Biashara ipi rahisi kuiendesha hata ukiwa mbali?

Biashara ipi rahisi kuiendesha hata ukiwa mbali?

Kila biashara ni rahisi sana ukisimuliwa. Ingia ufanye ndio utajua kuna mambo hukuwahi kuambiwa. Imani yangu juu ya biashara ni

1. Sio kila mtu anaweza kufanya biashara. Naamini kuwa kila kazi iliyopo chini ya jua ni wito. Ili dunia iwe na balace lazima kila kazi ifanyike. Ni lazima kuwe na mtu mwenye kufanya kazi ya chini kabisa amabayo wengine wanaidharau ili tu dunia iwe kwenye balance kwa sababu watu watahitaji huduma yake. Unaweza kuingia kwenye biashara ambayo kuna mwenzio katoboa uka past na usitoboe. Ninaamini kwamba ukijua kusudibla wewe kuwepo duniani itakusaidia kujua nini sahihi kwako kufanya.

Namna moja wapo ya kujua ni pamoja na msukumo wa ndani yako. Kama kuna msukumo unatoka ndani yako kufanya jambo flani, kuna uwezekano mkubwa hio mdio calling yako. Kuna mdau hapo juu kasema biashara inakuhitaji wewe uliye na maono nayo, ila kuna watu wanamwita mtu wa negativity. Niseme hivii, huyo jamaa yupo sahihi asilimia zote. Kusimamia wazo ili likue huwa inatoka ndani yako. Yaani wewe ndio uko na maono ya kile unachokifanya kitu ambacho wengine hawataona.

Mfano mdogo sana, tunakubaliana wote kuwa biashara zina changamoto si ndio, sasa namna ya ku dela na baadhi ya changamoto inahitaji wito wa ndani ulionao. Kwamba uwe na msukumo wa ndani kutatua na kuzivumilia changamoto zitakazojitokeza. Mfano una fanya biashara ya kununua na kuuza, umenunua ila mzigo hautoki, hapo unahitaji msukumo wa ndani yako ku push kwa namna yoyote mzigo utoke. Sasa kufikiri hizo strategy kama unachokifanya sio kitu ukipendacho utafika muda utaona unateseka na huo ndio huwa mwanzo wa kuuwa biashara, ila kama inatoka rohoni uta feel proud sana kutafuta solution.

2. Imani yangu ya pili ya biashara ni kwamba kila biashara ina lipa. Tofauti ni mitaji na usimamizi. Ndio maana kila biashara inaanzishwa kila leo na kila biahsra ina kufa kila leo na zingine zina miaka zinaishi na kukua zaidi.

3. Ni vizuri kuomba ushauri wa nini ufanyanye ila ni vizuri zaidi kufanya unachokipenda kwa kuwa ndio utakisimamia kwa umakini. Biashara ni maisha, ili uifaidi inatakiwa iingie kwenye dami iwe sehemu ya wewe. Hio bond ikikosekana mwanzoni mwa biashara kufa kwake ni kugusa tu. FANYA UNACHOKIPENDA NA NDICHO UTAKACHOKISIMAMIA.

4. Kama huna passion na biashara ila unataka kuwekeza pesa yako ili izae, basi usifanye biashara, fanya uwekezaji wa hio pesa. Wekeza kwenye BINDS, wekeza kwenye viwanja, wekeza kwenye nyumba za kupangisha na vitu vingine kama hivyo. Usizungushe pesa ili hali wewe huna muda huo hata hapo mwazo wa biashara utalia.

ZINGATIA: Biashara ni kuzungusha pesa kwa haraka ikupe faida ndogo au kubwa ka haraka. Kuwekeza ni kununu au kutengeneza kitega uchumi kwa gharama kubwa au ndogo, kisha kitakuingizia pesa kidogo kidogo na baada ya muda mrefu sana ndio utaanza kuingiza faida.
Umetoa darasa mkuu
Ninakuunga mkono kwa 100%
Huu ni ushauri wa watu ambao wako field (wanafanya biashara).
 
Biashara kuendesha ukiwa mbali inawezeakana lakini shida kuu ni kukosekana Kwa kitu kimoja tu
UAMINIFU.
kama hutoibiwa ama kudokolewa faida basi itaibiwa jumla
Utakuwa umechezea mtaji wako tu.
Biashara inahitaji uwepo wako ndipo itaenda Kwa ufanisi
Japo watu waaminifu wapo lakini namna ya kuwapata Sasa
Ukimpa mtu ng'ombe, hataishia kuiba samadi na maziwa tu akauza.
Ataiba ng'ombe amuuze.
 
Sisi tuliowekeza makampuni Italy, England, Portugal, Netherland, MLS biashara zetu unafanya popote, na kukagua mahesabu hata usiku wa manane unakagua bila wasi.
 
