Biashara ipi ina mzunguko mkubwa kwa maeneo ya uswahilini Dar kati ya hizi?

Yejmaz20

Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
23
Reaction score
24
Wakuu wa JF

Kati ya biashara ya underwear, pochi, viatu vya kike na watoto na biashara ya phone accessories ipi ambayo una uwezekano wa kupata wateja wengi kila siku kwa maeneo ya uswahilini au yenye kipato Cha kawaida kwa hapa Dar?
 
Phone accessories, weka na Computer ya kuingiza nyimbo na movie hapo utaona mzunguko wa mitipula/pesa
Shukrani sana ndugu vipi ukizilinganisha hizo mbili phone accessories na underwear, viatu vya kike .......kwa mitaa ya kawaida ambayo sio uswahilini
 
Wakuu wa JF

Kati ya biashara ya underwear, pochi, viatu vya kike na watoto na biashara ya phone accessories ipi ambayo una uwezekano wa kupata wateja wengi kila siku kwa maeneo ya uswahilini au yenye kipato Cha kawaida kwa hapa Dar?
Inategemea na mahitaji ya wenyeji kwenye kila mtaa
Je ni wenyeji pekeyao?
Je wana muingiliano na wageni/wapita njia?
Je kuna shughuli nyingine za kiuchumi karibia? Kama
Bar.. Pubs guests nk
Viwanja vya michezo
Taasisi za elimu
Stand za magari
Viwanda vidogo vidogo nknk
 
Wakuu wa JF

Kati ya biashara ya underwear, pochi, viatu vya kike na watoto na biashara ya phone accessories ipi ambayo una uwezekano wa kupata wateja wengi kila siku kwa maeneo ya uswahilini au yenye kipato Cha kawaida kwa hapa Dar?
Weka accessories betry, memory, flash, card reader, usb, chaja protecto, airphones, na vingine ambavyo sijavitaja hakikisha unaweka bei rafiki sio kubwa sana wala ndogo sana maana ukiweka ndogo sana watasema ni fake

Sikushauri uweke kava za simu kubwa labda viswaswadu kava ni biashara kichaa sana
 
Vipi biashara ya hizo underwear, pochi /mikoba, viatu vya kike , slippers na sandles ....hii changamoto yake nin hasa Mkuu?
 
Sawa Mkuu ni sehemu ambayo ina population sio haba hapo ni maisha ha kipato Cha kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…