Look at this so selfless fellow! Thank you for your selflessness. Priceless kabisa. Nashukuru sana. In your great education, Manpower hujaizungumizia apo kaka... You shall need engineers?
Thanks bro, kwangu huwa naamini mafanikio ni ile hali ambayo nimefika naweza kufanya wengine wakafanikiwa pia japo kwa kuwapa taarifa/ushauri juu ya kile ninachoweza kuwasaidia.
Back to the topic;
Kuhusu man power kama utaweza pata wasomi (professionals) ni nzuri zaidi lakini kwa uzoefu hizi kazi wanaofanya wengi ni form four leavers tu ambao wamejifunza na kupata uzoefu.
Japo wana weakness zao kwny kazi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupambana na changamoto mpya, mostly hizi kazi ni repeatitive in nature kwa hyo inawezekana katika muda wote aliojifunza kazi hakukutana na aina flani ya changamoto hivyo simply anakuwa ignorant kwny eneo husika.
All in all wanafanya kazi vizuri especially ukikuta aliyemfunza alikuwa vizuri na muhusika pia ni mtu wa kujiongeza na muaminifu pia maana hizi kazi vijana wengi wanaangukia kwny tamaa ya wizi. Ila kwa hali ya sasa bado unaweza kuwadhibiti through means km vile cctv cameras.
Watu hasa utaohitaji kuwa nao ni:
1. Mchomaji wa dhahabu
2. Vijana 4-8 kwa ajili ya kupakia na kushusha cabon, kufanya usafi etc
3. Mpishi (salary 150k - 200k per month)
4. Mlinzi (mostly ni wamasai) - around 150-200k per month.
5. Obvious itaongezeka gharama ya chakula cha kila siku from morning to evening (atleast 3 meals)
Hao #1&2 unaweza kuwalipa mshahara kati ya 250-300k per month then kila ukishusha mzigo unawapa posho lets say 20k each. Na miongoni mwao unateua supervisor wako hapo, kama hauko karibu unaweza kuwa na Manager pia kwa ajili ya kusettle issues za kiserikali na hizo agencies zingine wanapofanya visit au km kuna changamoto yoyote.