Una Tsh 50,000,000/= unazotaka kutumia kama mtaji wa biashara lakini muda wako wa kuisimamia kwa karibu sana ni finyu. Labda unakuwa huru wiki moja tu kila mwezi, siku zingine zote za mwezi unakuwa busy na shughuli zingine.

Mtu kama huyo anaweza kuianzisha biashara gani?

Labda:
1. Mghahawa?
2. Hardware?
3. Duka la nguo?
4. Duka la vifaa vya umeme?
5. Duka la simu?
6. Kiwanda cha juisi?
7. Huduma za kifedha kama uwakala wa M-PESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA, BANK?
8. Biashara gani hasa?

Utatumia mbinu gani ili kuweza kuisimamia kikamilifu hata ukiwa mbali?
hakuna,labda ununue ardhi mashamba na viwanja
 
Fanya biashara ya uwekezaji huko UTT
 
Kama huna muda wa kusimamia ni bora uweke hela yako UTT,tunachangamoto kubwa sana ya kupata vijana wa aminifu…kwakweli hili linaumiza mnoo…unamchukua kijana msomi unampa kazi (tena una mtoa kijijini aliko rudi baada ya kumaliza chuo) lakini anakuja kufanya vitu vya ajabu,anakuibia,anachezea hela yako wala hajali kabisa.

Niliamini wasomi wana tija kuliko darasa la saba lakini bora uajiri la saba kuliko hawa wasomi wetu.

Siku za nyuma nilikua sielewi kwanini kampuni nyingi wana wapa wakenya na wahindi nafasi za juu na watz nafasi za chini,kumbe ni kukosa uaminifu,kujituma na kuithamini kazi.
 
1. Jenga nyumba yenye muundo wa chumba sebule kadhaa pangisha.
2. NUNUA Hisa kwenye Taasisi zenye ziko imara kiuchumi.
HAKUNA BIASHARA NYINGINE ZAIDI YA HIZO
 
Ushauri:
1. Ajenge nyumba ya lupangisha au lodge.
Au
2. Aweke kwenye bank "fixed deposit"
 
Una Tsh 50,000,000/= unazotaka kutumia kama mtaji wa biashara lakini muda wako wa kuisimamia kwa karibu sana ni finyu. Labda unakuwa huru wiki moja tu kila mwezi, siku zingine zote za mwezi unakuwa busy na shughuli zingine.

Mtu kama huyo anaweza kuianzisha biashara gani?

Labda:
1. Mghahawa?
2. Hardware?
3. Duka la nguo?
4. Duka la vifaa vya umeme?
5. Duka la simu?
6. Kiwanda cha juisi?
7. Huduma za kifedha kama uwakala wa M-PESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA, BANK?
8. Biashara gani hasa?

Utatumia mbinu gani ili kuweza kuisimamia kikamilifu hata ukiwa mbali?
Hizo biashara zote zinahitaji usimamiz wa karibu...usijaribu kufanya hizo biashara

Mm ni mwajiriwa na biashara nnayoifanya bila stress yeyote ni ya kununua na kuuza vyombo vya moto...gari,bajaji hata pikipiki

Nanunua kwa watu wanaouza kwa bei mteremko,naipimp kdg nauza kwa bei ya juu

Hii biashara naifanya huu mwaka wa 4...imenipa Faida nzur sana,sijawahi jutia...sema ina hitaji uvumilivu Coz kuna wakati magari,bajaji au pikipk zinazouzwa kwa bei ya chini zinaadimika...inabd uvumilie tu

Changamoto nyngne ya hii biashara ni Madalali...aisee hawa watu ukishindwa cheza nao vzr huambulii kitu..ila ukikaa nao kiujanja ujanja,mambo yanaenda vzr tu
 
Una Tsh 50,000,000/= unazotaka kutumia kama mtaji wa biashara lakini muda wako wa kuisimamia kwa karibu sana ni finyu. Labda unakuwa huru wiki moja tu kila mwezi, siku zingine zote za mwezi unakuwa busy na shughuli zingine.

Mtu kama huyo anaweza kuianzisha biashara gani?

Labda:
1. Mghahawa?
2. Hardware?
3. Duka la nguo?
4. Duka la vifaa vya umeme?
5. Duka la simu?
6. Kiwanda cha juisi?
7. Huduma za kifedha kama uwakala wa M-PESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA, BANK?
8. Biashara gani hasa?

Utatumia mbinu gani ili kuweza kuisimamia kikamilifu hata ukiwa mbali?
Biashara nzuri ni kubeti tu. Mwambie ajenge undugu na m bet, sport pesa, x bet kwa wiki hakosi bn 1
 
Back
Top Bottom