Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

JPM alikuwa na kiburi mpaka anafikia hatua ya kuwasema maaskofu mbele ya mimbari wanayotumia kuhubiri kila jumapili na kufanyia ibada takatifu kama sekramenti za mageuzi, alizidiwa na kiburi cha kibinadamu. Na alijijua akawa anawaomba watu wamuombee.

Musiba amerithi tabia zile zile za wajita wa kanda ya ziwa, kujiona wana haki mpaka wanapitiliza. Jeuri huku akisahau kuwa binadamu ana muda mfupi tu juu ya ardhi.
 
Mshauri Musiba aombe msamaha yeye mwenyewe na uache kumlazimisha Membe kukubali msamaha kwa kumtishia eti asipowakubalia maaskofu litamkuta la kumkuta! Basi kama unaona hao maaskofu wana upako huo wacha tuone nani litamkuta la kumkuta.
Hao maaskofu kama wangekuwa wana busara na kwamba wanajua nguvu ya maneno yao basi wangetumia hiyo nguvu ya maneno yao na busara zao kumuonya Musiba au hata kuonesha tu kwamba hawafurahishwi na matusi na kashfa dhidi ya Membe na watu wengine na wanalaani matamshi haramu na mabaya ya Musiba dhidi ya watu wengine,lakini wao walichagua kuwa wanafiki kwa kuogopa kusimamia haki.
Naamini Membe halitamkuta lolote baya bali litamkuta huyo anayetamani baya limkute Membe.
 
Yaani Pascal anaona Musiba amewaheshimisha kwa kuwa na mali alizozipata kama malipo ya kuhamasisha watu wauawe na kuwatukana baadhi ya binadamu wasio na hatia.

Tukiwa na fikra za namna hii ni laana na janga kubwa kwa Taifa. Tutayafurahia hata majambazi yanayotajirika baada ya kupora na kuua watu kwa vile tu kwa kupitia huo uovu, yamekuwa na mali.
Hapa ndo anatuonyesha kwamba wakati ule anajipendekeza kwa mwendazake ili apate teuzi basi ingetokea akapewa hiyo kazi alikuwa anafanya musiba basi naye angejitoa ufahamu vile vile kisha aje kusingizia majini , watanzania tunapenda sana ubinafsi.
 
Kwahiyo unapingana na mahakama iliyomtia hatiani?
Kama hana kosa, nini kinamfanya kuhaha kutuma watu wamuombee msamaha?
Mahakama zinasoma mchezo wa kisiasa uliopo ndio maana jaji mkuu kwenye utawala huu aliwahi kuwaambia mahakimu na majaji kwamba unapotoa hukumu jaribu kutazama mahitaj na matakwai ya utawala uliopo (serikali). Mahakama haziko huru wakiamua vinginevyo wanafukuzwa maana mteuzi ndiye mtawala ambaye anakumbatia visasi kwa sasa kwa kujificha nyuma ya mlango wa demokrasia

You have a lack of wisdom and prudence, that's why you despise the opinions of others with your temporary pride that will make you pay for that rudeness.
 
Wanabodi,

Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipofanya makosa yale, hakuwa yeye, alikuwa ni possessed na demons hivyo kuwa kama kichaa kabisa! ni shetani alikuwa akimiliki na akimtumia!, hivyo baada ya kuombewa, mapepo yamemtoka, ametambua makosa yake, ametubu, ameomba msamaha, as a human being, anastahili msamaha, hivyo natoa wito kwa Bernard Membe, amsamehe tuu mtu huyu, hakujua atendalo!, Ila maadam ameombewa msamaha na Maaskofu, Membe ukikaidi maaskofu...

Mimeandika haya, baada ya kusoma mahali humu kuhusu Tetesi: - Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba.

Duh..., kama mwandishi huyu, ambaye mimi nilimuona kama ni mwandishi kilaza, kanjanja na kichaa kabisa Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma, anamiliki mali kama hizo!, then huyu jamaa ni kichwa sana!. Ametuheshimisha sana, hivyo najiunga na Maaskofu, Membe amsamehe tuu!.

Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu huyu kichaa, ameishajirudi, akili zimemrudia!, amekubali kosa, ametubu dhambi zake kwa viongozi wake wa dini, wanamuomba Membe amsamehe, Membe asamehe tuu.

Kumuombea msamaha kichaa huyu, hakuna maanishi naunga mkono ule ukichaa wake aliokuwa akiufanya!, no!, namuombea msamaha wa kibinaadamu tuu kwa kutambua udhaifu wa binadamu ni viumbe dhaifu na kuna wakati binadamu tunafanya makosa bila kujijua hivyo kujikuta mtu ametenda kosa bila kujua atendalo.

Kila binadamu anastahili a second chance.

Asamehewe.

