Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Hatoki mtu hapa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Septemba 15 kinaanza kimbunga kumbakumba

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Hatoki mtu hapa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Septemba 15 kinaanza kimbunga kumbakumba

Sioni kwanini Membe amuunge mkono Lisu. Hawa watu wa ccm ndio huwa wanavuruga upinzani. Nimefurahi sana yeye kugoma kumuunga mkono Lissu, maana huko mbele ya safari ndio huwa wanaingia kwenye vikao vya siri vya cdm na kujifanya ni washirika wa upinzani, kumbe ni mashushu uchwara wa CCM...
Mkuu hili watu wengi hawajaliona. Lakini Nina imani Chadema wamefurahishwa sana na kauli hii ya Membe maana kama angekubali kujiunga nao wangefanyaje kumkwepa?

Ni sawa una chakula cha kutosha wanao na mgeni unamwambia karibu chakula. Akisema asante endeleeni hurudii tena kumkaribisha zaidi ya kushukuru moyoni.

Asante sana Membe kwa kurahisisha mambo
 
ndio kaandika nini sasa hiki?
IMG_20200908_221556.jpg
 
15 september 2020 October😁😁😁😁 Membe ana mkwara sana
 
Mkuu hili watu wengi hawajaliona. Lakini Nina imani Chadema wamefurahishwa sana na kauli hii ya Membe maana kama angekubali kujiunga nao wangefanyaje kumkwepa?...
Membe kumsapoti Tundu Lissu hadharani ni faida zaidi kwa chadema kuliko kuendelea na kupambania kiti cha uraisi bila kujulikana nia yake hadharani.

Tundu Lissu si mjinga anajua alichokuwa anakitafuta alipozungumza kule Zanz. Anataka wafuasi wa ccm waliopo upinzani watoke mafichoni wawe hadharani au wabaki upinzani wakiunufaisha upinzani. Sasa Rangi halisi ya Bm italazimika kuonekana hadharani baada ya Yale matamshi ya Tundu Lissu.
 
Hapa tatizo ni ruzuku itokanayo na kura za urais. Akijitoa Membe, Chama kitakosa ruzuku ya kutosha.

Kumbuka Act wana uhakika wa kura nyingi Zanzibar, ukijumlisha na chache za bara, itakuwa si haba.
 
Hapa tatizo ni ruzuku itokanayo na kura za urais. Akijitoa Membe, Chama kitakosa ruzuku ya kutosha.

Kumbuka Act wana uhakika wa kura nyingi Zanzibar, ukijumlisha na chache za bara, itakuwa si haba.

Wapiga kura Zanzibar hawavuki laki tano na hawezi kupata zote, hata akipata kura zote Znz + bara ambazo ni chache, hiyo ruzuku inatoka wapi kwa idadi hiyo ndogo?
 
Wapiga kura Zanzibar hawavuki laki tano, na hawezi kupata zote, hata akipata kura zote Znz + bara ambazo ni chache, hiyo ruzuku inatoka wapi kwa idadi hiyo ndogo?

Kwani kuna kikomo cha idadi ya kura za urais ili upate ruzuku?
 
Sioni kwanini Membe amuunge mkono Lisu. Hawa watu wa ccm ndio huwa wanavuruga upinzani. Nimefurahi sana yeye kugoma kumuunga mkono Lissu, maana huko mbele ya safari ndio huwa wanaingia kwenye vikao vya siri vya cdm na kujifanya ni washirika wa upinzani, kumbe ni mashushu uchwara wa CCM.

Mtu kaitumikia CCM zaidi ya miaka 40 leo mnataka awe sehemu ya upinzani!

Hata huko Zanzibar anayeungwa mkono na CHADEMA ni Maalim Seif, kwakuwa ni mpinzani wa kweli na sio chama cha ACT.
Ndio hapo sasa mafanikio yoote aliyopata kwa mgongo wa ccm hawezi kuyasaliti kwa mambo madogo tena ya mateso ktk upinzani
 
Yaani Kachero Mbobezi ambaye alikuwa kiongozi wa taasisi nyeti hiyo unategemea awe mpinzani? Ndiyo maana alijiunga CCM C na CCM B akaunga mkono C. CCM hatuwezi sisi ni Babalao. Mitano Tena kwa Magufuli.
 
Kuna hatihati ya uchaguzi kufanyika kwa awamu mbili kutokana na sababu ambazo haziwezi kuwekwa hapa!
 
Mgombea wa kiti cha urais kupitia ACT wazalendo ameanza kuonja shubili ya kujinadi kisiasa.

Hii imetokea mara tu baada ya kusambaa habari kuwa amekataa kabisa kuungana na cdm ili kumsimamisha mgombea mmoja wa kiti cha urais.

Hapa chini ni moja wapo ya mkutano yake ambapo yupo pekee yake akiwa amezungukwa na bebndera za chama tu.

Tumkumbushe tu kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Screenshot_20200909-133641.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom