Kila biashara ni rahisi sana ukisimuliwa. Ingia ufanye ndio utajua kuna mambo hukuwahi kuambiwa. Imani yangu juu ya biashara ni
1. Sio kila mtu anaweza kufanya biashara. Naamini kuwa kila kazi iliyopo chini ya jua ni wito. Ili dunia iwe na balace lazima kila kazi ifanyike. Ni lazima kuwe na mtu mwenye kufanya kazi ya chini kabisa amabayo wengine wanaidharau ili tu dunia iwe kwenye balance kwa sababu watu watahitaji huduma yake. Unaweza kuingia kwenye biashara ambayo kuna mwenzio katoboa uka past na usitoboe. Ninaamini kwamba ukijua kusudibla wewe kuwepo duniani itakusaidia kujua nini sahihi kwako kufanya.
Namna moja wapo ya kujua ni pamoja na msukumo wa ndani yako. Kama kuna msukumo unatoka ndani yako kufanya jambo flani, kuna uwezekano mkubwa hio mdio calling yako. Kuna mdau hapo juu kasema biashara inakuhitaji wewe uliye na maono nayo, ila kuna watu wanamwita mtu wa negativity. Niseme hivii, huyo jamaa yupo sahihi asilimia zote. Kusimamia wazo ili likue huwa inatoka ndani yako. Yaani wewe ndio uko na maono ya kile unachokifanya kitu ambacho wengine hawataona.
Mfano mdogo sana, tunakubaliana wote kuwa biashara zina changamoto si ndio, sasa namna ya ku dela na baadhi ya changamoto inahitaji wito wa ndani ulionao. Kwamba uwe na msukumo wa ndani kutatua na kuzivumilia changamoto zitakazojitokeza. Mfano una fanya biashara ya kununua na kuuza, umenunua ila mzigo hautoki, hapo unahitaji msukumo wa ndani yako ku push kwa namna yoyote mzigo utoke. Sasa kufikiri hizo strategy kama unachokifanya sio kitu ukipendacho utafika muda utaona unateseka na huo ndio huwa mwanzo wa kuuwa biashara, ila kama inatoka rohoni uta feel proud sana kutafuta solution.
2. Imani yangu ya pili ya biashara ni kwamba kila biashara ina lipa. Tofauti ni mitaji na usimamizi. Ndio maana kila biashara inaanzishwa kila leo na kila biahsra ina kufa kila leo na zingine zina miaka zinaishi na kukua zaidi.
3. Ni vizuri kuomba ushauri wa nini ufanyanye ila ni vizuri zaidi kufanya unachokipenda kwa kuwa ndio utakisimamia kwa umakini. Biashara ni maisha, ili uifaidi inatakiwa iingie kwenye dami iwe sehemu ya wewe. Hio bond ikikosekana mwanzoni mwa biashara kufa kwake ni kugusa tu. FANYA UNACHOKIPENDA NA NDICHO UTAKACHOKISIMAMIA.
4. Kama huna passion na biashara ila unataka kuwekeza pesa yako ili izae, basi usifanye biashara, fanya uwekezaji wa hio pesa. Wekeza kwenye BINDS, wekeza kwenye viwanja, wekeza kwenye nyumba za kupangisha na vitu vingine kama hivyo. Usizungushe pesa ili hali wewe huna muda huo hata hapo mwazo wa biashara utalia.
ZINGATIA: Biashara ni kuzungusha pesa kwa haraka ikupe faida ndogo au kubwa ka haraka. Kuwekeza ni kununu au kutengeneza kitega uchumi kwa gharama kubwa au ndogo, kisha kitakuingizia pesa kidogo kidogo na baada ya muda mrefu sana ndio utaanza kuingiza faida.