Hapo ndio mahesabu ya betting yanapokuwaga magumu.
Utaweka 200,000 kwa odds 1.5 utakula 300,000 faida 100,000
Utarudia kutafuta odds 1.5 kwa dau la 200,000 halafu mhindi anatembea nayo yote yote unabaki na 100,000 ambayo siyo faida maana una hasara ya 100,000 tayari.
Baada ya hapo unapanick, unataka urudishe 100,000 yako upumzike.
Unaamua kutafuta odds 2 kisha unastake 100,000 yote ili upate 200,000 na vichenji.
Hapo mhindi anakushangaza anapita nayo yote.
Kwa ufupi huu mchezo unaitaji utulivu. Mhindi ametengeneza mahesabu ya kumbeba yeye, so kumla maana yake umefosi.