best maandazi recipe

best maandazi recipe

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Wapendwa leo niliandaa maandazi matamu balaa haya nlitumia hivi vipimo....jaribu na wewe uje uniambie kama hutashibia jikoni

Mahitaji

Unga kg 1

Sukari robo ila usijae

Samli 5 tablespoon + I tablespoon ya siagi (unaweka kwa sufuria inakua yamoto) siagi ni kwa ajili ya ladha nzur zaid

Hiliki 1teaspoon

Tui la nazi

Yai 1

Hamira 1 tablespoon

Mafuta ya kukaangia maandaz

Namna ya kutaarisha

Kwanza kabisa weka tui robo kikombe add sukar 1tablespoon na hamira (hiki ni hatua ya kuumua hamira na kuitizama kama bado ipo active ili usije haribu upishi wako kama itakua imeshapita mda) itafanya bubbles kwahiyo bado ipo active

Weka unga changanya na sukar na hiliki...changanya vizur

Mimina samli yamoto kiasi kwenye unga..changanya kwa mikono safi

Mimina hamira ulioumua

Weka yai then tui

Kanda hadi iwe laini...

Subiria 30 minutes iumuke

Katakata maandfazi yako

Acha yaumuke

Weka karai mafuta yakipata moto kaanga hadi yawe brown..

Maandazi tayar kwa kuliwa.
 
Maandazi

1400028988763.jpg
 
Thanks for whetting my appetite. I haven't had them in a long time and it's about time now.

Mi huwa napenda kuyakata katikati halafu napaka red plum jam.

Ya hivyo naweza kumaliza hata kisadolini kizima!
 
Asante farkhina sasa bado nakula mtori next week ntayaandaa haya..nilikuomba receipe ya half cake laini tamu ukanibania farkhina.mwenzio nikipika huwa hazilainiki na ninazipenda kweli.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
asante farkhina sasa bado nakula mtori next week ntayaandaa haya..nilikuomba receipe ya half cake laini tamu ukanibania farkhina.mwenzio nikipika huwa hazilainiki na ninazipenda kweli..

Sijakubania mbona niliweka kule
 
***Halfcake***

Mahitaji

Unga nusu

Maziwa/maji

Yai 1

Sukar vijiko 6 vya kulia

Baking powder 2 teaspoon

Zafaran (yellow food coliring)

Tangawizi ya unga 1 tablesppon

Vanilla powder 1 teaspoon au vanilla ya maji (arki)

Mdalasini 1/2 teaspoon

Hiliki 1/2 teaspoon

Mafuta kwa ajili ya kukaangia

Pinch of salt

Siagi 1 tablespoon

Namna ya kutaarisha

Changanya dry ingredients zote (unga,mdalasini,sukar,chumvi,h iliki,baking powder)

Vunja yai then weka katika dry ingredient....weka siagi changanya vizuri

Weka maziwa then changanya vizuri hadi utengeze donge moja

Kanda hadi iwe laini...subiria for 30 minutes

Katakata halfcakes kutokana na shape unayopenda...

Weka karai jikoni then kaanga hadi ziwive

Tayari kwa kuliwa
 
ameline hipo apo juu recipe hope u r happy now...vipi vibinti wazuri wanaendeleaje?
 
Last edited by a moderator:
Farkhina yaani mie bila kuona picha sijaridhikaaa....

Pls weka picha ili niigizie .
 
Thanks for whetting my appetite. I haven't had them in a long time and it's about time now.

Mi huwa napenda kuyakata katikati halafu napaka red plum jam.

Ya hivyo naweza kumaliza hata kisadolini kizima!

Mie hupenda kula na soup ya kuku na chai ya maziwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Best umesahau kuweka hatua ya kuchanganya hamira. mdogo wangu Eiyer atapika bila kutia hamira hapo lol. na utukumbushe kuweka samli ya moto kabla hatujaweka hamira kusudi isife nguvu.

asante mamito, hadi likizo iishe mmh! maandazi na mie huwa nashibia jikoni, lol
 
Heee usinikumbushe hiyo ya kupika maandazi bila hamira....nliwahi pigwa kofi la haja nlipika maandazi wakati wa kusubiri kuumuka hayaumuki kumbe nlisahau hamira weee ilikua kesi si ndogo maskini mama angu lile kofi alonipiga hadi leo sisahau kutia andazi hamira....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom