Biashara inayoweza kukutoa ni ile inayokupa faida ya Tsh. 50,000 na kuendelea kwa siku

Biashara inayoweza kukutoa ni ile inayokupa faida ya Tsh. 50,000 na kuendelea kwa siku

Biashara yoyote ile ili uipende na ikulipe ipasavyo mpaka ushangae. Unapaswa hiyo biashara yako uiweke katikati sehemu husika, yaani upate location sahihi. Hakuna cha ushirikina wala nini biashara ukiipatia location sahihi utakimbiza mpaka uhitishe wasaidizi, uchawi wa biashara ni kupata location sahihi kutegemea na biashara yako husika.

Ata uwe na mtaji kidogo ila ukapatia location basi umeula, kuna dogo huwa nafahamiana nae basi huwa nikipata wasaha huwa naenda tunapata stori mbili tatu. Basi kuna siku alinigusia kuhusu biashara yake, hiyo biashara ukiiona utaichukulia poa na mbaya zaidi mimi na wewe tunaweza idharau na kutoifanya. Dogo aliniambia hiyo biashara yake mtaji ni 650k hapo kila kitu kaweka, akiuza mauzo kwa siku kisha akitoa matumizi ya siku anabaki na faida ya kiwango cha chini ni 70k. Dogo location aliyopo inamlipa sana
Fungua nywila hizo
 
Naunga mkono hoja...... location ni muhimu sana, hata ukiwa na 10m ukawekeza kwenye poor location na usipogundua mapema ukakomaa Basi jua tu utarudi nyuma.

Mfano Kuna rafiki yangu yeye anauza matunda kwa hiyo location akienda stereo anafunga mzigo wa laki sita wa matunda ambao kwa hiyo location ilivyochangamka baada ya siku mbili anaenda Tena sokoni.

Wakati anaanza alikuwa anakomaa Mwenyewe na akosi 70k to 100k Kama faida kwa siku.

Kwa Sasa anachukua hesabu ya 50k na hashughuriki anasimamia Mambo yake mengine yaende yaongeze kipato.

Kwenye masuala ya biashara amekuwa mentor wangu sana, pia najivunia kuwa rafiki yake maana Hana Roho mbaya kwenye maswala ya idea na fursa za biashara.
Niunganishe nae kaka
 
Hii

NMBBonus Account, akaunti maalumu ya kuweka akiba kwa ajili ya malengo yako ya muda mrefu. Akaunti hii inakupa mpaka asilimia 13* ya faida kila robo ya mwaka.
Katika hii account unaruhusiwa kutoa fedha mara moja tu katika miezi mitatu au ukasubiri na kupata gawio lako Kila baada ya miezi mitatu. Sema hii bonus account ni nzuri Kama unaweka mzigo mkubwa Kama million 500 , billion 1 au zaidi
Iyo 500M na Billion umezitaja kama elfu moja ivi?

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana kupata zaidi ya 50 endapo utabadilika mtazamo,kukariri biashara,pia focus kuboresha biashara ulionayo,mm ni wakala wa mpesa na huduma zingine za pesa mtandaoni,nimefunguka ofisi eneo ambalo ni kijiji ambako kuna pop.kubwa,nimetafuta line za lipa kwa mpesa,lipa kwa tigo,miamala yote ya kutoa pesa natoa kupitia line za lipa,faida ya maeneo ya pembezoni wateja wengi ni wale wanaotoa pesa kwani wanatumiwa na ndugu wa mjini,wateja wengi wanampa wakala simu ndio atoe hela,n.k sio haba ni sikosi 75000- 100000 kwa siku

Naweza sema wewe ni mjanja ila pia naweza sema kilio chako kinakuja coz izo Lipa zinakuja kufanyiwa kitu kimoja kikubwa balaaa
 
Biashara inayokupa Elfu 50 kama faida kila siku ni miaka 5 tu unaingia uchumi wa kati [emoji851]hapo no kuhonga no kujipongeza ni kazi kazi
 
Hii ni exclusive nakup now wameweka mashart no Tin, leseni haupati LIPA

Wameweka makato pia wansom location ya lain yako, wanasoma Location lain ya uwakala , wanaangalia kuwek na kutoa then wanazipa makato
Inaonekana lipa ni time bomb
 
Mimi nafikiri biashara hutofautiana kutokana na maeneo sio lazima uwekeze 5ml ndo uingize faida ya 50k,unaweza kuweka laki 2 na ukaingiza faida ya laki au 70k inategemeana unafanya nn na upo eneo gani,watu wa ziwani kama wapo nadhan wataielewa hii kwa upande wa samaki,mabondo n.k mtu ananunua mzgo wa lak 5 then mauzo yanatoka laki 7 just nusu saa tu amemalza kazi.
 
Back
Top Bottom