Linachukua sio chini ya miezi saba ndio maana nililima eka 5Vizuri..Hili zao la mihogo shambani linachukua muda gani hadi kuvuna?
Achana nao bei sasa hivi haillipi kabisa nisikudanganye. Uzuri wa mhogo ukishafunga juu majani hupalilii tena.niunganishe nao mkuu nilime muhogo kwa bei yao elekezi
Ila nwanzoni kusafisha shamba na zile palizi 2 au 3 inakula, ingawa jamaa yangu mmoja alimwaga dawa ya magugu.
Ile kampuni ni ya Mhehe mmoja anaishi China. Alinikuta pale Mwenge vijana wake wamechambua mihogo yangu mengine wakaitupa alipofika aliirudisha yote kwenye viroba vikapimwa tena.
Nilipokaa nae mezani kuhusu bei alikataa kuongeza anadai ni mambo ya soko la dunia.
Hiyo Kampuni iko Mwenge hawajaweka bango nje sijui kwa nini ila ukitokea zile taa kuelekea cocacola mita 100 njia ya kwanza kulia unapita ya pili nadhani unaingia kulia halafu unaenda mita 40 au 50 kuna geti jeusi, mi mwaka mzima sijafika pale sijui kama bado wapo ila hapo ndio mhogo wangu uliwekwa halafu nikaitwa niupime tena katika kg 50 bags ili wanilipe, kuna viroba vingine vilizidi vingine vilipungua.
Naona kuna watu wanauliza mhogo unachukua muda gani. Haipungui miezi 7
Ila ili angalau kila shina lifike wastani kg 20 ni miezi 8 au 9.
Ndio maana inabidi ulime angalau eka 4 na kuendelea.
Hata wao ukiwaambia eka moja hawafuati mzigo ni hasara.
Eg:
18kg x 4000 miche kwa eka x ( bei) ya kununua x eka 5 ndio utaona matusi yake.
Ila mhogo mkavu unapungua uzito nusu
Achana na mhogo kwa sasa mpaka mazingira yakae vizuri.