Kwakuwa umeshajua kilichokukwamisha,sasa unaweza kufanya tena vizuri zaidi,ila hapa no.2 kuwa napo makini sana, wanasema usicheke na nyani utaambulia mabua.Ninamfahamu jamaa alikuwa na duka limesheheni vitu kibao ni kama mini supermarket,alikuwa anafanya mwenyewe,ikatokea jamaa akapata shuguli nyingine akamuachia mkewe yeye akawa anakuja akipta nafasi,huwezi amini biashara iliyumba vibaya mno,mke hajui customer care,full kunununa na kufokea wateja,aliposhtuka wateja wamemkimbia na biashara imeshuka,ikabidi arudi mwenyewe kijiweni,mpaka sasa yuko vizuri sana na mke sikumuona tena pale dukani,maana ilifikia mahali mpaka walikuwa wanafokeana live na mkewe pale dukani...