Betting ilivyokwenda na milion moja yangu

Leo nimepigwa fimbo hadi nikakimbilia huku nako ni fimbo tu
 
Attachments

  • 732AEF72-15F9-42DF-AF2C-A99202020CB9.png
    732AEF72-15F9-42DF-AF2C-A99202020CB9.png
    315.2 KB · Views: 19
  • 4DA2FC34-049C-4EE4-B341-9C859D2CCBDC.png
    4DA2FC34-049C-4EE4-B341-9C859D2CCBDC.png
    303.2 KB · Views: 22
Huku nikampa bekstas huku nikampa city
 
Attachments

  • 6E725335-0761-47B8-8227-35E2124686C6.png
    6E725335-0761-47B8-8227-35E2124686C6.png
    749.7 KB · Views: 21
  • 68E23AA6-90A3-4D3C-871C-9C3A345E1F09.png
    68E23AA6-90A3-4D3C-871C-9C3A345E1F09.png
    712.1 KB · Views: 17
Hakuna cha skills wala strategic, makampuni tuu ya kupredict ambao wanafanya critical analyize ya match hisika wanakula za uso…

Huwez kuweka strategic cjui skill kwny match ambayo ww huchezi, wala sio coach… tena kwny current situation ambayo condition ya uwanja, utimamu wa wachezaji na mipango ya bench la ufundi huijui…

Ww n mbahatishaji km wabahatishaji wengine…
Leo city kafa, arsenal kafa, na yanga kafa pia… hapo unachomokaje labda mr betting
Kaka unayosema ni kweli 🤣🤣🤣🤣😍asante kwa kunirekebisha apo kwa man city umeongea
Vijana tufanye kazi mali ipo shambani
 
Wakati fulani miaka kadhaa iliyopita, niliweka dau langu kubwa zaidi kwenye betting 1,000,000 TZS kwenye option ya draw kwenye mechi tatu tofauti.

Nilijiamini sana kwamba hii ilikuwa tiketi yangu ya ushindi mkubwa. Mechi mbili zilitoka tofauti kabisa na nilivyotarajia, na ndani ya dakika chache, mkeka wangu wote ulikuwa umetoweka. Hilo lilikuwa pigo kubwa si kwa sababu tu ya kupoteza pesa nyingi, bali pia kwa sababu ya hisia za kutokuwa na uwezo wa kudhibiti matokeo.View attachment 3123834

Lakini unajua nini? Nilijifunza kitu kikubwa siku hiyo.

Potevu la pesa halikuwa mwisho wa safari yangu. Hakuna aliyeanza kufanikiwa kwenye betting bila kupitia changamoto kama hizi. Hii ni sehemu ya mchezo, na jambo muhimu ni jinsi unavyojifunza kutokana na kila dau – la kushinda na la kupoteza.

Baada ya tukio hilo, nilijifunza kuwa NIDHAMU ni kila kitu. Nilianza kubeti kwa mipango, kutumia pesa ambazo nimezipanga kwa ajili ya burudani, na si kwa shinikizo. Pia, niliweka malengo ya muda mrefu na kuepuka kurudia makosa yale yale.

Wengi wetu tunapitia hali kama hizi lakini kama wewe unavyofahamu, hatujifunzi kwa kushinda pekee. Tunakua kwa kushindwa. Kila tiketi inayochanika inatufundisha jambo jipya.

🔑 Somo: Betting siyo njia ya kupata pesa haraka inahitaji uelewa, mipango, na nidhamu. Ukiweka bidii na ukajifunza kutokana na makosa yako, utapata mafanikio ya muda mrefu.

Soma Pia: Betting ni mchezo unaoweza kukuletea umasikini hata kukuua!

Kwa hiyo, ushindi na hasara ni sehemu ya safari yetu. Jifunze kutokana na kila hatua, na hakikisha unakuwa na mtazamo wa muda mrefu. Hata wakati unaposhindwa, bado unakuwa mshindi kama unajifunza kitu kipya.

Je, wewe una stori yako ya kupoteza au kushinda? Hebu tushirikishe hapa!

Updates Nimesoma comment nyingi zinadai kuwa yawezekana niliuziwa Mechi na wale jamaa wa Fixed,naomba niwajibu hapa sijawai kufanya huo upuuzi iko hivi nimeanza kubet miaka sio mengi wakati wa kombe la dunia linacheza kitu ambacho kilinifanya niweke Milioni tayari nilikuwa nimeshakula zaidi ya Milioni 6 kwa siku 2 tu tena kwa option ya draw kipindi hicho kampuni ya Gwala Bet inaanza wenzangu na mimi nadhani mnakumbuka Gwala Bet ilikuwa inatoa 500 Free bet kila siku.

