Biashara gani itanitoa kimaisha niepukane na umasikini?

Ulicho ongea ni kweli mnooo. Kuna jamaa mmoja kaenda kwa wakala mkuu wa gas y kupikia orex kampuni ni copa gas kisha kanunua vikirikuu vingi kinoma ananunua gas kwa copa gas kisha yy ndio anaingia kuwa uzia mawakala wadogo anakimbiza balaaa.
Mpk copa gas wakala mkuu kamwachia baadhi ya maeneo jamaa awe anauza yy tu.Na mwisho w mwaka copa gas anampatia jamaa commission a lot of money. Kwakua ni mteja wake mkubwa. Ss nasikia jamaa anatafta Canter kuongeza mauzo yake kutoka vikirikuu.
 
Very bold.
 
Fungua Bekary Kiwanda Cha mikate Na Uzoefu Kwenye Hili Tunaweza Kushirikiana
 
Ushauri mzuri sana huu mkuu
 
Asante, mkuu Kwa idea but nazan nikikubaliana na hilo yanipasa nipate balance zaidi ya hiii niliyonayo ili niweze fanikisha tofaut na hapo nitaishia njiani mkuu
 
Asante, mkuu Kwa idea but nazan nikikubaliana na hilo yanipasa nipate balance zaidi ya hiii niliyonayo ili niweze fanikisha tofaut na hapo nitaishia njiani mkuu

Wewe anza na logistics kwa level yako ya mtaji yani gari used iwe ist au vitz / bajaj….Then innovate on the same direction as the capital grows. Following the steps i adviced you….on my earlier posts.

Mimi naamini utafanikiwa na kuna siku utakuja kubali nimekushauri kitu sahihi, mimi nimepita huko sitaki upoteze hela kwa unpromissing ventures hela yenyewe ukiipoteza ku i remake ni utapasuka haswa.

Huezi kosa hela daily from logistics nature of business hasa hizi bajaj sijui uber kitu ambacho kitakutuliza akili ya kutafuta mishe za hela za mbio ndefu. Utakula, Utavaa, Utaishi sehem kdgo yenye staha na heshima mjini hapa utakuwa nayo huku malengo yako yakiwa ni ya mbali ila kwa mrengo huo huo.
 

Kwa kufanya Biashara ya uber hicho kitu napingana na wewe mkuu. Sasaivi biashara ya uber haina hela hiyo hesabu uloisema Sijui 40k-60k ni uwongo. Hiyo hesabu labda unaweza kuipata kipindi cha weekend ijumaa na jmosi tena kwa kukesha na sio guarantee. Biashara tax mtandao gari zimekuwa nyingi mno requests ni chache kuna kipindi madereva wanakosa hata mafuta ya kurudi na gari majumbani kwao wana yapaki mjini wanakula daladala kesho anarudi kulifata gari. Kwakuwa gari litakuwa lake atakuwa na uhakika tu wa kupata Hela ya kula elfu10-15 kwa siku huku mtaji wake wa milion10 ukiwa salama kwakuwa atakuwa kautia kwenye gari ili siku yoyote akiona namna gani haelewi analiuza gari.
 
Brother mimi nakushauri usianze kitu kipya kabisa usichokijua, jaribu kujiendeleza kwenye kitu ambacho unauzoefu nacho ambacho kimekuwezesha mpaka kuweza kufikisha hiyo milioni 10.

Kama wewe ulikua unafanya kazi ya udalali, basi jaribu kuifanya kwa ubora zaidi hiyo kazi yako, hii na maanisha kwa jaribu kuifanya ukiwa kwa usasa zaidi ukilenga aina flani ya wateja, ambao unaamini wanaweza kuongeza pato lako.

Kwa kuanzia, anza kwa kufanya ya fuatayo:-
1. Tafuta vibali na Leseni ili kuweza kuifanya kazi yako kisheria.
2. Tafuta ofisi rasmi ambayo itakuwa inajulikana na muda wote mteja ukimwelekeza basi ataweza kukufikia.
3. Ongeza circle ya connection ya madalali wanaofanya kazi kama yako.
4. Jaribu kulenga aina ya kazi/ vitu vya udalali unavyolenga ku specialize, yanai kama ni dalali wa majengo, vyumba, , magodown, mashamba na nk, au dalali magari, (Kikubwa hapa jaribu kuwa umelenga vitu flani)
5. Ongeza juhudi katika kujitangaza na kutafuta wateja ambao unaamini wataongeza kipato, kama mwanzo ulikua una wateja wa kuwasubiri mtaani, basi sasa anza kwa kuwatafuta wateja wakubwa zaidi kama makampuni, wafanyabiashara wakubwa na n.k
6. Tengeneza kanuni ambazo zitakutofautisha kazi yako ya udalali na madalali wengine ambao wapo mtaani, mfano uongo, kuweka bei kubwa ya juu, kutokuwa na uaminifu na n.k
7. Jipe muda katika kuendesha biashara yako kabla ya kuanza kuona faida, usitegemee faida ya haraka.
8. Tengeneza connection na watu wenye uelewa zaidi wanao husiana moja kwa moja na biashara yako kama Mawakili na wanasheria; Land officers, ma ofisa wa TRA, Polisi n.k (Hawa watakusaidia kwenye kazi zako za kila siku kama kuandaa mikataba, ushauri wa kuhus maswala ya kodi kwako na kwa mteja wako.
9. Fuatilia na kuwa na nidhamu ya kila pesa inayoingia na kutoka kwenye ofisi yako.
10. Fanya kazi kwa bidii na mtangulize Mungu katika kila hatua unayofanya katika kazi yako.

Yangu ni hayo nikiwa kama mtafutaji mwenzako wa kitaa.

AU Ukionashida kwenye yote kabisa tuite tuweke heshima Bar
 
Nimekupata sana ndugu na nimekuelewa vema sana Asante kwa ushauri.
 
Dalali unamiliki milion 10 umeshindwa hata kununua shamba ukate viwanja vidogo vidogo kisha utumie udalali wako uuze kwa faida???????

Ama kweli penye miti wajenzi hakuna!!!!!!!

Sent from my OPPO R11s using JamiiForums mobile app
Hili wazo na mimi nilikuwa nataka nimpe,ila nikaona watu watasema mtaji mdogo,lkn hiyo Hela ni nyingi anaweza akachukua eneo akalikata viwanja vya laki nanenane au 1m ili viende haraka na maisha yakaendelea
 

NONSENSE
 

Acha kumdanganya mwenzako biashara ya uber inalipa wewe huijui na hujawahi kuifanya. Uber nimefanya two years na kwakutumia Gari na hakuna nilichopata zaid ya kuumiza gari. Kwanza wabongo mlivyo na roho za kukunjiana huwa hamsemi ukweli siri za mafanikio yenu/kuelezea biashara zenu namna mlivyo anza njia mlizopitia mpaka kukuza mitaji kuwa mikubwa. Wengi wenu mkiombwa ushauri wa baishara mnaishia tu kusema“Kuna jamaa anapiga pesa alianza na kirukuu ya kukodi sasaivi ameshanunua zake nne na mwezi ujao anavuta Fuso” STUPID!! biashara zenu binafsi mnazozifanya au zilizowatoa huwa hamzisemi. Bla bla tu na kujifanya mna ideas nyingi vichwani kumbe wachawi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…