Betting ni mchezo unaoweza kukuletea umasikini hata kukuua!

Betting ni mchezo unaoweza kukuletea umasikini hata kukuua!

Forex hamna kitu bora ukazane na betting. The only way unaweza kutengeneza hela kwenye masoko ya fedha ni stocks na derivatives.
hiz kazi ni ngumu kweli kweli, wananufaika watu wachache sana
 
Hakuna faida kwenye Forex narudia tena na tena Forex ni kama network marketing unapewa link ujiunge kwa trading platform fulani kila ukitrade aliyekupa link anapewa comission. Ni utapeli mtupu kwenye forex.
ndio maana unakuta mtu kakomaa kusambaza link, hiyo ni kwa faida yake yeye mwenyewe,si kwamba anatangaza fursa
 
Sidhani kama kuna mtu anabeti/alibeti kunishinda mimi!

Betting ina addiction ile mbaya, ikikukumba siyo rahisi kucomoka!

Hongera nyingi kwa aliegundua hii michezo, alitumia akili kwelikweli! Nimetumia kila mbinu, kila hesabu ninazozijua lakini kipigo kiko palepale!

Pia niwape pole wale mnaoamini kwamba ipo siku watatusua kwenye Betting, mnajidanganya, mtaambulia hasara kiuchumi na kiafya!


Namuona mtu mmoja anataka kusema ati "beti kwa starehe tu" "bet what you can afford to lose" pole sana.


Kadri unavyopoteza ndivyo unavyozidi kupambana ili uokoe ulichopoteza, aidha kwa kuongeza dau au odds. Wazee wa hizo kazi wananielewa


Kwasasa accounts zangu zote za kubetia nimeshazifunga japo kuna wakati nashawishika sana kufungua account mpya (addiction hiyo)najizuia.


Baadhi ya vitu vilivyofanya niamue kuachana na betting;


-Nilikuwa napoteza muda mwingi (hata wa kazi) kutengeneza mkeka (uchambuzi)

-Maumivu makali ya kihisia baada ya timu moja kunichania mkeka niliotumia muda mwingi kuutengeneza, (na hiyo timu iliyochana italaaniwa sana sana😮‍💨)


-Niliona kabisa hapa nikiendelea hivi, presha na kisukari vile palee!

Hakuna wakati mgumu kama pale timu uliyoipa ushindi inafikia dakika ya 70',80' ubao unasoma 0-0, mapigo ya moyo yanaenda mbio, umekaa tu cha ajabu unatokwa jasho kama vile unapanda mlima!!



-Ilifika hatua nikawa napumzika kwa muda mchache sana, muda wa kulala mimi niko live, siyo kwamba nachati wala nini, ni nabetika!

Hata ukinitumia ujumbe WhatsApp usitegemee kujibiwa, ukipiga simu kama sio mtu ambae namheshimu sana jibu ni moja tu "nitakupigia badae kidogo, nipe dakika tano" mpaka pale tukio ninalofuatilia litakapokamilika (tabia mbovu sana hii)

Leo nimemsikia mtu anasema anatafuta mtaji aanze kubeti😆😆
Kama hujawahi kubeti, wala usitake kujifunza.

Kweli betting ni haramu ni heri uraibu mwingine wowote ila sio betting/kamari, betting ni mufilisi janjaruka mapema.
Mkuu naoma wewe ulikuwa umefikia hatua mbaya sana. Ni heri ulipoamua kuachana na kamari kabla haijakuua.

Kamar ni mchezo wa starehe kama ilivyo kucheza karata au game kwenye compiuta/simu. Tatizo kubwa ni pale haadhi ya watu wanaichukulia kamari kama kazi na chanzo cha mapato. Mnakosea sana aisee.

Afu eti mkeka ukochana timu moja mtu unaumia. Kwanini? Unahekesha sana mkuu. Abyway, ukiwa na hela za mawazo usicheze kamari. Ni ushauri tu
 
Mkuu naoma wewe ulikuwa umefikia hatua mbaya sana. Ni heri ulipoamua kuachana na kamari kabla haijakuua.

Kamar ni mchezo wa starehe kama ilivyo kucheza karata au game kwenye compiuta/simu. Tatizo kubwa ni pale haadhi ya watu wanaichukulia kamari kama kazi na chanzo cha mapato. Mnakosea sana aisee.
unabeti?
 
Acha kudanganya umma kamari Ina tajirisha watu ona hiyo listi chini wacheza kamari na pesa zao
Screenshot_20240806-181515_(1).png
 
Back
Top Bottom