Mr IQ
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 1,024
- 1,377
- Thread starter
- #101
Nimejifunza kitu kizuri sana kwako.. inatakiwa nijifunze kuwa mfuatiliaji kwenye biashara.Ukitaka kupata pesa za biashara uwepo wewe
Hakuna alternative
Haipo
Nakuhakikishia haipo
Hata ukiwa na branch za hizo biashara zako sema ukafungua mikoa miwili
Lazima moja italega
Hawa wenye makampuni na mawiwanda wanaajiri. Watu wa kuzisimamia hizo
Ulinzi wa hali ya juuu
Lakin pia biashara nyingi watu wanafunga cctv camera na usimamizi kama kambi ya jeshi
Mimi nipo kwenye biashara yangu asilimia 99%
Hiyo moja nikisafiri kufata mzigo lakini pia
Nina vijana ila na mimi napiga kazi ukija huwezi jua boss nani
Wote sisi ni wafanyakazi wa kazi yangu
Mzunguko wangu ni mauzo ya milion 10-15 kwa mwezi
Wastan wa laki 4 mpaka 5 kwa siku
Ila ninabana mpaka kona
Picha linaanza nimefunga camera
Namba mbili kila siku kama wewe unavyoamka kwenda kazini na mimi naenda kwenye biashara
Na sikai kwenye kitu
Tunafanya wote kazi
Kwa kifupi stoo zote najua hadi box la mwisho lilipowekwa hata ukiniamsha usiku
Najaribu kukuambia nini
Yote hayo uwezi fanya ukiwa umeajiriwa
Usikope pesa alafu ukaweka kwenye biashara ambayo huwezi kuisimamia
Mimi ni mwanamke nina backup ya mume wangu
Wakati naacha kazi nilisema kivyoyote sitalala njaa
Ila asilimia kama 80 nilishapna mwangaza wa biashara yangu ila kilichokua kinakosekana ni kimoja
UWEPO WANGU
nakushauri usikope pesa ukaweka kwa biashara ambayo inakuhitaji
Yaani ukaweka milion lets say 30 alafu ukamuachia kijana acheze nazo
Eeeh sikushauri
La mwisho
Uko mkoa gani nikushauri kitu kizuri sana.
Ambacho kwa mimi nakiona ni simple na halihitaji uwepo wako
Japo kina gharama
Ila kwa nature ya wewe ulieajiriwa kitakufaa
Kwasasa nipo Mkoa wa Pwani, ila kikazi ntahamia Nyanda za juu kusini(Greencity) next year Mwenyezi mungu akijalia, Kama unampango wakunishauri anzia Greencity ndugu yangu.