Bernard Membe: Nikiapishwa kuwa Rais wa Tanzania viongozi wote wa dini (mashekhe) watarudishwa Zanzibar

Bernard Membe: Nikiapishwa kuwa Rais wa Tanzania viongozi wote wa dini (mashekhe) watarudishwa Zanzibar

Niwe mkweli, sioni haja yoyote ya kuungana mkono, maana huko mbeleni huwa kunazuka tafrani zisizo na sababu yoyote.

Cha muhimu tu wakati wa kampeni vyama hivi visishambuliane kuonyesha vinashindana vyenyewe kwa vyenyewe badala ya kushindana na CCM.

Hayo unayoona huko Zanzibar ni ngome ya Seif, lakini ushindi wa kweli wa CHADEMA uko huku bara. Na kwa upande huu wa bara, cdm ina uungwaji mkono wa kutosha.

Muungano wa Ukawa umewafanya CUF & NCCR kuleta tafrani zenye kuharibu haiba ya CHADEMA, jambo ambalo sio sahihi kujirudia sasa.
Kila apambane kivyake na kuna ngome,

ACT ambayo imechukua wanachana wengi wa CUF na majeruhi wa kisiasa kutoka CUf ,CCM na Chadema , itakuwa na nguvu pwani na kusini yote pamoja na kanda ya Magharibi kwa bara.

Pia uchaguzi huu udini utatawala sana.
 
Niwe mkweli, sioni haja yoyote ya kuungana mkono, maana huko mbeleni huwa kunazuka tafrani zisizo na sababu yoyote.

Cha muhimu tu wakati wa kampeni vyama hivi visishambuliane kuonyesha vinashindana vyenyewe kwa vyenyewe badala ya kushindana na CCM...
Kura ni rahisi sana kugawanywa kukiwa na picha nyingi za wagombea.
 
Hajui mahitaji ya watanzania huyu,tunataka elimu bora,miundo mbinu mizuri,huduma za afya bora nk.sasa mashehe wanamsaidia vipi mtanzania aliyeko liwale?

Jpm ni bora akatawara milele hadi hiki kizazi za kina lissu na membe kipite
 
Kauli hii ina maana gani kwamba ni ahadi ya Mh Membe kuwa atakaposhinda kiti cha Urais na kuapishwa basi siku inayo fuata viongozi wa dini watarudishwa Zanzibar...
Huo ndio utawala wa sheria wanaojinasibu wataufuata? Ikiwa huyu jamaa au Lissu watashinda nchi hii itaingia katika chokochoko za kidini na kikabila. Unapotaka watu wawe na uhuru usio na mpaka katika kuzungumza kwa kisingizio cha uhuru wa habari na mazingira yetu haya ambapo watu hujazwa jazba kirahisi basi tegemea vurugu za kidini na kikabila.

Mnakumbuka uchochezi uliofanywa huko nyuma kupitia mahubiri ya kidini katika nyumba za ibada na kanda za kaseti yalizaa uvunjaji wa mabucha ya nguruwe huko Kimara, uvunjaji wa makanisa mbagala, kushambuliwa wakristo Zanzibar? Pia uchochezi wa marehemu Mtikila dhidi ya jamii ya kiasia mara baada tu ya mkutano watu waliojazwa chuki wakawashambulia wahindi.

Hawa watu watashindwa uchaguzi na wanajua watashindwa ila watafanya vurugu kwa sababu safari hii wanalazimusha ushindi.

Serikali isimhurumie yeyote atakayejaribu kuleta vurugu.

Uchaguzi sio fursa ya kupokezana madaraka kwa lazima hata kama mtu ameshindwa.
 
Kura ni rahisi sana kugawanywa kukiwa na picha nyingi za wagombea.

Wagombea wako 10+, unategemea zisigawinyike? Lakini yote kwa yote, wagombea wanaoweza kupata zaidi ya kura 1m+ ni wawili tu ambao ni mgombea wa ccm, ambaye anaweza kushinda kihalali au kinyume chake, na mgombea wa Cdm kama hatawekewa mizengwe kutokana na maagizo ya rais aliye madarakani.
 
Siamini Senior wa system kama Membe anafanya Haya hivi kweli anataka Urais au yupo hapo kuhakikisha Wanagawana kura na TAL na yeye kama system kuendeleza utiifu wake kwa Sponsor, Kama membe ni kweli anautaka urais kutoka moyoni tena kupitia ACT basi mzee huyu yupo desperate sana na anahitaji msaada wa haraka sana wakisaikolojia.
 
Hujui hayo yalikuwa makubaliano katika ukawa na pia ni adhma ya Maalim Sefu hadi sasa.
Sasa kama Seif angeshinda Zanzibar alafu Tanzania bara akashinda mgombea wa Ccm mgelitekeleza vipi? Maana wewe umeshupaza shingo Mzee Seif kushinda Zanzibar.
 
Wagombea wako 10+, unategemea zisigawinyike? Lakini yote kwa yote, wagombea wanaoweza kupata zaidi ya kura 1m+ ni wawili tu ambao ni mgombea wa ccm, ambaye anaweza kushinda kihalali au kinyume chake, na mgombea wa Cdm kama hatawekewa mizengwe kutokana na maagizo ya rais aliye madarakani.
Kuna wa tatu ambae yupo pale kuchukua kura za mwingine. Achilia mbali hao 10+
 
Atawarudisha Zanzibar wakiwa huru au atawahamishia magereza ya Zanzibar?

Je na wale maadui zake 12 alioahidi kuwapeleka uhamishoni Kenya itakuwaje?
 
