Leo nimeumia sana pale Uwanja wa Taifa.
Nimeamini Lugha(English) ni tatizo kubwa kwetu Watanzania! Kuna wanaijeria walifika pale, mlango wa kuwasikl (Arrival) wakitaka kuingia ndani!
Wale jamaa wakafosi kuingia kupitia mlango ule bila kukaguliwa, sasa kwakuwa wao wanajua English, na pale wenzangu (walinzi hawajui) lugha, ikawa lugha gongana!
Jamaa wakawa wanatukana tena kwa ubabe, mwisho wa siku wakaingia bila kukaguliwa!
Nilicho observe pale mpaka wao kuingia kibabe, ilikuwa ufahamu finyu wa lugha kwa wenzetu!
Hakika watanzania itatuchukua muda mrefu sana katika soko la ushindani kimataifa, na tatizo kuu ikiwa ni Lugha.
Morison, anacheza na akiki ya hizi timu sababu kuu ni exposure aliyonayo!