Gulio Tanzania
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,325
- 7,807
Mpaka sasa nipo katika biashara kwa kipindi cha miaka mitano sasa nina uzoefu kiasi chake ila nilichojifunza cha kwanza elimu inahitaji Sana katika ufanyaji wa biashara. Kuna umuhimu mkubwa hata Serikali kuanzisha mitaala ili watu wapate elimu juu somo hili.
Biashara nyingi bado nazoziona hasa hizi ndogo ndio vijana wengi wanaotoka chuo nimeona wanazifanya lakini nyingi hazikui.
Mitaji ya kuanzia laki 8 mpaka million 2.
Wengi nimegundua wanacheza na biashara zenye kuingiza faida ya Tsh. 20,000 akijitahidi sana ni 30,000. Sasa kama unaingiza elfu 20 kwa siku kwa mwezi utaingiza laki sita pesa ambayo haiwezi kukuza mtaji wako.
Mfanyabiashara ambaye anaingiza faida ya elfu 30 kwa mwezi atakuwa na uhakika wa kuingiza laki 9 kwa mtaji alionao itaonekana bado ni pesa kubwa lakini tuangalie matumizi yake kwa mwezi ni laki 6 atasevu laki 3 kwa mwaka ataingiza faida ya mil 3.6 bado ni faida ndogo Sana kuweza kukutoa kimaisha.
Nilichojifunza wafanyabiashara wengi wenye mitaji midogo wanakosa ni elimu bado wengi wana ile hali ya kujibana kwenye matumizi yao binafsi lakini hawafikiri kuzalisha zaidi faida. Mfanyabiashara ukifikiria kujibana ndio kukuza mtaji unakosea utashindwa kuruhusu akili nyingine ya kuzalisha zaidi faida kwenye biashara unayofanya ama chanzo kingine cha kipato.
Angalia sasa kama utaweza kuingiza faida ya elfu 50 kwa siku kwa mwezi utaingiza mil 1.5 matumizi yako binafsi laki 7 utaweza sevu kila mwezi laki 8 kwa mwaka mmoja tu utakuwa umepata faida ya mil 9.6