round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 933
- 3,051
Biashara ni mchakato: Jifunze kwanza, kisha pata ujuzi, jenga connections zako, ndipo utakapojua cha kufanya na mtaji.
Lakini kwa watanzania wengi ni kinyume, wanaumiza sana vichwa kupata mtaji ili kuanza biashara lakini jambo hili kwenye process nzima inabidi iwe hatua ya mwisho kabisa. ndio maana wengi biashara wanazifunga, mitaji inayeyuka, wanaofanikiwa bila nidhamu ya pesa wamejikuta wakifilisika, n.k.
Kuparamia biashara bila kupitia mchakato / process ni sawa na kwenda vitani bila mafunzo, wafanyabiashara wengi wapya wanaotegemea mitaji zaidi hadi kupata mafanikio hupitia mchakato kwa maumivu zaidi ikiwemo kuanguka na kuinuka mara kadhaa na aina hii ni wachache, wengi biashara zikiwashinda hawana roho za kurudia.
LEARNING
Wazungu wanasema uki Learn kinachofuata L inatoka una Earn, na hakunaga namna nzuri ya kujifunza kama kwa vitendo / Practicle. Kujifunza kwenye vitabu, Youtube, n.k. iwe ni kupata basics au umekosa kabisa sehemu ya practicle.
Ni vizuri zaidi ujifunze biashara ukiwa unashiriki, Watu waliobahatika wanakuta familia tayari zina biashara na kuna utamaduni wa kuwafunza tangu wadogo, hio ni advantage kubwa sana hasa kwenye family za wahindi na waarabu, waswahili tunakosea sana kusubiri Watoto wafike 25 wameshakomaa sana hao, you cant teach easily new tricks to an old pet, ngumu sana kumkunja samaki aliekauka.
Kwa wale wengine uwe tayari kujifunza hata kwa kujitolea, kubali kujishusha ujifunze, angalia unataka kufanya biashara gani kisha approach wadau uombe kazi ama kujitolea na ujitume sana usibweteke kukaa sehemu ya kazi tu omba baadhi ya vitu umsaidie boss kuna mengi unapata. kama unataka ufanya biashara ya mazao nenda uwe msaidizi wa dalali wa mazao, kama unataka uuze spare za magari kajitolee kwenye maduka ya spare, Unataka kufanya kilimo omba uwe msaidizi wa mkulima tumia hio chance uone hatua zote za kuandaa shamba mpaka kuvuna, Unataka kufuga omba kazi kwa mfugaji, Ni mwanzo mzuri wa kuanza kujifunza, boss anataka kwenda kulipia leseni muombe umsaidie, mzigo umekwama omba ruhusa ukafatilie utajifunza mengi, boss anataka akague mzigo muombe umsaidie atakufundisha, jitoe sana lengo lako ni kupata madini sio kutegemea huo mshahara na kufurahia kazi chache, unapoona kuna shida ambayo inabidi itatuliwe fanya uwezavyo uombe uwepo, chukulia kama fursa sio kazi.
KUPATA UZOEFU.
Uzoefu wa mtu haununuliki, unanunuliwa kwa muda wakati unajifunza
Wakati unajifunza (Learning) utapata ujuzi (Experience) wa kujua tabia za soko, aina za wateja, kuzijua ofisi za vibali vya biashara, Mbinu za matapeli, n.k. hii itakusaidia sana usiwe mgeni ukianzisha yako.
Hali hii pia inakufanya uone jinsi ulimwengu wa biashara ilivyo na competition, unapata kitu muhimu kinaitwa Nidhamu / Discipline, muda huu tayari unajitolea au kupokea pesa kidogo inakujengea nidhamu ya pesa.
NETWORKS
Huwezi kufanya biashara kivyako hasa hapa Tz unahitaji Circle.
Muda mwingi unapokuwa kwenye shughuli flani basi unazungukwa na watu wenye maslahi yanayofanana, Utaanza kujuana na wateja, utajuana na watoa vibali, utajikuta umo kwenye groups za wadau, kuwajua suppliers, n.k. muhimu zaidi kuwajua wababaishaji unaotakiwa kukaa nao mbali.
MTAJI
Baada ya kupitia mchakato ndipo uanze kuwaza mambo ya mtaji, process ulizopitia ni sawa na upinde uliovutwa, mtaji ni kama kufyatua, ukianza biashara itafika mbali zaidi kuliko ya mgeni.
Confidence / Business spirit ya kufanya biashara unayo, Connections zipo, Uzoefu unao, maarifa unayo, Discipline unayo, ni silaha kubwa sana hizi na muhimu zaidi kila moja uliipata hatua kwa hatua one step at a time.
Mnapowaona wahindi, waarabu, wapemba, n.k. wapo walioishia la saba lakini wanafanikiwa kwenye biashara hakunaga shortcuts, Tangu wakiwa wadogo wanafundishwa biashara (Learning), kwenye hii process wanaona jinsi pesa ilivyo ngumu kupatikana wanajifunza kitu kingine Nidhamu (Discipline), watapata uzoefu wa kudeal na wateja na changamoto za biashara (Experience), Kwenye mchakato wanajuana na wadau wengine wanajenga mtandao (Networking), Hatua ya mwisho ndio wanapewa mitaji au kukabidhiwa kuziendeleza biashara za familia.