Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

hii inawezekana kutegemea na aina ya biashara!

mfano anatefuga kuroiler akawalisha inavyotakiwa na akauza rejareja kila mwezi anaweza fikisha hata 4M

hata anayeweka layers mayai yanalipa kama atachanganya chakula yeye mwenyewe!
Sawa mkuu,ngoja wafugaji waje hapa watatupa uzoefu wao.
 
Mkuu kuna kitu inaitwa Novatechfx.
Unaweka hela yako wanaizungusha.
Wanalipa kila week.
Hiyo 300m kwa week wanakupa sio chini ya 7m.
Nipe elimu kidogo ni bank gani hufanya hivyo?
 
Hiyo return ni ya juu sana sielewi kwa nini unalalamika. Ume invest 300M returns kwa mwaka ni 60M ambayo ni karibia 20%. hamna biashara nyingine yenye such high returns. Hata treasury bills/bonds annual returns ni around 10%.
Return yake ni ndogo mkuu. With 20m investment napata net profit 800k-1.2m kwa mwezi
 
Sawa mkuu,ngoja wafugaji waje hapa watatupa uzoefu wao.
mie pia nafanya ufugaji huu! ingawa si kwa kiwango hiki ila nina muda mrefu! na nimeshafanya research kubwa tu! nikipata mtaji wa kufka 10M nitatoboa! maana mabanda ni yangu na chakula nachanganya mwenyewe! magonjwa ya kuku napambania mwenyewe,
kikubwa usicheze na mtaji kwenye biashara kama hii
 
Bro mpaka nafikia malengo ya kutafuta huo mfupa kweli ntakua sina connection za mizigo kweli?? Niko jikoni me ndo natafuta sub contract nawagawia kazi... kwa sasa tuna kazi ya Rwanda kigali $117 kwa tani., kila trip gari inabakiza 3,100,000 faida na kwa mwez mtu kwenda trip 3 uhakika wengine 4! Siku nikiishiwa kazi ntakuchek mkuu, af usiidharau 113 ndo chombo ya kumtoa maskini mafichoni, mchawi dereva tu mzuri [emoji16].. pamoja [emoji1666]
Vip ukiwa na 114 mende alfu ukaweka tella pili imeekaaje

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
😂😂😂

Unayumba mzee ha ha ha.

Kwa all legit business, zisizo na makando kando. Tena zile ambazo zinakaguliwa haswa. Most katika hizo net profit huwa zina range 10% ikienda sana 30%. Tena hizi rate ni kwa well established company ama brand.

Chukua mfano Giants tech Company kama Amazon.
Total Assets over 400+ billions dollar
Total Revenue over 400+ billions dollar
Ila annual net profit inatulia kwenye just 30+ billions dollar.

Je vipi hapo kwa mtizamo wako hawa jamaa hawajui kufanya biashara eeh? Hapo ukiizoom vizuri net profit unaona kabisa inasoma below 10%.

Zunguka kote kwa ma top notch kama Alphabet Inc, Sio Meta wala Apple, sio Alibaba wala nani kote net profit utaikuta kwenye range hiyo ya 10% ikienda saaaana 30%.

Issue ya faida mara 2 mara 5 au hata mara 500 kwa kubeti 😂 ni biashara ya kuifanya kihuni sana, sio kwamba hazipo zipo ila sio sahihi kwa kila mtu.

Personality yako ndio itakayoamua unafanya biashara ipi na itaingiza shi ngapi kwa uwekezaji unaoenda kufanya. Maana mwingine hapa atasema hizo Mil300 ukifungu danguro la pisi kali ukawa unakula kila kichwa 50k kwa siku watu 20 n m1 kwa mwezi ni 30M kwa mwaka 360M...

Yah ni hesabu za kufikirika ila zinashawishi. Swali juu ya swali, hiyo biashara ni legal kwa eneo ulipo? Hiyo biashara itakutambulishaje kwenye jamii unayoishi? Katika hustle zako una standard ulizojiwekea za kukuingizia kipato au kila mzoga mbele as long as unaingiza pesa hata kuua unaweza?

