Kilimo gani hicho? Wewe unafanya hicho kilimo chenye kuingiza hela nyingi kwa muda mfupi?
Kwanza ukiachana na mazao ambayo serikali inasimamia haya mengine unakula faida 100% bila TRA kunusa. Hii ni tundu ambalo TRA wataliziba baadae, sasa hivi liko wazi.
Usinifuate mimi mazingira ya soko na shamba hayawezi kuwa sawa.
1. Shamba liwe lako.
2. Lenye rutuba sio kila kitu lazima uweke mbolea
3. Chanzo cha maji cha uhakika
4. Shamba liweze kufikika kama sio hapo au jirani tu.
5. Soko.
6. Hicho unacholima utauzia shambani au utagharimia kupeleka kwenye soko au mnunuzi.
7 Pia kulima kwa simu na kutuma hela hakufai kama huwezi kujihusisha mwenyewe achana na kilimo. Kama una mind degree yako pia kaa pembeni, kule shamba unakutana na watu kila aina.
Mimi nililima mihogo na kabla ya kulima nilikuwa na maongezi na mkataba na kampuni iko Mwenge, wao walikuwa wanapeleka mhogo China.
Kwa hiyo nililima fresh tu wakataka mhogo niukatekate kama slesi za 5cm halafu nikaushe baadae wakaniletea viroba vya 50kg nijaze.
Kukata kata ikawa shida. Wakaniazimisha mashine ya kukatakata na jenereta bure nikaa kaa nazo wiki 2.
Nilitengeneza mhogo tani 2 wakaja wakaufwata mzigo shambani kwa gharama zao.
Hela waliingiza kwenye akaunti ndani ya siku 4.
Sasa hivi nimewakimbia bei wameshusha sana haina maslahi. Nataka kulima kitu kingine.
Kilimo usiige ile ujifunze halafu unaboresha kwako.