Biashara nzuri ya uzalishaji isiyo ya umachinga

Ahsante mkuu kwa ufafanuzi mzuri ufafanuzi wako umeniongezea kitu

Mimi nilifanya uchunguzi mdogo kuna kipindi nilihitaji kuanzisha hii kitu kwa udogo nikaanza kufuatilia majibu nikaona naweza wazo bado ninalo na Mungu akipenda nitazalisha maji kijijini hapa one day

Ila huyo mwamba anakatisha watu tamaa kwa kitu asichokifanyia uchunguzi zaid ya kusoma kwenye mitandao
Anahitaji labda uzalishaji mkubwa, awe na uwezo wa kuchakata Lita elfu 5 kwa lisaa.
 
Million 100 yote ya nini?. Kuna RO zenye uwezo tofauti inategemea wewe unataka uzalishe Lita ngapi kwa siku. Kuna RO zinazochakata mpaka Lita 500 kwa sasa ambapo ukipiga kwa masaa 9 ikiwa inatembea unapata 500×9=4,500 Lita . Sasa RO Kama hii nibei ndogo sana.

Baada yahapo unahitaji machine ya Filling, ingawa pia unaweza tumia Manual Filling (Nimeshuhudia hili) ambapo gharama yake ni ndogo sana.

Kama unahitaj uanze kitajili andaa hio mil 100. Lakini kama unataka uanze kimasikini niela ndogo.

Mfano maji PANGANI(kama sijasahau jina) yanazalishwa SIDO ya pale Tanga(GOFU CHINI) Na mzalishashaji kajisajili kama mzalishashaji mdogo. Nenda kaangalie machine alizonazo kisha utakuja kubadili kauli yako.

Ukienda urafiki hapo RO yao nizaidi ya mil 100. Sasa inategemea wewe unataka uzalishaji wa aina gani.
Hizo mashine ndogo pamoja na mashine ya ujazaji na ufungaji inaweza kugharimu kiasi gani mkuu maana nina kisima nilichimba kina maji mengi nina wazo la kuanzisha kiwanda kidogo cha maji. Nitashukuru ukinipa mwongozo mkuu.
 
Nimefanya kazi kiwanda cha water& cosmetics, plastics, pamoja na soft drinks.

Blowing machine ya nini?. Hii inatumika kama unanua preform then unaenda kuziblow kwenye PET BLOW MOULDER MACHINE ili upate size ya chupa unayohitaji. Huna haja nayo kwa sababu Kuna makampuni yanauza chupa ukiweka oda unauziwa chupa unazotaka.

Labeling machine hii inasaidia kuweka lebo, lkn huna haja nayo kwa sababu Kuna baadhi ya viwanda kama PPTL&MAMUJEE& A ONE wanaofanya kazi ya Labelling ni watu na machine zipo kidogo na muda mwingine hazifanyi kazi kwa sababu zinaharibika mara Kwa mara wengi wanazinunua kutoka India.

Shrinking machine huna haja nayo kwa sababu unaweza nunua hand Drayer ndogo ambayo itakusaidia kuzifanyia shrinking lebo Ili zishikane vizuri na chupa.

Jengo unakodi sido na nibei ndogo.

Marketing utaanza kwa kufanya Mwenyewe na kusambaza madukan .

Labour kwa kazi ya maji unahitaji operator mmoja wa RO ambae pia anaweza kua supervisor at the same time kwa watu wanaofanya labeling& Shrinking ukamlipa pesa iziyozidi elfu kumi per day.

Filling machine unatumia manual Filling, unahitaji watu wasiozidi 4 ambao wanaweza jaza zaidi ya Lita 1000 kwa siku na ukawalipa pesa Kila mmoja isiyozidi elfu 7.

Baada yahapo ukihitaji hizo machine unazotaka wewe lazima uwe pia na Compressor kwa sababu machine hizo ni pneumatic machine haziwezi tembea bila upepo. Hasa Blow MOULDER, capping &Filling machine pia ukitaka unavyotaka wewe lazima uwe na machine ya PET INJECTION MACHINE kitu ambacho hakina ulazima. Pia utahitaji Cooling tower kwa sababu injection machine nyingi ni cold mode.

Ukitaka uzalishaji kama wako andaa zaidi ya mil 500.

Lakini kama wangu kwa mzalishaji mdogo haizidi mil 20.
Umeandika jambo gumu mpaka nimeliona ni rahisi. Shukrani nimeshawishika sana na hii biashara.

