best maandazi recipe

Kuumua hamira kabla pia inafanya maandazi yako yasinuke hamira na kutofanya vidoto vyeusi ikiwa umezidisha hamira...


Kama ivo poa coz sipendi harufu ya hamira mara nyingi natumia baking powder
 

kumbe kula jikoni ndo kunakufanya unisubirishe chamber?
 
Mwenzio sipendi harufu ya hamira kabisaaaaaa.

Tena napenda maandazi ya kimombasa ambayo hayajajaa unga ndani. Yaani kunakuwa empty halafu hayana harufu ya hamira.

Wanakula asubuhi na mbaazi.

Hapo umetulia zako unasubiri Tahmeed ujirudie Bongo Daslaam.

Kudaadeki.
 
Hayo yawe motoo ooo sinia linaishia jikoni. ...mi hupendelea na katles za samaki/kuku....nitashibaje?
 

Mm linone kabisaa nyama ndani ilimradi liive. Hapo nitahisi nakula andazi!! Na mate yalee yanatrremka kooni..lol
 

Andazi kwa maharage linapendeza pia.
 
Hayo ya kubake tunaitaga ya kipemba/kupambia...
Upembani yanaokwa na mkaa huzidi utamu naona!!

Yeah yanakua matamu basi mie nafkiri yale yanayosukwa ndo yanaitwa ya kupambia...unajua hata mishkaki ya kuchomwa na mkaa na ya kuchomwa na grill ni tofauti utamu ya mkaa inakua mitamu zaidi....
 
Pia mazuri ukiya bake unaweka ufuta juu

Farkhina nieleweshe vizuri nikamsapraizi mama watoto, nini tofauti ya samli na siagi. Nipe kipimo cha maji na tui la nazi maana haya mambo ya jikoni yamenipita kushoto kidogo.
 

Ha ha haaaaaaaa. Wazee wetu hao. Ndo mpk leo yanakusaidia maskin
 
Ahsanta habibty. Vp haya yanafaa kuweka ile bizari tam? Mana mi napenda kuweka bizari tam yanakua yana ladha nzuri.
 
Farkhina nieleweshe vizuri nikamsapraizi mama watoto, nini tofauti ya samli na siagi. Nipe kipimo cha maji na tui la nazi maana haya mambo ya jikoni yamenipita kushoto kidogo.

Namsaidia. Siagi ni margarine/butter ile tunapaka kwenye mikate ya slices. Samli ghee ni ile tunatumia kupikia hata kwenye vitu vya kukarangiza pia tunatumia kama. Mfano wa samli ni aseel, cowboy, tanband kismayuu n.k.

Kuh tui la nazi au maji, ni makisii tu coz unakanda na dough yako iwe kiasi kama inavokua ya chapati. Kwa kuongezea atakuja mwenyewe chief cook farkhina
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…