Nikaona hawa wazee wana kiasi kidogo cha ushindi 20M max,acha niende betpawa nikazipige hela sio kwamba nilikurupuka hapana kawaida uwa nina strategy zangu kwenye draw haikuwa bahati ila baada ya muda si mrefu niliirudisha kwa option ya draw pia.

Hadi mtaa wakaniita Mturutumbi maana ili sio jina langu harisi ila niwambie tu bet sio nzuri maana kuna muda mambo yanagoma kabisa
Ushahidi wa kuliwa umeweka,, Ushahidi wa kula million 6 kwa siku mbili hujaweka…

Naona umeamua kutuchemshia chai ya Magadi sio?
 
Alafu utasikia kunatangazo Lao kwny redio mdada kala million 50 aviator…..

Ukiuliza ushahidi ukwapi? wanakimbia kimbia tuu, kudadadeki…
Watu wanakula ila usijaribu aviator ya betpawa mimi kule nimeamua kua nacheza jackpot tu ya shilingi mia nikipata haya leo kanifuta machozi 75k kwa 100 pesa nzuri sana
 
Attachments

  • 598B1E28-11E5-4DD9-84E4-46F2EA1F5320.png
    598B1E28-11E5-4DD9-84E4-46F2EA1F5320.png
    187.3 KB · Views: 14
Alafu utasikia kunatangazo Lao kwny redio mdada kala million 50 aviator…..

Ukiuliza ushahidi ukwapi? wanakimbia kimbia tuu, kudadadeki…
"Weka hela hapa, kindege kitapaa weee halafu utapata pesa nyingi" Halafu kweli mtu anaweka.
 
Betting sio kazi nimefanya forex nikaacha. Betting na forex zinataka watu wenye uhakika wa kula na kuishi yaani wanaiweza kusaidia wengine. Just imagine hapo ukiwa na njaa utaona 2m ni nyingi so hutokaa uweze kusubiri mkeka ushinde mamilioni same to forex inahitaji kuweka order unayomudu kupoteza! Ni mtazamo wangu ata mimi sometimes naweza kuona Bora kuchukua 1m nayoiona kuliko kusubiri 40m hahaha 🤣 🤣 🤣
 
Attachments

  • IMG_20241026_120553.jpg
    IMG_20241026_120553.jpg
    751 KB · Views: 14
  • IMG_20241026_120640.jpg
    IMG_20241026_120640.jpg
    696.5 KB · Views: 17
  • Screenshot_20241111_034114.jpg
    Screenshot_20241111_034114.jpg
    200 KB · Views: 14
Nilichoshangaa Korea na Japan wanaobeti ni wazee kuanzia 55+ nimeingia betting clubs vijana wanahesabika tena ni above 35 na wanamaisha wanajua nini wanafanya na sehemu za betting zina ulinzi mkali kuzidi ata Bank 🏧.

Kwa mtazamo wangu betting ingefanywa kuwa mchezo wa MATAJIRI na wasomi kuanzia Masters mtu wa Degree kurudi chini asiruhusiwe kabisa kufanya Forex. Akipatikana afungwe miezi 3 na viboko 12 wakati anatoka jela... Natania ila ni kama kweli vile .....hapa namanisha jobless na wengineo wasio na uhakika wa kula wasiruhusiwe kufanya betting au Forex.

Nchi masikini kuruhusu betting kwa raia wake ni kuwaonea kabisa naona ni kama kutokujali wananchi wa hali ya chini. Wanakuwa wanapoteza nguvu kazi na kuwa na urahibu/ addiction bila sababu ya msingi.

Betting zingefashwa kuwa huduma za anasa kama kwenda kunywa chai kempsky au Serena hotel wakati uwezo hauruhusu.
 
Wakati fulani miaka kadhaa iliyopita, niliweka dau langu kubwa zaidi kwenye betting 1,000,000 TZS kwenye option ya draw kwenye mechi tatu tofauti.

Nilijiamini sana kwamba hii ilikuwa tiketi yangu ya ushindi mkubwa. Mechi mbili zilitoka tofauti kabisa na nilivyotarajia, na ndani ya dakika chache, mkeka wangu wote ulikuwa umetoweka. Hilo lilikuwa pigo kubwa si kwa sababu tu ya kupoteza pesa nyingi, bali pia kwa sababu ya hisia za kutokuwa na uwezo wa kudhibiti matokeo.View attachment 3123834

Lakini unajua nini? Nilijifunza kitu kikubwa siku hiyo.

