TANZIA Bi Fatma Karume Afariki dunia, akiwa na umri wa miaka 97

TANZIA Bi Fatma Karume Afariki dunia, akiwa na umri wa miaka 97

Allah Amsamehe na Amrehemu na Ampe Kauli Thaabit, Allahumma Aamiin.
Unamuamrisha Mungu amsamehe? Sijaona mahali umemuimba Mwenyezi Mungu amsamehe.

Halafu kiuhalisia mtu hawezi kusamehewa madhambi yake kwa watu kumwambia Mungu amsamehe.

Kitabu cha mtu kinafungwa pale tu pumzi inapokata hivyo baada ya hapo amali zake akiwa hai ndizo zitamuongoza wapi aende huko akhera.
 
Bi Fatuma Kurume aliyefariki, na Fatuma Karume ,yule Mwanasheria asiyependa kuolewa ,mbona majina yanafanana!
 
Aliyekuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume amefariki dunia leo, Septemba 21, 2026
Asante kwa Taarifa,
Taarifa ya kifo cha Bi.Fatma imetangazwa rasmi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
sio Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ni Mhe Othman Masoud Othman,(OMO)
Mama Fatma Karume alizaliwa Februari 2, 1929, Bumbwini Misufini, anatajwa kuwa miongoni mwa Wanawake walioshiriki katika harakati za kisiasa Zanzibar.
RIP Mama Fatma Karume,huyu ni miongoni mwa wake wa waasisi wawili wa taifa hili Nyerere na Karume, mwenzake ni Mama Maria Nyerere.

Moja ya sifa za ziada za Fatma Karume ni vocal na mkweli daima,wakati Maria Nyerere ni mkimya.

Fatma Karume,from time alikuwa akizungumzia ukweli halisi wa kilichokea Zanzibar siku ile ya usiku wa kuamkia siku Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya January 12,1964.

P
 

Attachments

  • IMG-20260921-WA0111.jpg
    IMG-20260921-WA0111.jpg
    43.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom