Biashara ipi rahisi kuiendesha hata ukiwa mbali?

Umetoa darasa mkuu
Ninakuunga mkono kwa 100%
Huu ni ushauri wa watu ambao wako field (wanafanya biashara).
 
Ukimpa mtu ng'ombe, hataishia kuiba samadi na maziwa tu akauza.
Ataiba ng'ombe amuuze.
 
Sisi tuliowekeza makampuni Italy, England, Portugal, Netherland, MLS biashara zetu unafanya popote, na kukagua mahesabu hata usiku wa manane unakagua bila wasi.
 
hakuna,labda ununue ardhi mashamba na viwanja
 
Fanya biashara ya uwekezaji huko UTT
 
Kama huna muda wa kusimamia ni bora uweke hela yako UTT,tunachangamoto kubwa sana ya kupata vijana wa aminifu…kwakweli hili linaumiza mnoo…unamchukua kijana msomi unampa kazi (tena una mtoa kijijini aliko rudi baada ya kumaliza chuo) lakini anakuja kufanya vitu vya ajabu,anakuibia,anachezea hela yako wala hajali kabisa.

Niliamini wasomi wana tija kuliko darasa la saba lakini bora uajiri la saba kuliko hawa wasomi wetu.

Siku za nyuma nilikua sielewi kwanini kampuni nyingi wana wapa wakenya na wahindi nafasi za juu na watz nafasi za chini,kumbe ni kukosa uaminifu,kujituma na kuithamini kazi.
 
1. Jenga nyumba yenye muundo wa chumba sebule kadhaa pangisha.
2. NUNUA Hisa kwenye Taasisi zenye ziko imara kiuchumi.
HAKUNA BIASHARA NYINGINE ZAIDI YA HIZO
 
Ushauri:
1. Ajenge nyumba ya lupangisha au lodge.
Au
2. Aweke kwenye bank "fixed deposit"
 
Hizo biashara zote zinahitaji usimamiz wa karibu...usijaribu kufanya hizo biashara

Mm ni mwajiriwa na biashara nnayoifanya bila stress yeyote ni ya kununua na kuuza vyombo vya moto...gari,bajaji hata pikipiki

Nanunua kwa watu wanaouza kwa bei mteremko,naipimp kdg nauza kwa bei ya juu

Hii biashara naifanya huu mwaka wa 4...imenipa Faida nzur sana,sijawahi jutia...sema ina hitaji uvumilivu Coz kuna wakati magari,bajaji au pikipk zinazouzwa kwa bei ya chini zinaadimika...inabd uvumilie tu


Changamoto nyngne ya hii biashara ni Madalali...aisee hawa watu ukishindwa cheza nao vzr huambulii kitu..ila ukikaa nao kiujanja ujanja,mambo yanaenda vzr tu
 
Biashara nzuri ni kubeti tu. Mwambie ajenge undugu na m bet, sport pesa, x bet kwa wiki hakosi bn 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…