Biashara siyo rahisi

No. Huo ni ufinyu wa kifikra. Ni huku kwetu ndio tuna ujinga wa kuweka kazi kwa madaraja, wenzetu Ulaya thamani ya kazi ni kazi hakuna iliyo chini wala juu. Ndio maana tumekaa na mawazo ya Phds na GPA za darasani huko mtaani hamna kitu.
Siyo mambo ya kucheka haya mkuu
 
No. Huo ni ufinyu wa kifikra. Ni huku kwetu ndio tuna ujinga wa kuweka kazi kwa madaraja, wenzetu Ulaya thamani ya kazi ni kazi hakuna iliyo chini wala juu. Ndio maana tumekaa na mawazo ya Phds na GPA za darasani huko mtaani hamna kitu.
Lete ufafanuzi wa maana halisi ya mchuuzi.
 
Kwa lugha nyepesi ni mtu anayechukua bidhaa kwa wingi na kuuza kwa faida. Mfano, mchuuzi wa samaki ananunua samaki pwani anaenda kuchuuza sokoni, Muuza mitumba ananunua contaoner china anachuuza Kariakoo, muuza magari ananunua Japan anachuuza Magomeni. Hao ni wachuuza bidhaa unazoziona, lakini mfano Vodacom ananunua internet toka kwa mwenye nazo anatuuzia sisi bando n.k.
 
Wewe sasa ndo umeongea ukweli kuhusu biashara.
 
Hata kina Bakhressa pia na Musk ni wachuuzi tofauti ni ukubwa wa huo uchuuzi. Biashara yoyote ni kuuza ama huduma au vitu na kutengeneza faida na ndio uchuuzi wenyewe.
Uchuuzi ni kununua kisha kwenda kuuza kwa bei ya juu kidogo ili upate faida, Bakharesa hayupo kwenye category ya mchuuzi.

Yeye ni producer tena mkubwa tu, kwahiyo yeye ni service provider.
 

I couldn't agree more except for sehemu ya uchawi. Hakuna uchawi ingekua mtu anaroga na kufanikiwa maskini wote wangekua matajiri maana ndo wanashinda kwa waganga Kila siku. Africa ingekua tajiri kuliko USA.

Kukwepa Kodi au kukandamiza wafanyakazi au customers is the name of the game worldwide sio bongo tu hasa wakati kampuni inajitafuta. Ukijifanya mtakatifu hutoboi abadan.
 
Uchuuzi ni kununua kisha kwenda kuuza kwa bei ya juu kidogo ili upate faida, Bakharesa hayupo kwenye category ya mchuuzi.

Yeye ni producer tena mkubwa tu, kwahiyo yeye ni service provider.
Usichanganye habari. Anachofanya yeye ni kuongeza thamani ya bidhaa. Tunarudi kule kule tu, ubunifu tu kwenye huo huo uchuuzi ili kupata faida zaidi. Ananunua mahindi anauza unga. Yule mchuuzi wa samaki naye angeweza kuwakaanga mfano, au akiwa na uwezo akasindika kwenye kopo akauza bei mara 6 zaidi
 
Mtu anaefanyw bulk mangoes kuwa juice, mtu anaetengeneza sukari za kutosha kuhuduma zone nzima, na mengine kama hayo unawezaje kumuita mchuuzi? Tafuta maana halisi ya neno uchuuzi, mtu wa production anawezaje kuitwa mchuuzi?

Kwenye chain ya biashara & Chain ya supply, kiini huwa ni PRODUCTION sasa mtu anaehusika na production hawezi kuwa mchuuzi hata siku moja.

Eti mchuuzi[emoji23].
 
Hebu google translate tu hilo neno, utalipenda tu
 
ukishaongeza thamani bidhaa actually unakuwa sio mchuuzi tena bali ni entrepreneur au mjasiriamali.

Sole purpose ya ujasiriamali ni creativity and innovation. Ama ubuni kitu kipya ama ufanye maboresho katika bidhaa ila uchuuzi ni kuongeza margin tu katika mali ili uuze kwa faida.
 
Angalau ww hujataja uchawi, hivyo vingine vyote ni sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo sio biashara. Ni uchuuzi na haina tofauti na kuajiriwa.
Kama biashara haiwezi kusimama wakati wewe haupo, ujue ni uchuuzi. Bora hata kuajiriwa kunakuwa na mafao NSSF/PSSSF.
Naona mavitabu ya motivation speakers yanakudanganya. Biashara sio rahisi hivyo
 
Naona mavitabu ya motivation speakers yanakudanganya. Biashara sio rahisi hivyo
Hapana. Tuambiane ukweli. Kwani uchuuzi ni kitu kibaya? Ni ngazi tu katika biashara.
Mimi sinaga hata muda na motovesheno spikaz.
 
Hayo majina/maneno ni urembo tu. Sawa na mtu anatembea pekupeku, au avae yeboyebo, au avae nike haijalishi wote wanatembea point A kwenda B.
 
Kwenye biashara hakuna kulala na ukilala unapiga tu mahesabu kichwani[emoji23][emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…