Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara ni uvumilivu tu, mwanzo huaga ni mgumu, lazima uanze na kupata kidogo
 
Logistics ina faida sana ila again , sio kwa kila mtu!
Simu ya dereva kuwa lori limeanguka na copper ya watu imeibiwa inataka ujasiri wa hali ya juu kuipokea na kuifanyia kazi .
Sahihi mkuu ndo mana gari zina bima comprehensive na mzigo unakatiwa bima pia.. ndo mana nikasema inamtoa mtu makini yan ni kufatilia kwa karibu sana usi relax..anyway hakuna biashara isiyo na risk! the higher the risk...

Boss wangu wa kwanza nilianza nae kazi 2016 deceber ana gari 23..nimeachana nae 2019 ana gari 159! Naongea kwa experience sijahadithiwa.
 
Fundisha hapa hapa wote tuelemike kwa faida ya jamii yako
Mkuu, tabia ya members humu ndani siku hizi imefanya watu wengi wawe wazito sana kuchangia publicly.

Unaweza toa ushauri/wazo bure kabisa kutokana na field experience uliyonayo then anaibuka mtu anakuita 'motivational speaker' au anakutusi kabisa!!
 
Umekurupuka sana mpaka naona aibu mimi aisee..wap nimesema unapata USD3500? Binafs hua sichangii kitu kama sina personal experience mana sina muda huo wa kupoteza! Kuna mmoja juu apo ame challenge kumuuliza na yeye hajui ndo wabongo tulivo imradi jitu likukashifu tu! kwanza milion 300 sio yako inakuwashia nn? Au ndo chawa wa hiari 👀
 
Mkuu, tabia ya members humu ndani siku hizi imefanya watu wengi wawe wazito sana kuchangia publicly.

Unaweza toa ushauri/wazo bure kabisa kutokana na field experience uliyonayo then anaibuka mtu anakuita 'motivational speaker' au anakutusi kabisa!!
Ni kweli nadhani hizi changamoto zisikukatishe tamaa, Bado Kuna watu wema humu.

SI unaona huyu bwana HIMARS yeye kaona Mimi nimekuja kutafuta umaarufu humu
 
Mbona kubwa SANA
 
Sasa unaita hio 5m faida halafu unatuambia bado hujalipa mishahara. Chai.
 
Hatufanyi vitu tunavyopenda, tunajifunza na kupenda ndio tunafanya, ukisema fanya kile unakipoenda some of us tunapenda kulala na kula misosi na kula bata sana.....
 
Biashara ni ngumu sana nikiwaza nasema tu wacha wafanyabiashara tuitwe risk takers

Nina biashara 3
Moja mtaji laki 3 ila kila siku napokea feturn ya avarage ya 9000
Nyingine ina mtaji 2,000,000 return yake monthly hata laki na nusu haifikishi (though ni eneo la kimkakati huko mbele italeta return nzuri tu I hope)
Biashara ya 3 Mtaji milion 2 , daily return wastan ni sh 10,000

Cha kushangaza eti naogopa kupoteza ile location ya biashara ya pili nikiamini nikiiacha nitakuja kuililia huko mbele maana ni potential area sana huko mbele miaka mitano baadae

Na zote tatu ni biashara zisizo na mwingiliano yaani ni biashara tofauti kabisa.

Biashara ni ngumu sana for sure
 
Sasa unapataje faida kabla ya kutoa running costs ikiwepo hiyo mishahara ya wafanyakazi??

Faida inapatikana after running cost kutolewa..
Ndio boss, hizo ni typing error angalia heading hapo ndani nimekosea.

Ishu ni kwamba Kwa huu mda mchache biashara imeenda kinyume na matarajio yangu
 
Anaepata 5m per month kwa mtaji wa 300m, anapata faida nzuri.
Hasa kama anatoa ajira kwa watu, hiyo pia ni faida.
 
Ungewekeza JATU Plc, kilimo bila stress....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…