Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?

Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?

Kama ukipata taarifa sahihi na connection ya kutosha kwa wahusika wenyewe utajua ukweli wote. Ila kwa sasa na hali ilivyo naona ishu za dhahabu zina pesa. Ila mpaka upate ujuzi na connection sahihi. Narudia tena ni kuwa ishu za dhahabu zinapesa nyingi mno ila inabidi upate ujuzi na connection ya kutosha.

NB: Mimi sina connection wala ujuzi.

Dhahabu ukubali kusoma mchezo kwanza..then usiwe mtu wa kukata tamaa...jitune maisha ya porini...kuwa SMART... hela utaiona! Sijui kama kuna sehemu hawajui wala kufahamu kukata tamaa kama machimboni..hii spirit ingekuwa kwa kila raia maisha yangekua nafuu sana
 
Kwanza ukiachana na mazao ambayo serikali inasimamia haya mengine unakula faida 100% bila TRA kunusa. Hii ni tundu ambalo TRA wataliziba baadae sasa hivi liko wazi.

Usinifuate mimi mazingira ya soko na shamba hayawezi kuwa sawa.

1. Shamba liwe lako.
2. Lenye rutuba sio kila kitu lazina uweke mbolea
3. Chanzo cha maji cha uhakika
4. Shamba liweze kufikika kama sio hapo au jirani tu.
5. Soko.
6. Hicho unacholima utauzia shambani au utagharimia kupeleka kwenye soko au mnunuzi.
7 pia kulima kwa simu na kutuma hela hakufai kama huwezi kujihusisha mwenyewe achana na kilimo. Kama una mind degree yako pia kaa pembeni, kule shamba unakutana na watu kila aina.


Mimi nililima mihogo na kabla ya kulima nilikuwa na maongezi na mkataba na kampuni iko mwenge wao walikuwa wanapeleka mhogo china.

Kwa hiyo nililima fresh tu wakataka mhogo niukatekate kama slesi za 5cm halafu nikaushe baadae wakaniletea viroba vya 50kg nijaze.

Kukata kata ikawa shida. Wakaniazimisha mashine ya kukatakata na jenereta bure nikaa kaa nazo wiki 2.

Nilitengeneza mhogo tani 2 wakaja wakaufwata mzigo shambani kwa gharama zao.

Hela waliingiza kwenye akaunti ndani ya siku 4.

Sasa hivi nimewakimbia bei wameshusha sana haina maslahi. Nataka kulima kitu kingine.

Kilimo usiige ile ujifunze halafu unaboresha kwako .
Sasa ulitakiw uwe unapelelza uanzee kupeleka mwwnye mzigo.niliona wschina wanaichkua sana lushoto
 
Hakuna tena wengine wote tunagombaniana buguruni , huu mhogo wachina sio wanakula wanafuata starch na kuna mbegu maalum yenye starch nyingi.
Mkuu mbegu unanunua wapi? Na wanauzaje
Au unatumia za wakulima wenzio wakishavuna ?
 
Kuna kikampuni cha wachina 2016 walisema limeni mihogo kwa wingi tutanunua kilo 1000/= wana wakajaa wakaja moro kwa fujo wakalima hatari...mhogo ulipokomaa wakanunua kwa shilingi MIA...narudia..shilingi MIA..hahaa wapi shogangu Shoma...alidata balaa[emoji1787][emoji1787]..cheza michezo yote sio mchezo wa soko la TZ
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Unajua Milionea bado maisha yako yatakuwa ya kawaida kwa Tanzania ?, Unless otherwise upo UK au USA na unaongelea Dollar au Pounds...

Pia sustainability je ni vitu vya msimu au once you are settled umemaliza ?, Kwa nchi kama bongo kila kitu kinabadilika kila kukicha kwakweli shughuli nyingi ni bahati nasibu... (vitu vingi ni unpredictable) ukizingatia mambo mengi sustainable yanahitaji long term plans..., sasa utaplan vipi long term wakati kesho anaweza akaja chizi akabadilisha kilichopo leo?
Nikaona mtu anapenda kuandika Kiswaenglish na viashiria vya kujifanya anajua sana hua kumdharau na kumpuuza kama mtu mjinga mjinga tu
 
Back
Top Bottom