Biashara ipi rahisi kuiendesha hata ukiwa mbali?

Huu ni ukweli mchungu sana ambao sisi waaafrika weusi wengi aidha hatuujui au tukiujua huwa hatuukubali mpaka ujaribu halafu yakukute...!

Sina cha kuongeza....mtoa mada, kaweke hela zako UTT au bora uwekeze kwenye real estate(nyumba za kupangisha)....ingawa watakwambia real estate hailipi, ukweli inalipa bali kwa rate of return ndogo, uzuri wake ni kwamba pesa yako inakuwa haijapotea, ipo kwenye mjengo unaokupa kidogo kidogo kwa mwezi.

Nje ya humo utalia tu.....been there, done that!
 
Sasa tufanyaje na hii mitaji yetu?
Save your money kwa kuwekeza kwenye trust funds kama UTT, iTrust etc....nunua stocks kama Shares, Bonds etc...

Forget about the getting rich quick schemes, they don't work in real world, utapoteza pesa zako.

Nenda na principle ya Kawia ufike, weka pesa kwenye hizo trust funds & stocks....utapata returns kidogo kidogo lakini with the compounding effect, eventually utakuwa na ukwasi...just needs discipline & patiency. Bottom line hapa ni kwamba hutopoteza pesa zako.
 
Hapo utt ipi nzuri ukwasi au bond fund?
 
Kwanza tayari kashafeli ukianza kuuliza hivyo tu itakuwa sababu moja ya kufeli aisee hii kitu imewahi kunikuta aisee
 
Nunua BOND
 
Acha vitisho na kutisha watu mnakuwa na mentality za kuwaaminisha watu kuwa Biashara ni za watu fulani .
Sio vitisho mkuuu,,anajaribu kumweleza uhalisia.biashara ukimwachia mtu mostly watanzania sio waaminifu..

Biashara inapoanza inamuitaji zaidi mwenye maono yake hadi itaposimama ndio waweza muachia mtu asimamie.. otherwise uwe level ya uwekezaji ndio unaweza anza kwa kuajiri wataalamu husika wasimamie biashara Yako.
 
Mkuu kama una hiyo pesa peleka UTT. Ushauri wa bure bila consultation fee.
 
Ahsante sana wadau Kwa michango yenu,natumaini mleta mada kaelewa,kiufupi wadau mmesema biashara ni wito,na mwenye wito ndie mwenye msukumo wa kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazojitokeza ili kufikia maono yake,Kwa kuongezea biashara inahtaji ukaribu wako zaidi kuliko hata kazi yako,yani biashara iwe sehem ya maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…