Biashara ya boda boda

Hii bishara kwa kweliii inahitaji moyo mm nilinunua last year mwezi wa kumi ilinipa changamoto kubwa sana hasa kwa dereva..
Yan dereva alikua mwongo afu boda anaigawa kama karanga za kuonja..
Worse case ikaibiwa this year mwezi wa nane.. ninachoshukuru Mungu wakati nanunua niliiweka bima kubwa hivyo bima now wamenilipa ila kwa kifupi biashara hii wanafanya iwe ngumu ni madereva hesabu....
Now nmeamua kufanya biashara ya kukopesha (microfinance) nayo inachangamoto zake ila sio kama boda boda...
Kama utanunua boda boda uwe na dereva mzuri na uweke bima kubwa....
 
Vizuri sana mbona nimeskia bodaboda hawakati bima kubwa mm nimenunua zangu nimeulizia nimeambiwa hawakati bima kubwa,bodaboda kweli ukipata dereva asiejua maisha utalia tatizo letu wengi wetu tukiona vijana wamekaa maskani tunawapa bodaboda wengine hawawezi kazi bora utafute mtu aliesota na maisha huwa waaminifu sana
 
Wanakata kaka mm nlikata Jubilee Insurance bima ilikua 162,500 we ulizia jubilee Insurance vizur..
 
Unatumia mbinu gani kwenye Ku manage hapo vijana?
1.makazi ya dereva,kujua sehemu anayotoka ni muhimu,ikiwemo barua ya utambulisho .
2.mdhamini wa dereva mwenye kueleweka.
3.shirikiana na mwenyeji mfano mwenyekiti wa mtaa kuwabaini dereva mzuri,kwani huko mikataba mbalimbali husainiwa,vile vile vijiwe vya bodaboda.
4.kufunga mfumo wa ulinzi kwenye chombo chako,mfano tracking system, bima kubwa.
5.pokea pesa kwa siku,maana kuna madereva wengine wakishalundika huona ugumu kuzitoa zote.
6.hakikisha mkataba una mashiko kisheria,ikibidi tafuta mwanasheria akusaidie kudrafti.
 
Wadau hii fulsa imekaaje unanunua pikipiki mwisho wa siku unaingiza pesa ya mboga!!
Wenye uzoefu wa biashara hii tupeane uzoefu...
 
Kwasasa ni biashara nzuri sana kwa baadhi ya maeneo.Kama unaendesha mwenyewe hasa kipindi hiki ambapo umalaya umekithiri.
 
Vizuri sana na vilevile dereva
usimbane saana sasa mwanasheria utampata vipi wanasheria si wanalipwa hela nyingi sio wengine hatuna uwelewa huo
 
Vizuri sana na vilevile dereva

usimbane saana sasa mwanasheria utampata vipi wanasheria si wanalipwa hela nyingi sio wengine hatuna uwelewa huo
Sio lazima mwanasheria kamili,hao ni ghali,wapo wa bei che
 
Njoo tuongee kama tutafika makubaliano 0713 727478
 

Unapiga mishe gani mkuu?
Tusaidiane kimawazo
 
Kila biashara ina changamoto zake cha muhimu ni kutokua negative na kutokata tamaa. Kuliko usiwe na chochote kinachokuingizia hela hata sh 100 bora uwe na boda boda yako na ili uone faida Nunua boxer used Iliyotumika mwaka au mwaka na nusu, ukinunua mkononi kwa mtu ni tsh 1.2M then unatafuta dereva anayejitambua unaingia nae mkataba ambapo kwa siku ni sh 15000 na mkataba ni wa mwaka baada ya mwaka pkpk itakua yake. Ukimwambie hivyo ataitunza na hamtasumbuana, service etc n juu yake pia ukiweza kuwa na boda zako 2 au 3 utafurai
 
Utaendesha mwenyewe....???
Utanyanganywa.
Utampa dereva..??
Itaibiwa
Achana na hiyo biashara kichaa
Kila biashara ina changamoto mbona kuna watu wanafanikiwa kwenye bodaboda wanamiliku mpaka 20,mm ni mmiliki nnazo kadhaa mbona changamoto za kawaida tu.
 
Hii biashara inahitaji usimamizi wa hali ya juu sana, usiwe mtu wa kupiga simu mara zote. Mfuatilie hatua kwa hatua
 
Kuna biashara nyengine mtu anaweza kuidharau haswa za uswahilini ila zinapesa japo sio nyingi ila hukosi faida kati ya 20-40 kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…