After all Biashara kubwa kwanza ni ngumu sana kuifanyia uhuni. Tofauti na biashara ndogo ndogo ambazo hupigwi sana torch za seikali.

Kwa Mil 300, kulingana na aina ya biashara 5per month, 60 per annum ni standard otherwise ukitaka kuipatia faida (net profit) of over 100Mil inakulazim kile unachozalisha ukiwekee price tag ya karibu mara 2 to 3 zaidi ya gharama za uzalishaji.

Sasa kama una leseni na una- operate legally huu uhuni unaufanya vipi labda ukaufanye kwenye dunia yako 😂.

Check biashara hizi chache kwa mfano
1.Real estate.kununua na kuuza viwanja.mfano unanunua heka 10 kwa m300 then KILA hekta unatoa viwanja 6,kila kiwanja unauza milioni 20
o kwa heka uliyonunua m30 unapata revenue ya m120 so eka kumi unapata total revenue 1.2 bilioni. Toa gharama zote mfano tax, operation cost, nk haizidi milioni 300 per year.

2.Kuwa na plant ya kuponda kokoto total investment ni m250.
Lori moja la kokoto 30 tonn wanauza milioni 1.2 hapa profit ni speed yako ya market unacheza na watu wenye plant za concrete mixers,wakandarasi unawapa percentage yao wakupe tenda.
3.Kusuply madini ya matani mfano chokaa,quartz,nk
4.Kuwekeza kwenye recycling taka za plastic, karatasi,
 
Kuna mda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara. Nimewekeza tsh. million mia tatu(300m+) nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi. Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
kuna Saccos ukipeleka hiyo wanakulipa 2% kila mwez kama faida
 
Hata zaidi ya bilioni 10 kwa mwaka unapata kwenye madini,unapiga fully yaani madini ya matani na ya gram pia.Inayokata pesa ni madini ya gram.Matani uhakika pesa inarudi.
Ajirisk tu huko kuliko kungojea vimillion 5 kwa mwezi kwa million 300
 
Kiuharisia biashara inahitaji roho ngumu aina. Ila kwa hiyo hela yako hupaswi kupata faida hiyo kwa mwezi. Kama ni hivyo ikusanye hiyo M.300 yote wekeza kwenye hisa za mabank. Kwa pesa hiyo utakuwa unapata return ya si chini ya Milioni 25 kila mwezi. Na hapo hakuna wa kumlipa,wala hakuna pressure hata kidogo. Unakula hiyo ukiwa umetulia tu nyumbani.

Naitamani sana hii biashara,siku nikipata tu mkwanja mrefu lazima nijitupie huko
 
Angalau nimepitia Comments zote na kwa hakika kuna waliotoa maoni mazuri mno.

Tatizo nilioliona kwa Mhusika ni kwamba, aliset expectations kubwa. Au huenda alijiingiza kwenye biashara baada ya kuona returns za mwenzake.

Huenda anailinganisha gross profit yake na gross ya biashara iliyo-mature tayari.

Nikuhakikishie, kama ndo kwanza biashara ina mwezi mmoja maana yake ina faida kubwa sana. Kazia kupiga kazi huku ukisuburi. I'm sure, onto the next month utapata gross ya 8m.

Hao wanashauri juu ya UTT na BOT bonds wameshachelewa. Maana hata ukisema uikimbie biashara yako ya sasa, hutopata tena ile 300m. Lazima ipungue.

Ungesema ni aina gani ya biashara ili ufahamishwe kama ime-under perform.
 
mie pia nafanya ufugaji huu! ingawa si kwa kiwango hiki ila nina muda mrefu! na nimeshafanya research kubwa tu! nikipata mtaji wa kufka 10M nitatoboa! maana mabanda ni yangu na chakula nachanganya mwenyewe! magonjwa ya kuku napambania mwenyewe,
kikubwa usicheze na mtaji kwenye biashara kama hii
Safi Sana mkuu,all the best.
 
Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara. Nimewekeza tsh. million mia tatu(300m+) nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi. Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
Duh pole sana.
 
Back
Top Bottom