Paskali
Leo hii na ww unamshauri Membe amsamehe Musiba kweli? Hivi wakati anadhalilisha watu ulikuwa unajickiaje? Mapaka kufikia kuwaita watu mashoga na fedheha chungu nzima. Membe kazia hapo hapo liwe funzo kwa wengine
 
Mahakama zinasoma mchezo wa kisiasa uliopo ndio maana jaji mkuu kwenye utawala huu aliwahi kuwaambia mahakimu na majaji kwamba unapotoa hukumu jaribu kutazama mahitaj na matakwai ya utawala uliopo (serikali). Mahakama haziko huru wakiamua vinginevyo wanafukuzwa maana mteuzi ndiye mtawala ambaye anakumbatia visasi kwa sasa kwa kujificha nyuma ya mlango wa demokrasia


You have a lack of wisdom and prudence, that's why you despise the opinions of others with your temporary pride that will make you pay for that rudeness.
Kwenye specific case ya MUSIBA, matakwa ya watawala ni yep? Kwani hakutukana kweli? Kwani hakutishia watu vifo?

TUWE WAKWELI HATA KAMA UKWELI WENYEWE UTATUUMA
 
Naona ni kama vile Membe yupo katikati, asiposamehe uwezekano wa kulipwa kile kiasi chote cha pesa na Musiba ni mdogo, au awe tayari kulipwa kidogo, unless Membe awe alishafanya uchunguzi juu ya mali anazomiliki Musiba.

Kama Musiba akishindwa kulipa bado itabidi Membe amgaramie Musiba akiwa gerezani, hii yote naiona mitego kwa Membe.
Kumgharamia mfungwa kiasi gani kwa siku?Wasamaria wema tutachanga kwa ajili kumhudumia mpendwa wetu Musiba.
 
Musiba ana akili timamu kabisa hivyo hastahili kuombewa msamaha na yeyote zaidi ya yeye mwenyewe. Mimi pia nitakuwa upande wako na wa wote wanaoshiriki kumuombea msamaha Musiba ikiwa tu Musiba katoka kwake kaenda kupiga goti mbele za Membe kukiri makosa yake na Membe akakataa kutoa msamaha.

Mpaka sasa Musiba anafanya sinema la kuja kusema baadaye alionewa ndio maana hakulazimika kuomba msamaha yaani kwa kifupi kukaidi kwake kumuomba msamaha Membe anamaanisha kwamba hajamkosea Membe na Hana sababu ya kufanya hivyo.

Mimi ni mkristo ila siamini katika kuombewa msamaha kwa mtu aliye timamu kiakili hivyo naisubiri siku msamaha utakapoombwa na Musiba mwenyewe. Kama Makonda alimpigia magoti Mbowe kumuomba msamaha kwa maneno ya Sugu
Na aombe msamaha hadharani asimvizie nyumbani kwake
 
Naona ni kama vile Membe yupo katikati, asiposamehe uwezekano wa kulipwa kile kiasi chote cha pesa na Musiba ni mdogo, au awe tayari kulipwa kidogo, unless Membe awe alishafanya uchunguzi juu ya mali anazomiliki Musiba.

Kama Musiba akishindwa kulipa bado itabidi Membe amgaramie Musiba akiwa gerezani, hii yote naiona mitego kwa Membe.
Sasa membe kumlipia gharama za magereza anashindwa?yaani ni kama 10,000 kwa siku!!
 
Membe alihama chamia pinzani akagombea uraisi kwa tiketi ya ACT wazalendo aliposhindwa akambiwa na jpm aombe msamaha akakataa lakini samia alivyokuwa raisi akaomba msamaha akasamehewa lakini yeye anakataa kuwasamehe wengine.
 

Attachments

  • MaK.jpeg
    MaK.jpeg
    19 KB · Views: 5
Membe alihama chamia pinzani akagombea uraisi kwa tiketi ya ACT wazalendo aliposhindwa akambiwa na jpm aombe msamaha akakataa lakini samia alivyokuwa raisi akaomba msamaha akasamehewa lakini yeye anakataa kuwasamehe wengine.
Hii kampeni yenu ya kijinga Membe hataki, wakati anatukanwa mlikuwa wapi?
 
Pascal Mayalla hanunuliki ninamfahamu tangu kitambo.
Mimi nina idadi ya bahasha alizopokea toka aanze kazi yake, Ni kichaa pekee anayeweza kumtetea Musiba. Musiba aliowasema vibaya vilevile alikuwa akiomba mamlaka ziwachukulie hatua kali sana aliwaombea mabaya yawakute nasi tunamuombea mabaya yamkute kama yeye alivyowaombea wengine.
 
Hapana mkuu kinachompa kiburi Musiba ni hivyo vijisenti vyake sasa dawa ni kuuza hivyo vitegauchumi vyake walau robo tatu akabakiza na robo tu, hapo ndo atatia adabu.
Sijasema asilipie uharibifu aliosababisha Kwa watu wengine akiwemo Membe..

Ni lazima alipe. Kinachoweza kujadilika ni kiwango cha malipo. Na ni wajibu wake yeye mkosaji kukutana na aliyemkosea wazungumze. Ni wazi watapatana tu Kwa sababu Membe naye ni binadamu..
 
Back
Top Bottom