Nimefanya kazi kiwanda cha water& cosmetics, plastics, pamoja na soft drinks.
Blowing machine ya nini?. Hii inatumika kama unanua preform then unaenda kuziblow kwenye PET BLOW MOULDER MACHINE ili upate size ya chupa unayohitaji. Huna haja nayo kwa sababu Kuna makampuni yanauza chupa ukiweka oda unauziwa chupa unazotaka.
Labeling machine hii inasaidia kuweka lebo, lkn huna haja nayo kwa sababu Kuna baadhi ya viwanda kama PPTL&MAMUJEE& A ONE wanaofanya kazi ya Labelling ni watu na machine zipo kidogo na muda mwingine hazifanyi kazi kwa sababu zinaharibika mara Kwa mara wengi wanazinunua kutoka India.
Shrinking machine huna haja nayo kwa sababu unaweza nunua hand Drayer ndogo ambayo itakusaidia kuzifanyia shrinking lebo Ili zishikane vizuri na chupa.
Jengo unakodi sido na nibei ndogo.
Marketing utaanza kwa kufanya Mwenyewe na kusambaza madukan .
Labour kwa kazi ya maji unahitaji operator mmoja wa RO ambae pia anaweza kua supervisor at the same time kwa watu wanaofanya labeling& Shrinking ukamlipa pesa iziyozidi elfu kumi per day.
Filling machine unatumia manual Filling, unahitaji watu wasiozidi 4 ambao wanaweza jaza zaidi ya Lita 1000 kwa siku na ukawalipa pesa Kila mmoja isiyozidi elfu 7.
Baada yahapo ukihitaji hizo machine unazotaka wewe lazima uwe pia na Compressor kwa sababu machine hizo ni pneumatic machine haziwezi tembea bila upepo. Hasa Blow MOULDER, capping &Filling machine pia ukitaka unavyotaka wewe lazima uwe na machine ya PET INJECTION MACHINE kitu ambacho hakina ulazima. Pia utahitaji Cooling tower kwa sababu injection machine nyingi ni cold mode.
Ukitaka uzalishaji kama wako andaa zaidi ya mil 500.
Lakini kama wangu kwa mzalishaji mdogo haizidi mil 20.