Uchaguzi 2020 Bernard Membe hana kabisa mvuto!

Uchaguzi 2020 Bernard Membe hana kabisa mvuto!

Juzi niliongea na mtumushi wa Mungu akaniambia kuhusu nguvu ya damu...Lissu alivyopigwa risasi Dodoma alipoteza damu yake 40% hadi madaktari bingwa wa Kenya walisema huu ni muujiza kuwa hai...Sasa watu wanaotoa kafara za wanyama na watoto wa kuwazaa hawawezi kumshinda Lissu kwenye ulimwengu wa kiroho maana Lissu katoa damu yake kama Yesu...CCM mwisho wenu umefika damu ya Lissu inaenda kuwakomboa Watanzania kwenye kivuli cha wachawi na washirikina..tafakuri
Nime screenshot post hii naihifadhi kwa matumizi ya baadae.
 
Akiwa anaongea unamwona kabisa anatafuta maneno ya kuongea ambayo yatapokelewa kwa shangwe na hadhira yake, lakini wapi!
Sauti yake imefifia sana kama Lowasa tuu. Kwa kweli mmmh, ladha ya kumsikiliza hakuna.
 
Ngumu now kuwa judge wagombea wa upinzani since hata media zinawaogopa..

Charisma ..Lissu Yuko juu hata ya Magufuli.

Magufuli ana advantage ya 'machinery'.. behind
Kuna ugumu gani
Hata macho Kama hayana Basi masikio nayo hayasikii?
 
Huyu jamaa, hana kabisa mvuto akiwa jukwaani.

Siasa kwake naona si jambo alilonalo kiasili.

Anajitahidi sana kuongea na kudondosha vibwagizo akiwa jukwaani, lakini wapi! Hamna kitu kabisa.

Maneno hayamtoki mdomoni kiulaini. Linganisha Lissu akiwa jukwaani na huyo Membe, ni usiku na mchana.

Sauti haina mvuto. Hana msamiati wa kutosha wa kuchotea vibwagizo kuendana na hadhira iliyo mbele yake.

Anachokiweza ni vijembe vya kimafumbo huko Twitter.


Yaani huyu amshukuru tu JK, alimfanya akafahamika. Zitto sijui alifikiria nini huyu ndi agombee Urais. Mimi naona amwachie Lissu tu.

Havutii hata kumsikiliza.
 
Yaani huyu amshukuru tu JK ,alimfanya akafahamika. Zitto sijui alifikiria nini huyu ndo agombee Urais.Mimi naona amwachie Lissu tu.
Havutii hata kumsikiliza.

Membe yuko vizuri sana
Na mkianza kumshambulia Mgombea wetu basi tutataka kila mtu ashinde mechi zake

Lissu hamfikii Membe kwa kuongea Issues zinazomgusa mwananchi
Kama mnataka ma MC basi kamchukueni MC pilipili ndo awe mgombea, Sisi tunakwenda na Membe!
 
Membe Kama unakumbuka kampeni za kutia Nia CCM mwaka 2015 alikuwa pia akiongea utopolo mtupu, sio kwamba Hana hoja tu, bali Hana ajenda kabisa za maana
Mfano alipokuwa Unguja na Pemba, Jambo analoahidi Ni kuwatoa masheikh wa Uamsho mahabusu
Kati ya changamoto zote za Zanzibar yeye kaona tu Hilo. Hazungumzii hata reforms za mifumo ya kubadilishana wafungwa Kati ya bara na Zanzibar (extradition) ambalo ndio msingi mkuu wa hili la Uamsho
huwezi kusema utaachia watu huru Kama agenda yako kuu,
Ukiona hvyo ujue ndio akili yake ilipofika
Huyu naona hata darasani alifaulu kwa ku piga chabo
Hv kweli ukawashawishi watu wakupe kura Kwa Sababu utawatoa mashehe ndani??
Shida tupu
 
Nadhani hata zitto anajuta Sana ila tu hawezo kukiri hadharani
Anaumia ndani kwa ndani anatamani Oct ifike aondokane na aibu hii hahaha
 
Kama Chadema mnaanza kumshambulia mgombea wetu, basi nendeni na Lissu wenu mkashinde huo uchaguzi sisi tunasonga na Membe wetu tuje tuone!

Kwanza tunahitaji kujikita huku Tanzania bara, we have nothing to lose!

Zanzibar tuna uhakika wa kuingia serikalini ama kwa kushinda au kwa kuingia kwenye serikali ya umoja wa Kitaifa!

Kwa hiyo kila mtu ashinde mechi zake!

Membe tunamkubali, ni smart, anajua kujenga hoja, anajua siasa na yuko sober.

Tunakwenda na Membe!
 
Hahaaaa umnikumbusha mbali sana aiseee
Lowassa ndio hana mpinzani kwa Charisma. Yeye anapanda jukwaani anasema maneno matatu tu Elimu, Elimu, Elimu, ila shughuli yake si mchezo. Charisma yake hadi ilisababisha CCM washindwe kuiba kura Zanzibar, nguvu yote waliweka bara kupambana na mzee wa elimu
 
Lissu anawatesa sana wa kijani, now mpo kama mmenyeshewa mvua, kila mnapogusa hapashikiki. Mrudisheni Nape, naye kwa sababu kazibuka ataweza kushindana na Lissu. Polepole yeye analialia tu kwenye media.

Kiukweli size ya Lissu sio polepole wala Dr. Bashiru na ukali ukali wake. Sababu zaidi ya mgombea wa CCM wanapaswa kuwepo watu ambao hata kabla mgombea hajapanda jukwaani wawe wameshawapandisha midadi wananchi. Size ya Lissu ni Kikwete, Nape, Kinana, Ole sendeka, labda pia Heri James (napo sina uhakika) nazungumzia msisimko wa jukwaani. Yaani Magufuli sijui aliwaza nini kutuletea Bashiru na polepole 😀

Siasa ni sayansi na ni art vile vile na art hiyo lazima iguse hisia, bwana NN amemention hisia katika moja ya comments zake.
 
Back
Top Bottom