Sana! Tell me about it, Amigo!
Sasa hapo kuna mambo kadhaa yanaweza kuwa na utofauti kutegemeana na hasa eneo unalotaka kufanyia kazi.
Nb:
Sifanyi personally ila nahusiana nayo indirectly na nna jamaa yangu wa karibu sn ambaye tunafanya naye kazi ambaye anamiliki elution machines/plant, hivyo nna experience ya kutosha kukupa ABCs zake.
Nitaongelea kwa uzoefu wa Chunya:
1. Unaweza kujenga ama kupanga jengo ambalo tayari limejengwa ama kununua kabisa the full project ukipata mtu anayeuza au ukimpa mtu ofa atayoridhia maana kwa Chunya zipo nyingi tu.
2. Kama ni kujenga, unanunua eneo (kuna eneo lililotengwa kwa hizo mishe) unafata taratibu zote za vibali nk then utajenga jengo pamoja na miundombinu yote kama godown, ofisi, vyumba vya kulala, jiko, stoo, toilets, mifumo ya taka nk. Sina actual cost za ujenzi ila itategemea na unataka pawe na muonekano gani zaidi ndio itatoa gharama halisi. Hilo ni jengo tu mbali na machine za kuchenjulia.
3. Kwny kukodi mara nyingi ni kati ya 12m-15m per year, yaan hapo unakuta jengo liko na facilities zote then we unafunga mashine zako unaanza kazi.
4. Kuna taratibu za kufata pamoja na gharama za kulipia kuanzia halmashauri, Tra, NEMC na OSHA.
5. Gharama za machine pia hutofautiana kutkana na ufanisi wake. Mfano za huyu mwanangu zilikuwa around 60m kwa machine 2.
Baada ya kukamilisha hapo labda kingine cha kujiuliza unatarget wateja waje kufanyia kazi kwako au unataka kuchenjua mizigo yako mwenyewe?
Kama ni wateja kuna namna ya kuwa-tap ili wafanyie kazi kwako (hili sitaweka maelezo hapa sabab ni siri ya kazi ya jamaa yangu) ila ukiwa serious ntakusaidia namna ya kuenenda.
Pia unaweza kuwa unanunua makapi yaliyokwisha kuchenjuliwa kwny machine zingine na ukayapima ukaona bado unaweza kupata chochote pia ni fursa, ila hii inategemea na ufanisi wa machine zako maana zinatofautiana kiasi kwamba output ya machine moja inaweza kuwa input kwny nyingine.
Atleast utakuwa umepata mwanga mkuu.