Uchaguzi 2020 Bernard Membe hana kabisa mvuto!

Nime screenshot post hii naihifadhi kwa matumizi ya baadae.
 
Hata kelele za ‘twende na Membe’ zimezima sasa.
Hahahaaaa
Yaan binafsi nashangaa likuwa kila kukicha twende na membe
Ila jamaa Hana mvuto kabisa
Angepumzika tu wazeeshane na mkewe
Kwanza maringo yamemzidi
 
Akiwa anaongea unamwona kabisa anatafuta maneno ya kuongea ambayo yatapokelewa kwa shangwe na hadhira yake, lakini wapi!
Sauti yake imefifia sana kama Lowasa tuu. Kwa kweli mmmh, ladha ya kumsikiliza hakuna.
 
Ngumu now kuwa judge wagombea wa upinzani since hata media zinawaogopa..

Charisma ..Lissu Yuko juu hata ya Magufuli.

Magufuli ana advantage ya 'machinery'.. behind
Kuna ugumu gani
Hata macho Kama hayana Basi masikio nayo hayasikii?
 
Yaani huyu amshukuru tu JK, alimfanya akafahamika. Zitto sijui alifikiria nini huyu ndi agombee Urais. Mimi naona amwachie Lissu tu.

Havutii hata kumsikiliza.
 
Yaani huyu amshukuru tu JK ,alimfanya akafahamika. Zitto sijui alifikiria nini huyu ndo agombee Urais.Mimi naona amwachie Lissu tu.
Havutii hata kumsikiliza.

Membe yuko vizuri sana
Na mkianza kumshambulia Mgombea wetu basi tutataka kila mtu ashinde mechi zake

Lissu hamfikii Membe kwa kuongea Issues zinazomgusa mwananchi
Kama mnataka ma MC basi kamchukueni MC pilipili ndo awe mgombea, Sisi tunakwenda na Membe!
 
Ukiona hvyo ujue ndio akili yake ilipofika
Huyu naona hata darasani alifaulu kwa ku piga chabo
Hv kweli ukawashawishi watu wakupe kura Kwa Sababu utawatoa mashehe ndani??
Shida tupu
 
Nadhani hata zitto anajuta Sana ila tu hawezo kukiri hadharani
Anaumia ndani kwa ndani anatamani Oct ifike aondokane na aibu hii hahaha
 
Kama Chadema mnaanza kumshambulia mgombea wetu, basi nendeni na Lissu wenu mkashinde huo uchaguzi sisi tunasonga na Membe wetu tuje tuone!

Kwanza tunahitaji kujikita huku Tanzania bara, we have nothing to lose!

Zanzibar tuna uhakika wa kuingia serikalini ama kwa kushinda au kwa kuingia kwenye serikali ya umoja wa Kitaifa!

Kwa hiyo kila mtu ashinde mechi zake!

Membe tunamkubali, ni smart, anajua kujenga hoja, anajua siasa na yuko sober.

Tunakwenda na Membe!
 
Hahaaaa umnikumbusha mbali sana aiseee
 
Lissu anawatesa sana wa kijani, now mpo kama mmenyeshewa mvua, kila mnapogusa hapashikiki. Mrudisheni Nape, naye kwa sababu kazibuka ataweza kushindana na Lissu. Polepole yeye analialia tu kwenye media.

Kiukweli size ya Lissu sio polepole wala Dr. Bashiru na ukali ukali wake. Sababu zaidi ya mgombea wa CCM wanapaswa kuwepo watu ambao hata kabla mgombea hajapanda jukwaani wawe wameshawapandisha midadi wananchi. Size ya Lissu ni Kikwete, Nape, Kinana, Ole sendeka, labda pia Heri James (napo sina uhakika) nazungumzia msisimko wa jukwaani. Yaani Magufuli sijui aliwaza nini kutuletea Bashiru na polepole 😀

Siasa ni sayansi na ni art vile vile na art hiyo lazima iguse hisia, bwana NN amemention hisia katika moja ya comments zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…