Inaendelea.....
5: Kabla ya kuamua kufanya biashara flani ifnyie utafiti wa kutosha.
utafiti wa kutosha yani....sio tu thread wakuu nataka biashara ya mama lishe vipi, majibu yanakuja nunua sahani nunua sufuria na mwiko anza kazi inalipa[emoji81], maana yake nenda kwa mama lishe kakae hapo huku ukipiga story na kula angalia namna wanavofanya kazi zao, najua wanasambaza chakula na kukusanya hela jioni uliza changamoto zao tembelea wengi wa kutosha na biashara nyingine hivyo hivyo.
Experience yangu katika hili: nilivagaa biashara ya kukopesha nilienda kariakoo beba mapochi beba nguo biashara siijui nikakopesha watu.....mmmh nilibaki na majuto heri ningevaa tu hizo nguo na pochi nkabeba.
Experience yangu nyingine: nilifungua duka la vyakula mchele, unga, maharage nk nikamuweka housegirl nliekaa nae nyumbani miaka 7 nikiamini namjua ni mwaminifu, home nikaweka mwingine daaaah kumbe pesa haina uaminifu, alikua anakula hela zangu kama hana akili na kwakua nlimuamini nlifanya mahesabu kizembe hata mwezi unakata sijapiga hesabu.
Kosa lingine kubwa sana nilifanya kutokujua mi mwajiriwa naamka asubuhi naenda kazini yeye anaenda dukani, anauza ila anasema hajauza nitajuaje??? Hii biashara sikupaswa kuifanya kabisa make inahitaji uwepo muda wote namie kuwepo muda wote haiwezekani ila wala sijutiii sasa nisingefanya ningejifunza vipi.
Pia ilikua mbali na nyumbani mbali na kazini gharama za nauli daily nk mwisho nilichukua vyakula nkaweka nyumbani tukala.
Nmeamua kufanya biashara nyingine inayoendana na kazi yangu, nilianza kwa utafiti nimezunguka sana, nashukuru kuna jamaa anaifanya na sio mchoyo wa maarifa amenipa sio tu abc....yani ni abc hazi z ana roho nyeupe, nimepitia nyuzi sana, na ninaisimamia vema naamka mapema naanzia kwenye biashara kwanza saa mbili ndo naenda kazini, nikitoka chaaap narudi kijiwe,
naiona mwelekeo mzuri.....hii haifi yani ntakufa mie hii haifi [emoji81]
waajiriwa tuchague biashara walau yenye usimamizi wa kueleweka, isiokuhitaji hapo 100% yani inaweza kuendelea vema na haupo mfano biashara za kukodisha vitu mbalimbali, vyombo, maturubai, viti, nk nk vya kukodi ni vingi, au biashara inayohesabika unajua vilikua vitano kimeuzwa kimoja vimebaki vinne....
Kama ni biashara ya chakula, mfano mi nikitaka kuifanya nitauza ugali, nyama choma/mishkaki na kachumbari tuuuuu au ndizi kaanga/choma pia.....hii ina urahisi kusimamia nmeacha ugali 30 nikija nataka hesabu ya ugali 30 kama umebaki nitaona, ila ukianza na wali na michuzi mambo yatapandiana.