tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Nabet tu oale kunapokuwa na machaguo ya timu za ushindi. Silazimishi kama wewe.wewe ukibeti mara moja ndo unashinda?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nabet tu oale kunapokuwa na machaguo ya timu za ushindi. Silazimishi kama wewe.wewe ukibeti mara moja ndo unashinda?
point yangu ni moja tu, "betting ni kupoteza pesa na muda" baada ya kujua kiasi unachopoteza ndipo utaanza kujiona wa hovyo. Ndo maana nimekwambia wewe bado mchanga kwenye betting huna experience kuweza kumshawishi mtuSasa ndipo ucheze kama dozi ya dawa (mara 3 kwa siku)?
Mimi betting haijawahi kunitia hasara. I bet responsibly. Hasara kwenye betiing inakuwaje mkuu?point yangu ni moja tu, "betting ni kupoteza pesa na muda" baada ya kujua kiasi unachopoteza ndipo utaanza kujiona wa hovyo. Ndo maana nimekwambia wewe bado mchanga kwenye betting huna experience kuweza kumshawishi mtu
Umeliwa sh ngapi hadi Sasa mkuu?Sidhani kama kuna mtu anabeti/alibeti kunishinda mimi!
Betting ina addiction ile mbaya, ikikukumba siyo rahisi kucomoka!
Hongera nyingi kwa aliegundua hii michezo, alitumia akili kwelikweli! Nimetumia kila mbinu, kila hesabu ninazozijua lakini kipigo kiko palepale!
Pia niwape pole wale mnaoamini kwamba ipo siku watatusua kwenye Betting, mnajidanganya, mtaambulia hasara kiuchumi na kiafya!
Namuona mtu mmoja anataka kusema ati "beti kwa starehe tu" "bet what you can afford to lose" pole sana.
Kadri unavyopoteza ndivyo unavyozidi kupambana ili uokoe ulichopoteza, aidha kwa kuongeza dau au odds. Wazee wa hizo kazi wananielewa
Kwasasa accounts zangu zote za kubetia nimeshazifunga japo kuna wakati nashawishika sana kufungua account mpya (addiction hiyo)najizuia.
Baadhi ya vitu vilivyofanya niamue kuachana na betting;
-Nilikuwa napoteza muda mwingi (hata wa kazi) kutengeneza mkeka (uchambuzi)
-Maumivu makali ya kihisia baada ya timu moja kunichania mkeka niliotumia muda mwingi kuutengeneza, (na hiyo timu iliyochana italaaniwa sana sana😮💨)
-Niliona kabisa hapa nikiendelea hivi, presha na kisukari vile palee!
Hakuna wakati mgumu kama pale timu uliyoipa ushindi inafikia dakika ya 70',80' ubao unasoma 0-0, mapigo ya moyo yanaenda mbio, umekaa tu cha ajabu unatokwa jasho kama vile unapanda mlima!!
-Ilifika hatua nikawa napumzika kwa muda mchache sana, muda wa kulala mimi niko live, siyo kwamba nachati wala nini, ni nabetika!
Hata ukinitumia ujumbe WhatsApp usitegemee kujibiwa, ukipiga simu kama sio mtu ambae namheshimu sana jibu ni moja tu "nitakupigia badae kidogo, nipe dakika tano" mpaka pale tukio ninalofuatilia litakapokamilika (tabia mbovu sana hii)
Leo nimemsikia mtu anasema anatafuta mtaji aanze kubeti😆😆
Kama hujawahi kubeti, wala usitake kujifunza.
Kweli betting ni haramu ni heri uraibu mwingine wowote ila sio betting/kamari, betting ni mufilisi janjaruka mapema.
Mkuu Kamali ni mbaya Sana Ila ukiacha usiache Kwa kutangaza.juzi kati hapa nimedownload mpesa statement nikafuatilia miamala yangu ya miezi sita iliyopita, nikagundua betpawa peke yake wamekula nusu ya mshahara wangu Wa miezi hiyo sita!
Nakosa lakini nikishinda mara moja naingiza pesa nyingi sana. Kwa mfano naweza kupoteza hadi Tsh 50,000 lakini nikishinda nabutua hadi Tsh 900,000. Kwa hali hii nafilisikaje, kwa mfano?unapobeti huwa unakosa ama hukosi?
kama unastua mdogo mdogo una dalili za kuacha. Mara nyingi unapoacha kwa muda, ukirudi unazidisha mara mbili ya mwanzo ila ukiona perfomance iko chini kuliko awali ni dalili nzuri amini utaacha tu.Mkuu Kamali ni mbaya Sana Ila ukiacha usiache Kwa kutangaza.
Nilileta uzi humu WA kuacha kunywa pombe lakini huwezi Amini bado nastua mdogo mdogo Yani nimepunguza Tu.
Najua Taratibu nitaacha lakini najiuliza nikiacha mazima kunywa pombe nitatumia starehe gani jibu sijalipata bado.
Pamoja Sana mkuu.kama unastua mdogo mdogo una dalili za kuacha. Mara nyingi unapoacha kwa muda, ukirudi unazidisha mara mbili ya mwanzo ila ukiona perfomance iko chini kuliko awali ni dalili nzuri amini utaacha tu.
Hela za freemason ukizipata nunua hata shati,iwe kumbukumbu.ila ukitaka zizidi mawee.zinarudi zoteni hivyo mkuu, wewe umesema ukweli, wanaojifanya wajuaji hapa haiwaijui betting vzuri hawa
elfu hamsini?! maana yake ukibeti kwa elfu kumi unatafta odds kuanzia 90!Nakosa lakini nikishinda mara moja naingiza pesa nyingi sana. Kwa mfano naweza kupoteza hadi Tsh 50,000 lakini nikishinda nabutua hadi Tsh 900,000. Kwa hali hii nafilisikaje, kwa mfano?
Tatizo unabet kwa papara ndio maana unaliwa ovyo kisha unakimbilia hapa kulakamika. Bet kwa utulivu uonje faida ya kamari mkuu.
mkuu, umeongea point, betting utashinda kweli lakini hela unayoipata huko ni kama mkopo wenye riba ya asilimia elfu ya ulichochukua na lazima utailipa tu!Hela za freemason ukizipata nunua hata shati,iwe kumbukumbu.ila ukitaka zizidi mawee.zinarudi zote
Betting Haina mchanga Wala mzoefu ni akili Yako tu na pesa Yako acha habari zako mtu anaweza akabeti Leo na akapata hela ambayo wewe hujawahi kuipatainaonyesha wewe kwenye betting ni mchanga sana ipo siku utaelewa, nimekuquote pale juu ili nione uwezo wako