Uko sahihi kabisa, imejionyesha dhahiri bila shaka uwezo wa hivi vyama kuungana haupo, na haya mashinikizo ya kuungana ni ya washabiki ambao hawajui kwa uhakika namna vyama hivi vinavyoendeshwa...
Kuna ukakasi mwingi kwenye hili la kuungana. Hata niliangalia kelele nyingi zaidi za kuungana zaidi ya kutoka kwa mashabiki wa hivyo vyama, lakini pia ni Zitto na ACT yake ndie anaonekana kupigia chapuo zaidi hilo suala, na hata mahojiano yake ya karibuni anaonesha ni kama vile tayari hivyo vyama vimeshakubali kuungana.

Lakini nikiangalia kwa makini kabisa, Zitto anataka kukijenga chama chake huku bara, na hawezi kukijenga peke yake bila mgongo wa Chadema, hivyo anatumia hii nafasi ya kuungana na Chadema ili aweze kupata baadhi ya majimbo huku bara asimamishe wagombea wake, halafu wanachama, mashabiki, na wapenzi wa Chadema wasaidie kwa kiasi kikubwa kumpa ushindi huyo mgombea wa ACT, hiki ndicho Zitto anachokitaka toka Chadema.

Kutatua hii sintofahamu, itabidi idadi ya majimbo watayopeana hivyo vyama upande wa Zanz na Bara iwe sawa, bila kujali ukubwa wa eneo, mtu asiseme kwasababu bara ni kubwa basi apewe majimbo mengi.

Hili nalo lisipoangaliwa kwa makini ndio linaweza kuwa chanzo cha kupeleka majimbo CCM, ni kwa namna gani watawaandaa hao wapiga kura wa Chadema waichague ACT hilo ni jukumu lao.
 
Magufuli aking'oka madarakani nitafurahi na kusheherekea. Ni ngumu kwa kura Ila kwa maombi tu nikumuombea makamu wa Rais awe Rais kabla ya uchaguzi mkuu oktoba kwa mujibu WA Katiba.
Unaweza kufurahi hatukatai, ila mjue tutalia na kusaga meno endapo magufuli hatakuwa rais kwani opp hakuna viongozi ni wahiniwahuni tu
 
Huo ndio utawala wa sheria wanaojinasibu wataufuata?
Ikiwa huyu jamaa au Lissu watashinda nchi hii itaingia katika chokochoko za kidini na kikabila. Unapotaka watu wawe na uhuru usio na mpaka katika kuzungumza kwa kisingizio cha uhuru wa habari na mazingira yetu haya ambapo watu hujazwa jazba kirahisi basi tegemea vurugu za kidini na kikabila...

Sishangai maoni kama haya kutoka kwako. Unaonekana ulishiba itikadi ya siasa chafu za ccm, na huenda ww zamani ndio nyie mlikuwa na mnatembea na Mikanda ya sinema, kwenda kutishia wananchi kuwa vyama vingi vitaleta machafuko kama ya Rwanda. Kwa sababu umeshiba siasa chafu, ndio naona uko hapa kuzitapika.

Toka awamu hii ya Magufuli iingie chaguzi zote ameagiza zinajisiwe, kuanzia za marudio mpaka SM, ulikuwa wapi kuhubiri huu utoto unaoungea hapa? Ama wakati huo chaguzi za kishenzi zikifanyika ulikuwa jela?

Rais alikuwa anaagiza chaguzi zinajisiwe, kisha watu wakichoka kufanyiwa uhuni ndio uje na huu utumbo eti watashindwa kwahiyo wanajiandaa kuleta machafuko? Msiwaingize vyombo vya dola maana mnawalazimisha kuwabeba kwenye ushenzi wenu, kaa ww mbele ili ufurahi hizo dhuluma za kishenzi.
 
Kuna ukakasi mwingi kwenye hili la kuungana. Hata niliangalia kelele nyingi zaidi za kuungana zaidi ya kutoka kwa mashabiki wa hivyo vyama, lakini pia ni Zitto na ACT yake ndie anaonekana kupigia chapuo zaidi hilo suala, na hata mahojiano yake ya karibuni anaonesha ni kama vile tayari hivyo vyama vimeshakubali kuungana...

Nashukuru kwa kuuona ukweli ambao hata mimi nauona wazi. Ukijaribu kumuangalia Zito vizuri, kaungana na Sief ili kupata mtaji wa huko Zanzibar, lakini roho na akili yake yote iko huku bara, na anajua fika wapiga kura wa ukweli wa upinzani, ni wafuasi wa Cdm. Na ni ukweli ulio dhahiri Chadema ina wafuasi wasioyumba kwenye upinzani, na kwa kiasi fulani Zito anajiona ana jasho lake kwenye wafuasi hao wa Cdm. Hivyo Zito anataka sana ushirikiano na cdm, kwani anaijua vyema nguvu hii ya wafuasi wa Cdm.
 
Lakini mbona hawa Mashekh walikamatwa enzi ya yeye akiwa Waziri au? Ni hatua gani alizochukua wakati ule ukizingatia kuwa sheria ya kupambana na ugaidi ilitungwa wakati wake kama waziri wa mambo ya nje?

Kama hii issue nayo ni siasa isiwe tabu, tutamwomba Mh.Rais kama ataona inafaa shauri la Mashekh litizamwe kwa jicho la haki na uwazi.
Ajenda za udini katika siasa ni sumu kali zisizo na tiba.

Sielewi kwanini hakujihusisha mapema kwenye issue ya Viongozi hao wa dini.
 
Back
Top Bottom