Potevu la pesa halikuwa mwisho wa safari yangu. Hakuna aliyeanza kufanikiwa kwenye betting bila kupitia changamoto kama hizi. Hii ni sehemu ya mchezo, na jambo muhimu ni jinsi unavyojifunza kutokana na kila dau – la kushinda na la kupoteza.

Baada ya tukio hilo, nilijifunza kuwa NIDHAMU ni kila kitu. Nilianza kubeti kwa mipango, kutumia pesa ambazo nimezipanga kwa ajili ya burudani, na si kwa shinikizo. Pia, niliweka malengo ya muda mrefu na kuepuka kurudia makosa yale yale.

Wengi wetu tunapitia hali kama hizi lakini kama wewe unavyofahamu, hatujifunzi kwa kushinda pekee. Tunakua kwa kushindwa. Kila tiketi inayochanika inatufundisha jambo jipya.

🔑 Somo: Betting siyo njia ya kupata pesa haraka inahitaji uelewa, mipango, na nidhamu. Ukiweka bidii na ukajifunza kutokana na makosa yako, utapata mafanikio ya muda mrefu.

Soma Pia: Betting ni mchezo unaoweza kukuletea umasikini hata kukuua!

Kwa hiyo, ushindi na hasara ni sehemu ya safari yetu. Jifunze kutokana na kila hatua, na hakikisha unakuwa na mtazamo wa muda mrefu. Hata wakati unaposhindwa, bado unakuwa mshindi kama unajifunza kitu kipya.

Je, wewe una stori yako ya kupoteza au kushinda? Hebu tushirikishe hapa!

Updates Nimesoma comment nyingi zinadai kuwa yawezekana niliuziwa Mechi na wale jamaa wa Fixed,naomba niwajibu hapa sijawai kufanya huo upuuzi iko hivi nimeanza kubet miaka sio mengi wakati wa kombe la dunia linacheza kitu ambacho kilinifanya niweke Milioni tayari nilikuwa nimeshakula zaidi ya Milioni 6 kwa siku 2 tu tena kwa option ya draw kipindi hicho kampuni ya Gwala Bet inaanza wenzangu na mimi nadhani mnakumbuka Gwala Bet ilikuwa inatoa 500 Free bet kila siku.

Nikaona hawa wazee wana kiasi kidogo cha ushindi 20M max,acha niende betpawa nikazipige hela sio kwamba nilikurupuka hapana kawaida uwa nina strategy zangu kwenye draw haikuwa bahati ila baada ya muda si mrefu niliirudisha kwa option ya draw pia.

Hadi mtaa wakaniita Mturutumbi maana ili sio jina langu harisi ila niwambie tu bet sio nzuri maana kuna muda mambo yanagoma kabisa
Pole sna mkuu. Lakini inaonekana bado wewe ni mchanga sana kwenye betting. Ukishinda mkeka huwa unajiona unajua sana wakati ushindi kwenye betting ni bahati zaidi kwani hata Yanga ambao unaweza kuwaamini na kuwatilia dau la 10M nao pia hufungwa na timu ndogo kabisa. Hata juzi Man City katoka kupigwa na timu ndogo.

Mkuu Mturutumbi255 (mchawi) unaposhinda mkeka, huo ndio wakati wa kukaa chini na kutulia ubet kwa uhakika zaidi na kwa dau dogo. Sio wakati wa kukimbilia kubet kwa dau kubwa ukijiona unajua kubet au kwa kuwa umepata pesa nyingi. You will end up losing everything. Anyway, only bet waht you can afford to lose.
 
Watu mna mioyo migumu sana. Unaweka Milioni unabet draw?? tena mechi tatu?? aise! bora ungeweka double chance au hata over/under ungeambulia chochote
 
Mi nkiweka million , option ambayo haitonipa stress sana ni over 0.5 , ntasubiri goli upande wowote ule dakika 90 , wakitoka 0-0 basi nakubali nmeliwa , mi naona ukistake high acha tamaa Bora uweke ata odd 1 uweke million upate laki mpka laki 5 au uweke odds 2 tu upate faida sawa na stake Yako, option salama ni over 0.5 au ukilipuka sana mwisho over 1.5( NB hakuna option isiyochana, unajaribu tu kuminimize risk , ni Bora kusubiri goli upande wowote ule kuliko kusubiri mtu ashinde au asifungwe 🙌
 
Wakati fulani miaka kadhaa iliyopita, niliweka dau langu kubwa zaidi kwenye betting 1,000,000 TZS kwenye option ya draw kwenye mechi tatu tofauti.

