Biashara yenye faida kubwa ni biashara yenye mtaji mkubwa. Faida unayoizungumzia wewe unatakiwa utoe hapo Kodi, Mshahara wa wafanyakazi wako, Matumizi madogo madogo kama umeme, nauli na chakula nk. Ushahuri wangu kama mfanya biashara, duniani hakuna shortcut, wewe kama unadhania faida inatengenezwa kirahisi utajikuta watu wanakushauri na hawana background na biashara, hawana elimu ya biashara na ulivyouliza ni jambo la busara ila inaonyesha huna elimu ya kutosha ndio maana umeomba ushauri...
Ushauri wa zaida, fanya biashara unayoiweza na uliyo na ujuzi nao, biashara za kuambiwa utapata hasara kubwa mno kama huna uzoefu nazo. Anza biashara hata kama ni ndogo kwa kuwa una ujuzi nayo utafika mbali sana. Na una nafasi ya kukuza biashara yako kuwa kubwa zaidi. Bakhresa katoka kaitoa bishara ya kuuza maandani kutoka mtaa kwa mtaa mpaka imekuwa ni bishara kubwa na anauza nchi nzima wakati wengi wanalenga mtaa mmoja. Ila kwa ndoto zake na udogo wake kaufanya kwa makubwa...
Mie nilianza na shilling elfu 2 ila jimehangaika kwa miaka minne, ila nimenunua viwanja nimeweza kujikimu kimaisha na vitu vingi vyenye thamani ya mamilion ambayo sikutegemea kushika back then...
Ila kwa kwa million 100 afu hujui unataka ufanye nayo nini, manake labda hela ya urithi ila kama ungekuwa mtafutaji mda mrefu ungeweza kujua unachotaka kufanya. Kuwe serious na ukibabaika itakugharimu...