliambiwa kalamu za tume ya uchaguzi wino wake unayeyuka, siku ya kupiga kula nilitembea kwa miguu km 6 kufika kituoni nilipojiandikisha, siku hiyo daladala hazikuwepo! matokeo yake watu wakaunga mkono juhudi SIWAAMINI TENA WAPINZANI WANAOTOKA CCM, muda wote wanakuwa wapi hadi kipindi cha kuchukua fomu ndio wanachukua kadi?
 
2015 Kwa cdm ya Lowassa ilikuwa fundisho tosha. Kwenye hili la Membe kwenda ACT, muda utakuwa mwalimu mzuri.
Ndiye mgombea wa Chadema huyo Membe jiandae kisaikolojia . Chadema na ACT wanaenda ungana na mgombea wao Membe
 
Membe kaishukuru kamati kuu ya CHADEMA kwa kumpokea baadaye akasema ohh sio nashukuru kamati kuu ya ACT wazalendo!! Anaonyesha keshaongea na kamati kuu ya Chadema na wameshakubaliana sidhani kama kateleza ulimi hapana !!

WAZALENDO na CHADEMA wanaenda kuungana mgombea wao ndio huyu Membe mark my words ndio maana wajumbe wa kamati kuu waliotia nia kugombea chadema wa ndani akina Mbowe wamekimbia ugombea uraisi kiaina!!! kumpisha
Safari hii tutaona kama jamaa yenu atapiga PUSH UP majukwaani .....!!
 
Nguvu nilizopoteza kwa kununua kalamu yangu mpya ya "obama" dukani maana tuliambiwa kalamu za tume ya uchaguzi wino wake unayeyuka, siku ya kupiga kula nilitembea kwa miguu km 6 kufika kituoni nilipojiandikisha, siku hiyo daladala hazikuwepo! matokeo yake watu wakaunga mkono juhudi SIWAAMINI TENA WAPINZANI WANAOTOKA CCM, muda wote wanakuwa wapi hadi kipindi cha kuchukua fomu ndio wanachukua kadi?

Hawa ni mamluki wasiwape nafasi za juu, upinzani unajitosheleza na ni chuo cha kupika wanasiasa ambao ni tegemeo la ccm kupata wanasiasa Bora baada ya chuo Chao cha siasa kufa
 
Ndiye mgombea wa Chadema huyo Membe jiandae kisaikolojia . Chadema na ACT wanaenda ungana na mgombea wao Membe
Pandikizi la ccm Hilo imekula kwake,katumwa kuja kuzigawa kura za upinzani,ACT wasirudie kosa la cdm 2015 wataondoa Imani kwa wananchi
 
Bagamoyo Port expansion itapewa kipaumbele.
[emoji867]
Hili ndo dili lililowaumiza
 
Hujulikani uko wapi , unatoka rondo kama mtoro kuja dar,usafiri unabadilibadili kila sekunde ,nini tatizo?,ukweli hukuweka huru,hebu funguka,

Sasa kampeni utafanyaje kwa hii style?,au unajua kile mlichokua mkikifanya ?,unaogopa kimvuli chake?,najua unajua hakuna mkate mgumu mbele ya chai,kuwa na amani tele
 
Bernard Membe amehama tu Mwili wake kwenda ACT-Wazalendo. Katika hali ya kushangaza amekosea vitu vya msingi kabisa katika hotuba yake. Hii inaashiria kuwa hakujiandaa kisaikolojia kuhamia huko alikokwenda.

Kwanza kabisa ameitaja ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo kuwa ni "UWT" ambao ni Umoja wa Wanawake CCM. Aidha akiwashukuru viongozi wa Chama hicho kumkaribisha, amesema kuwa ni Viongozi wa CHADEMA. Viongozi hao wametabasamu kinafiki tu.

Hii hali itamtesa kwa muda mrefu sana katika maisha yake, kwa sababu anafanya hivyo akidhani anamkomesha mtu fulani, but deeper inside anaamini kuwa hakutakiwa kuwa hapo alipo ambapo siyo mahali sahihi kwake.
Uko sahihi kuwa hakutegeme kuwa hapo alipo. He will adapt to new situations1
 
Jasusi na chama chake wamekuja na mkakati wa kugawa kura za upinzani. duuh sisiem wana mbinu
Mnafanyiwa hivyo sababu ninyi ni manyumbu hamjielewi!

Si mlikuwa mnamshabikia humu kwamba ni jasusi mbobevu? Haya huyo huko kwenu sasa mshabikieni vizuri,,!

Kuna mjinga mmoja alikuwa anasema Membe ndio mgombea wa ccm ni suala la muda tu, sijui anajisikiaje muda huu.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom