Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

Kitakachotokea,Membe atauvuruga upinzani kuliko hata lowassa
Anachofanya Membe ni kuwatamanisha wapinzani wamkimbilie,lakini hana mvuto hata rob ya aliokua nao Lowassa
Membe aache taarabu,akachukue fomu hata chausta,ili uchaguzi unoge kama anavyojitapa
 
Miaka zaidi ya 50 Nchi haina maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, hivyo vimaendeleo kidogo ni haki ya watanzania ni pesa zao za walipa kodi siyo Hisani ya CCM, Tanzania ilipaswa iwe ni Nchi tajiri kuliko South Africa na hata America kutokana na kujaliwa neema zote, lakini chini ya CCM hakuna maendeleo na kibaya zaidi badala CCM waongeze maendeleo zaidi wanatumia pesa nyingi kwenye ununuzi wa wabunge madiwani wa upinzani, ni vigumu Taifa kupiga hatua katika mfumo huu wa ajabu uliosalia Duniani.
 
Kuwa na tume mpya ya uchaguzi ambayo inategemewa kuwa huru ita maanisha kufanya marekebisho ya katiba. Hata kama unaweza kusema kwamba muda hautoshi kufanya marekebisho hayo inabidi tu angalie vikwazo vingine ambavyo ni vikubwa zaidi kama vile gharama, usalama wa nchi haswa katika kipindi hiki cha uchaguzi na majidiliano bungeni yasiyo na tija na matokeo chanya. Nafikiri suluhisho ni kufanya tathmini ya tume yetu ya uchaguzi ili ku fahamu kama ina weza kusimamia uchaguzi ulio wa huru na haki tuki wahusisha wahusika wote. Kuhusu wasimamizi wa uchaguzi kutoka nje inabidi tufanye maamuzi kutokana na hali iliyopo. Je tuta ahirisha uchaguzi kwasababu ya wasimamzi kutoka nje ya nchi kuto kuwepo?, Je hali ya Corona nchini itakuwa mbaya sana kiasi cha kuwa zuia wananchi kushiriki kwenye uchaguzi?, Je kuna mikakati yoyote inayo weza ku andaliwa ku walinda wa simamizi dhidi ya Corona katika vituo vyao vya kazi?. Nina jaribu kufikiria njia ya ku hakikisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba uchaguzi utakao fanyika utakuwa wa huru na haki bila wa simamizi kuwepo
 
Yani ndio mnakumbuka tume huru leo na huyo Membe wenu?
Mlipokuwa busy kuanzisha mijadala ya kijinga kama vile rais hajui kingereza, Bashite, tetemeko la kagera na upuuzi mwingine kama huo tuliwaambia huo muda mngeutumia kudai tume huru.
Ona sasa siku hizi mko busy na kigogo eti anatoa siri za Magufuli! Upumbavu mtupu. Na msipoangalia huyo Membe ndio mgombea wenu mwaka huu!

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Mda uliopo unatosha kuunda Tume huru ya uchaguzi wala hawajachelewa kabsa
 
Sio lissu tena?
Le mutuz na cyprian Musiba walilewa Bar wakaropoka kuwa wameambiwa na Naibu Rais Daud Bashite kuwa Tundu lisu akigusa Ardhi ya Tanzania atakamatwa na kufungwa jela kwa miaka mingi kitendo ambacho kinamfanya ashindwe kurejea hapo Dsm.
 
Le mutuz na cyprian Musiba walilewa Bar wakaropoka kuwa wameambiwa na Naibu Rais Daud Bashite kuwa Tundu lisu akigusa Ardhi ya Tanzania atakamatwa na kufungwa jela kwa miaka mingi kitendo ambacho kinamfanya ashindwe kurejea hapo Dsm.
Le mutuz hanywi bia kamanda
 
Hapo ndio ushauri wa Bagonza kuwa sabasaba hii tuandamane kupeleka ujumbe kuwa tunataka tume huru ya uchaguzi unapoonekana wa maana.
Pengine hayo ni maono
Yaani mwezi wa saba huu ndio muandamane? Uchaguzi mwezi wa kumi? Nashauri msusie tu uchaguzi.
 
Upinzani kwa sasa unaweza kuyumba sana na ukawa kama umepotea kabisa but unaweza kuja ku gain momentum hata baada ya miaka 10 ijayo na ukaking'oa chama tawala madarakani......
hizi ni hesabu za nyakati.....
wachache sana wanaweza nielewa.....
Ukweli ndio huo walioko madarakani wanajisahau sana, hata Membe mwenyewe sidhani kama aliwahi fikiria kuwa anaweza kutamka hayo aliyoyatamka leo.
 
Ukweli ndio huo walioko madarakani wanajisahau sana, hata Membe mwenyewe sidhani kama aliwahi fikiria kuwa anaweza kutamka hayo aliyoyatamka leo.
Hawa ni WACHUMIA TUMBO tu. Hawana lolote, wanaangalia maslahi yao tu. Hawana tofauti na wale mnaowaita kwa KI- English - OPPORTUNISTS!
 
Fungu lipi? Lile la CHENJI YA RADA AU LILE LA FEDHA ZA LIBYA YA GADDAFI!? Tueleze vizuri.
Walao la Rada lilifika japo mahakamani. Tunahitaji mjadala na za Gaddafi .huyu mzee atadhani tumesahau walivyokuwa wanaitafuna nchi. Kuna siku serikali nzima ilokiwa inamwagika ughaibuni kufanya kongamano ikiongozwa na Mzee huyu.wanaomfikia wamwambie atupishe la sivyo tutaomba mahakama iunganishe mafuriko kwenye kesi yake na mwanaharakati huru
 
Kuna thread nilianzisha kuhusu namna ambayo rais wetu ame deal na janga la corona.

Kuna wakati tumezungumzia suala la utalii, pamoja na uchaguzi mkuu ujao. Sasa kuhusu watalii, ni wazi kuwa anga letu liko wazi na mipaka yetu kwa watalii kuja nchini. Kiukweli bado hatujaanza kuwaona watalii. Kuna shida hapo kwasababu ya kuficha takwimu zetu na hivyo wao wanachukulia taarifa za balozi zao, vyombo vyao vya habari nk.

Ikiwa hali nikama hiyo kwenye utalii, je wasimamizi kutoka nje watatia timu? Ni wazi sisi maisha ni kama kawaida na corona viongozi wanasema imeisha kwasababu wao ndo wenye hizo takwimu. Sina haja ya kuingia kwenye siasa za rais vs waziri mkuu vs waziri wa afya kuhusu idadi ya wagonjwa. Kwasababu mtaani wananchi wanafahamu ukweli. Hata hivyo wengi wanasema corona hakuna tena!

Je, kama raia wa mataifa hayo hawaruhusiwi kutia timu, je wasimamizi watakuja? Kuhusu waandishi, hao sina shaka watakuja kwasababu hao hata kwenye vita wanaenda kuripoti.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.
 
Uboya huu kudhani hatutaweza fanya uchaguzi eti kwa sababu UNDP hajatoa hela kwa waangalizi wa kimataifa au eti kisa corona uchaguzi utafanyika. Kwani hayo mataifa kama Urusi, Ufaransa, Ujerumani na Marekani huwa wanatuitaga kwenda kuwa waaangalizi wa kimatafa kwenye chaguzi zao?

Kuamin bila wao uchaguzi hauendi ni umbu-umbumbu uliopitiliza.
 
Kwani miaka ya nyuma ulifanyikaje? Hao waangalizi watakuwa bize wanaangalia uchaguzi marekani sis hawatuhusu.
 
Uboya huu kudhani hatutaweza fanya uchaguzi eti kwa sababu UNDP hajatoa hela kwa waangalizi wa kimataifa au eti kisa corona. Uchaguzi utafanyika. Kwani hayo mataifa kama Urusi, Ufaransa, Ujerumani na Marekani huwa wanatuitaga kwenda kuwa waaangalizi wa kimatafa kwenye chaguzi zao?

Kuamin bila wao uchaguzi hauendi ni umbu-umbumbu uliopitiliza.
Kwa hiyo alitaka tuahirishe uchaguz tusubiri wapate hela. Fikiria huyu ndiye rais sasa anaongoza nchi.
 
Tume huru sio tatizo, mtapewa tume huru lakini bado mtalalamika tu. CCM ina wanachama wengi zaidi ya nusu ya watu waliojiandikisha kupiga kura. Wakipiga kura wanachama wote wa CCM kwa mgombea wao CCM itashinda asubuhi tu. Vyama vyenu vya upinzani havina misingi imara. Sera ya CHADEMA ni nini? Je Chadema ni Liberals au conservatives? Je Chadema ni wajamaa au mabepari?

Ukiwa na msingi ni rahisi kuuza sera zako. Chama cha Mapinduzi ni Socialist Conservative. Ndomana wanagawa mambo mengi ya kijamii kwa usawa, kuna elimu bure kwa wote, matibabu bure kwa wote wa aina fulani. Nchi nyingi hazina tume huru kwasababu tume huru zinashawishika. Ni bora tume iwe chini ya muhili mmoja, itafanya kazi vizuri. Marekani hawana independent electoral commission.
 
Back
Top Bottom