mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika ukurasa wake wa Twitter amepakia picha akiwa anatabasamu huku akiwa ameshika Katiba ya chama cha ACT Wazalendo . Je, inaashiria kwamba amehamia katika chama hiki? Ikumbukwe Membe amefukuzwa kwenye chama cha Mapinduzi siku za hivi karibuni.
Amenukuliwa mara kwa mara akitaka kugombea Urais wa JMT.
=====================================Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watamtambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho baada ya kufukuzwa na chama chake cha zamani (CCM).
Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe huku akiwa ameshikilia kitabu cha ACT-Wazalendo.
Kwa muda mrefu sasa Bernard Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM baada ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanahalisi Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho.
Amenukuliwa mara kwa mara akitaka kugombea Urais wa JMT.
=====================================