Mkoa gani naweza ifanya hii nikapata wateja wa uhakika maana hapa Dar naona kama maji ni mengi sana
 
Mbali na haya,àmka Nenda Ofisi za Sido,Nenda Veta,Nenda Wizara ya Viwanda na biashara.Huko kuna Takwimu na Taarifa.Ukiweza pia pata data za TRA Juu ya imports nyingi toka Nje,Mfano Nchi inaagiza Sana bidhaa gani.Hizo ndiyo gaps.Kabla ya kuanza Hakikisha Una Taarifa na Maarifa Kwanza,kisha Ujuzi wa Kile unataka kufanya.Pili biashara ni pamoja na kutatua zile Changamoto ngumu,hii Kwa Mjibu wa Tajiri wa Kichina Jack Ma.Nakupa big up kuwazia Uzalishaji wa bidhaa badala ya uchuuzi.Kwa TZ watu wanapenda Sana uchuuzi maana hauhitaji Matumizi Makubwa ya Akili.Ukiweza Tembele pia mikoani.Ninapanga Kuzalisha bidhaa rahisi toka Kwa Mazao kama Karanga na Asali.Pia naendelea na mchakato wa Kuzalisha Sàbuni za Maji.Nimemaliza Mafunzo ya awali ya SIDO Geita.Nakutakia kila la Kheri.
 
Nimefanya kazi kiwanda cha water& cosmetics, plastics, pamoja na soft drinks.

Blowing machine ya nini?. Hii inatumika kama unanua preform then unaenda kuziblow kwenye PET BLOW MOULDER MACHINE ili upate size ya chupa unayohitaji. Huna haja nayo kwa sababu Kuna makampuni yanauza chupa ukiweka oda unauziwa chupa unazotaka.

Labeling machine hii inasaidia kuweka lebo, lkn huna haja nayo kwa sababu Kuna baadhi ya viwanda kama PPTL&MAMUJEE& A ONE wanaofanya kazi ya Labelling ni watu na machine zipo kidogo na muda mwingine hazifanyi kazi kwa sababu zinaharibika mara Kwa mara wengi wanazinunua kutoka India.

Shrinking machine huna haja nayo kwa sababu unaweza nunua hand Drayer ndogo ambayo itakusaidia kuzifanyia shrinking lebo Ili zishikane vizuri na chupa.

Jengo unakodi sido na nibei ndogo.

Marketing utaanza kwa kufanya Mwenyewe na kusambaza madukan .

Labour kwa kazi ya maji unahitaji operator mmoja wa RO ambae pia anaweza kua supervisor at the same time kwa watu wanaofanya labeling& Shrinking ukamlipa pesa iziyozidi elfu kumi per day.

Filling machine unatumia manual Filling, unahitaji watu wasiozidi 4 ambao wanaweza jaza zaidi ya Lita 1000 kwa siku na ukawalipa pesa Kila mmoja isiyozidi elfu 7.

Baada yahapo ukihitaji hizo machine unazotaka wewe lazima uwe pia na Compressor kwa sababu machine hizo ni pneumatic machine haziwezi tembea bila upepo. Hasa Blow MOULDER, capping &Filling machine pia ukitaka unavyotaka wewe lazima uwe na machine ya PET INJECTION MACHINE kitu ambacho hakina ulazima. Pia utahitaji Cooling tower kwa sababu injection machine nyingi ni cold mode.

Ukitaka uzalishaji kama wako andaa zaidi ya mil 500.

Lakini kama wangu kwa mzalishaji mdogo haizidi mil 20.
Mkuu nakutafuta umefunga PM yako, vipi nakupataje
 
Umeandika jambo gumu mpaka nimeliona ni rahisi. Shukrani nimeshawishika sana na hii biashara.

Mkoa gani naweza ifanya hii nikapata wateja wa uhakika maana hapa Dar naona kama maji ni mengi sana
Ushauri wangu fanyia Tanga, kwa sababu kuna bidhaa chache tu zinazotumika kule pia cheap labour wamejaa, na pale sido hakuna mlundikano wa watu. Pia Dodoma sio mbaya.
 
Hizo mashine ndogo pamoja na mashine ya ujazaji na ufungaji inaweza kugharimu kiasi gani mkuu maana nina kisima nilichimba kina maji mengi nina wazo la kuanzisha kiwanda kidogo cha maji. Nitashukuru ukinipa mwongozo mkuu.
Mashine ndogo hizo za RO zipo za mpaka mil 5/7. Issue ya ufungaji Haina haja ya machine kama waanza. Usiwekeze pesa nyingi kwenye soko ambalo hujawa na uhakika nalo.
 
Back
Top Bottom