Bernard Membe: Nikiapishwa kuwa Rais wa Tanzania viongozi wote wa dini (mashekhe) watarudishwa Zanzibar

Bernard Membe: Nikiapishwa kuwa Rais wa Tanzania viongozi wote wa dini (mashekhe) watarudishwa Zanzibar

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Kauli hii ina maana gani kwamba ni ahadi ya Mh Membe kuwa atakaposhinda kiti cha Urais na kuapishwa basi siku inayo fuata viongozi wa dini watarudishwa Zanzibar.

Hapa anamaanisha mashekhe wa uamsho ama ni viongozi wepi hao?

Na je kurudishwa Zanzibar tu ama kuachiwa huru kabisa mbona ameweka fumbo?


Screenshot_20200809-160846.png

Kauli hiyo ameitoa leo Zanzibar kwenye mapokezi ya viongozi wa ACT wazalendo
IMG_20200809_160858.jpg

Dini itatumika Kama mtaji wa kisiasa kwa Bernad Membe?
 
Waliofungwa kule wapi? Yaaani huyu kweli ndio mmpambanishe na jpm mtegemee ushindi
 
Kauli hii ina maana gani kwamba ni ahadi ya Mh Membe kuwa atakaposhinda kiti cha Urais na kuapishwa basi siku inayo fuata viongozi wa dini watarudishwa Zanzibar....
Hivi Edward hakujaribu hii gear ili apate mtaji?
 
Huyu atamuunga mkokno Lissu au atasimama yeye kama yeye?

Niwe mkweli, sioni haja yoyote ya kuungana mkono, maana huko mbeleni huwa kunazuka tafrani zisizo na sababu yoyote.

Cha muhimu tu wakati wa kampeni vyama hivi visishambuliane kuonyesha vinashindana vyenyewe kwa vyenyewe badala ya kushindana na CCM.

Hayo unayoona huko Zanzibar ni ngome ya Seif, lakini ushindi wa kweli wa CHADEMA uko huku bara. Na kwa upande huu wa bara, cdm ina uungwaji mkono wa kutosha.

Muungano wa Ukawa umewafanya CUF & NCCR kuleta tafrani zenye kuharibu haiba ya CHADEMA, jambo ambalo sio sahihi kujirudia sasa.
 
Hivi Edward hakujaribu hii gear ili apate mtaji?

Lowassa alisema atawaachia akina Babu Seya, Magufuli alipokuwa Rais ikibidi acheze na hiyo ahadi. Hata Mwinyi akiwa Rais itabidi afanye kama alivyoahidi Membe, ili kushusha munkari ya Wazanzibari, kwani ccm haina uwezo wa kushinda kihalali huko Zanzibar.
 
Niwe mkweli, sioni haja yoyote ya kuungana mkono, maana huko mbeleni huwa kunazuka tafrani zisizo na sababu yoyote. Cha muhimu tu wakati wa kampeni vyama hivi visishambuliane kuonyesha vinashindana vyenyewe kwa vyenyewe badala ya kushindana na ccm...
Kura za Lindi na Zanzibar na Kigoma kwa kiasi fulani,zinaweza kutuathiri iwapo hawataungana.
 
Lowassa alisema atawaachia akina Babu Seya, Magufuli alipokuwa rais ikibidi acheze na hiyo ahadi. Hata Mwinyi akiwa rais itabidi afanye kama alivyoahidi Membe, ili kushusha munkari ya Wazanzibari, kwani ccm haina uwezo wa kushinda kihalali huko Zanzibar.
Hata Masheikh pia alisema. Lakini sidhani alifuata ahadi ya Edward bali alifuata vigezo vya board of parole ili kuachia wafungwa.
 
Nadhani kuna maneno hapo Membe either hajayazungumza vizuri, au waliomnukuu ndio hawakumnukuu vizuri.

Hao viongozi wa dini anaowazungumzia naamini ndio wale masheikh wa Uamsho wanaoendelea kushikiliwa kwenye magereza huku bara, hivyo kusema tu atawarudisha Zanzibar hao watu naona haitoshi, angesema atawaachia huru warudi nyumbani.
 
Kauli hii ina maana gani kwamba ni ahadi ya Mh Membe kuwa atakaposhinda kiti cha Urais na kuapishwa basi siku inayo fuata viongozi wa dini watarudishwa Zanzibar...
Yeye ni sehemu kubwa na muhimi ya mfumo iliowaweka ndani watu hao, na pia kwenye majukwaa ya kimataufa alitetea kitendo hicho.
Ameshawaona waislam ni mapopoma siyo!!! Heri angekaa kimya tu!
 
Kura za Lindi na Zanzibar na Kigoma kwa kiasi fulani,zinaweza kutuathiri iwapo hawataungana.

Chadema huwa haina kura maeneo hayo, hata wakiungana. Labda kigoma kwa mbali.
 
Back
Top Bottom