Biashara siyo rahisi

Huu ni ukweli 100% na ujinga wa ngozi nyeusi ni kuamini waliofanikiwa ni washirikina, mtu akiona nina mafanikio fulani anaanza wewe kabila gani.

Nikimjibu mimi ni Mkinga anahitimisha kuwa ni mshirikina ila hajua mimi ninavyopambana kusaka pesa.
Sijui wakinga ni nani aliwawekea hii kitu maana mkinga kokote alipo lazma mafanikio yake yahusishwe na ndumba, iwe songea, mbeya au dsm
 
Hata kina Bakhressa pia na Musk ni wachuuzi tofauti ni ukubwa wa huo uchuuzi. Biashara yoyote ni kuuza ama huduma au vitu na kutengeneza faida na ndio uchuuzi wenyewe.
Mchuuzi ni mfanyabisshara wa level ya chini kabsa.Kama ni mfanyakazi basi ni mfagia ofisi
 
Sijui wakinga ni nani aliwawekea hii kitu maana mkinga kokote alipo lazma mafanikio yake yahusishwe na ndumba, iwe songea, mbeya au dsm
Kwanza, Kuna ishu ya upatikanaji wa mtaji na speed yao ya kukuza mtaji fastafasta.
Pili ishu ya kupata wateja wengi ghafla. Hata ushushe bei kuliko yeye kwa bidhaa sawa na yeye. Yeye atauza sana kuliko wote.
Wale waliopo kwenye biashara wanaelewa kuhusu changamoto ya wateja. Ila unashangaa mkinga anafungua pembeni yako na bidhaa kama zako ambazo wateja ni wa kusuasua. Ila yeye akiuza wateja mafuriko 😂. Halafu biashara ni wateja.

Pia wakiona biashara ngumu anasafiri kuenda kijijini, akirudi atauza mno 😂😂😂. Mafuriko ya wateja sio ya kawaida. Sasa ndio maana watu wanamashaka na wakinga





Ila kiufupi biashara ni ngumu. Unaweza kuwekeza na kujituma ila changamoto ni WATEJA.
 
😁 wateja kama wateja, kwa hiyo akitoka nyumbani mnaanza kuhesabu maumivu 😁
 

Mfanyabiashara mkubwa akijitahidi Sana kulala Kwa siku atalala masaa Mayank.
Wangi wanalala masaa Pungufu ya hayo
 
Kuna mtu alisema ni swala la muda tu mfanya biashara kuwa na makandokando.
Ila bora yawe haya ya kukwepa kodi kuingiza bidhaa kimagendo kuliko kujihusisha na mawizard
 
Kumbuka kama unazungushia mil 1 mpaka mil 300 wewe ni mjasiriliamali na sio mfanya biashara
 
Nani kakudanganya bidii Tu ndio zitakutoa kwenye biashara nchi hii ? , biashara bila mentality ya kimafia na ubabe either physical na spiritual hutoboi hasa Tanzania hi
Ili ufanikiwe kwenye Biashara ni lazima kimoja wapo kati ya hivi kihusike, umafia na ubabe, ukwepaji Kodi, Connection,Dili haramu au uwe na wazo la kipekee kabisa na zaidi ya hivyo uwe na usimamizi mzuri wa pesa otherwise hakuna Biashara isiyo na makando Kando au sijui ujinga unaoitwa kujituma.
 
biashara ni umafia hasa
 
Mchuuzi ni mfanyabisshara wa level ya chini kabsa.Kama ni mfanyakazi basi ni mfagia ofisi
No. Huo ni ufinyu wa kifikra. Ni huku kwetu ndio tuna ujinga wa kuweka kazi kwa madaraja, wenzetu Ulaya thamani ya kazi ni kazi hakuna iliyo chini wala juu. Ndio maana tumekaa na mawazo ya Phds na GPA za darasani huko mtaani hamna kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…