Nilijiamini sana kwamba hii ilikuwa tiketi yangu ya ushindi mkubwa. Mechi mbili zilitoka tofauti kabisa na nilivyotarajia, na ndani ya dakika chache, mkeka wangu wote ulikuwa umetoweka. Hilo lilikuwa pigo kubwa si kwa sababu tu ya kupoteza pesa nyingi, bali pia kwa sababu ya hisia za kutokuwa na uwezo wa kudhibiti matokeo.View attachment 3123834

Lakini unajua nini? Nilijifunza kitu kikubwa siku hiyo.

Potevu la pesa halikuwa mwisho wa safari yangu. Hakuna aliyeanza kufanikiwa kwenye betting bila kupitia changamoto kama hizi. Hii ni sehemu ya mchezo, na jambo muhimu ni jinsi unavyojifunza kutokana na kila dau – la kushinda na la kupoteza.

Baada ya tukio hilo, nilijifunza kuwa NIDHAMU ni kila kitu. Nilianza kubeti kwa mipango, kutumia pesa ambazo nimezipanga kwa ajili ya burudani, na si kwa shinikizo. Pia, niliweka malengo ya muda mrefu na kuepuka kurudia makosa yale yale.

Wengi wetu tunapitia hali kama hizi lakini kama wewe unavyofahamu, hatujifunzi kwa kushinda pekee. Tunakua kwa kushindwa. Kila tiketi inayochanika inatufundisha jambo jipya.

🔑 Somo: Betting siyo njia ya kupata pesa haraka inahitaji uelewa, mipango, na nidhamu. Ukiweka bidii na ukajifunza kutokana na makosa yako, utapata mafanikio ya muda mrefu.

Soma Pia: Betting ni mchezo unaoweza kukuletea umasikini hata kukuua!

Kwa hiyo, ushindi na hasara ni sehemu ya safari yetu. Jifunze kutokana na kila hatua, na hakikisha unakuwa na mtazamo wa muda mrefu. Hata wakati unaposhindwa, bado unakuwa mshindi kama unajifunza kitu kipya.

Je, wewe una stori yako ya kupoteza au kushinda? Hebu tushirikishe hapa!

Updates Nimesoma comment nyingi zinadai kuwa yawezekana niliuziwa Mechi na wale jamaa wa Fixed,naomba niwajibu hapa sijawai kufanya huo upuuzi iko hivi nimeanza kubet miaka sio mengi wakati wa kombe la dunia linacheza kitu ambacho kilinifanya niweke Milioni tayari nilikuwa nimeshakula zaidi ya Milioni 6 kwa siku 2 tu tena kwa option ya draw kipindi hicho kampuni ya Gwala Bet inaanza wenzangu na mimi nadhani mnakumbuka Gwala Bet ilikuwa inatoa 500 Free bet kila siku.

Nikaona hawa wazee wana kiasi kidogo cha ushindi 20M max,acha niende betpawa nikazipige hela sio kwamba nilikurupuka hapana kawaida uwa nina strategy zangu kwenye draw haikuwa bahati ila baada ya muda si mrefu niliirudisha kwa option ya draw pia.

Hadi mtaa wakaniita Mturutumbi maana ili sio jina langu harisi ila niwambie tu bet sio nzuri maana kuna muda mambo yanagoma kabisa
Safi sana.Je umeacha kubet au bado unaendelea.
 
Sema kuna visheria vyako ukiviweka kwenye betting na ukavifuta unaenjoy sana.

1. Idadi ya team (angalau zisizidi tano kwa slip)

2. Dau (kiasi cha dau kwa kila slip kile ambacho hata ukikipoteza kwa siku husika hakitoathiri mahitaji ya msingi)

3. Jumla ya odd kwa slip moja. (Odd 2 -4)
4. Option (masoko)
5. Idadi ya slip kwa siku.(1-4)
6. Fanya kama tu side hustle au fun.

Ukiweza kuwa na nidhamu hapo Kwenye mambo sita basi utaenjoy.
Hasara haifukuziwi emejiwekea sheria slip kwa siku ni tatu imechanika yote relax siku hiyo ni mbaya utaendelea kesho.
 
Back
Top Bottom