Bernard Membe yupo kweli?

Bernard Membe yupo kweli?

Wewe ni Ngabu kweli, Sisi kwetu Jina Ngabu linamaanisha, ni mtu ambaye Kwa Wakati Fulani, njaa imemshika,bahati Nzuri pengine akakutana na mtu akampatia karanga za kutafuna, Wakati wakiachana tu na huyo mtu aliyemgea karanga, Mbele yake akamwona mtu ambaye naye ananjaa, huyo mtu akataka kuomba karanga Ili ale, matokeo yake aliyeombwa, akaztupia zote mdomoni mwake akimwambia Yule jamaa aliyeomba kuwa, nimemaliza karanga na mdomo umejaa karanga asiweze hata kuongea vizuri, hiyo ndio inaitwa amezi Ngabu
😁😁
 
Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.

Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!

La hasha.

Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.

Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.

Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....

Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?

Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.

Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!

Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.
Unataka kujua alipo ili umfanye nini wewe gamba?
 
Hapo kumbuka vyombo vya habari vimepigwa marufuku ku-cover matukio ya TL.
Kabisa!

Ila hao watawala nao ni wapumbavu tu.

Katika zama hizi ni kazi bure kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza habari.
Hakika ni lawama batili kwa Serikali kwa hilo. Labda wanaotoa shutuma hizo wanafanya hivyo kwa makusudi kuifitinisha Serikali na wananchi kupitia mgongo wa vyombo vya habari.

Wanajua wazi kampeni hazijaanza ila ni wakati wa kutafuta wadhamini. Huyo anayefanya mikutano ya hadhara anafanya makusudi achukuliwe hatua ili apate kutafuta huruma ndani na nje ya nchi. Tufanye subira kampeni zianze rasmi.
 
Huyo jasusi bado hajaonja joto ya jiwe ya kuwa upinzani!

Siku atayopewa msukosuko atarudi mwenyewe CCM bila kupenda.

Membe hawezi kurudi.

CCM walimfukuza.

Zaidi alitukanwa na vijana wadogo wa CCM ambao angeweza kuwazaa.
 
Hakika ni lawama batili kwa Serikali kwa hilo. Labda wanaotoa shutuma hizo wanafanya hivyo kwa makusudi kuifitinisha Serikali na wananchi kupitia mgongo wa vyombo vya habari.

Wanajua wazi kampeni hazijaanza ila ni wakati wa kutafuta wadhamini. Huyo anayefanya mikutano ya hadhara anafanya makusudi achukuliwe hatua ili apate kutafuta huruma ndani na nje ya nchi. Tufanye subira kampeni zianze rasmi.

Mbona JPM amekuwa akifanya hayo kwa miaka minne sasa?

Na amekuwa akipita ktk majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kuwaponda na kuwachonganisha na wapiga kura wao.
 
Sawa mkuu lakini kumbuka bila haki hakuna amani. Kuimba amani kila siku TBC wakati walioko kwenye madaraka wanabana haki za watu ni upumbavu.
Hakika ni lawama batili kwa Serikali kwa hilo. Labda wanaotoa shutuma hizo wanafanya hivyo kwa makusudi kuifitinisha Serikali na wananchi kupitia mgongo wa vyombo vya habari.

Wanajua wazi kampeni hazijaanza ila ni wakati wa kutafuta wadhamini. Huyo anayefanya mikutano ya hadhara anafanya makusudi achukuliwe hatua ili apate kutafuta huruma ndani na nje ya nchi. Tufanye subira kampeni zianze rasmi.
 
Membe anaweka maslahi ya Taifa mbele siyo yake binafsi

Na hakuna maslahi makubwa kwa nchi zaidi ya kusaidia juhudi za kumng'oa Magufuli madarakani october 28 ,maana Magufuli ni sehemu kubwa ya kikwazo cha maendeleo ya kweli nchini hususan kwenye suala la fundamental freedoms za wananchi!

Kwa hiyo Membe yuko behind the scene anafanya hiyo kazi kwa weledi mkubwa sana
Membe ni Lowassa part 2 yule.
 
Back
Top Bottom