😂😂😂
Unayumba mzee ha ha ha.
Kwa all legit business, zisizo na makando kando. Tena zile ambazo zinakaguliwa haswa. Most katika hizo net profit huwa zina range 10% ikienda sana 30%. Tena hizi rate ni kwa well established company ama brand.
Chukua mfano Giants tech Company kama Amazon.
Total Assets over 400+ billions dollar
Total Revenue over 400+ billions dollar
Ila annual net profit inatulia kwenye just 30+ billions dollar.
Je vipi hapo kwa mtizamo wako hawa jamaa hawajui kufanya biashara eeh? Hapo ukiizoom vizuri net profit unaona kabisa inasoma below 10%.
Zunguka kote kwa ma top notch kama Alphabet Inc, Sio Meta wala Apple, sio Alibaba wala nani kote net profit utaikuta kwenye range hiyo ya 10% ikienda saaaana 30%.
Issue ya faida mara 2 mara 5 au hata mara 500 kwa kubeti 😂 ni biashara ya kuifanya kihuni sana, sio kwamba hazipo zipo ila sio sahihi kwa kila mtu.
Personality yako ndio itakayoamua unafanya biashara ipi na itaingiza shi ngapi kwa uwekezaji unaoenda kufanya. Maana mwingine hapa atasema hizo Mil300 ukifungu danguro la pisi kali ukawa unakula kila kichwa 50k kwa siku watu 20 n m1 kwa mwezi ni 30M kwa mwaka 360M...
Yah ni hesabu za kufikirika ila zinashawishi. Swali juu ya swali, hiyo biashara ni legal kwa eneo ulipo? Hiyo biashara itakutambulishaje kwenye jamii unayoishi? Katika hustle zako una standard ulizojiwekea za kukuingizia kipato au kila mzoga mbele as long as unaingiza pesa hata kuua unaweza?
After all Biashara kubwa kwanza ni ngumu sana kuifanyia uhuni. Tofauti na biashara ndogo ndogo ambazo hupigwi sana torch za seikali.
Kwa Mil 300, kulingana na aina ya biashara 5per month, 60 per annum ni standard otherwise ukitaka kuipatia faida (net profit) of over 100Mil inakulazim kile unachozalisha ukiwekee price tag ya karibu mara 2 to 3 zaidi ya gharama za uzalishaji.
Sasa kama una leseni na una- operate legally huu uhuni unaufanya vipi labda ukaufanye kwenye dunia yako 😂.