Wakubwa habari zenu,
Nina mtaji wa kama mil 3 hivi ila baada ya kupitia thread mbalimbali za humu JF nikaona bora niwekeze katika biashara mojawapo kati ya hizi
1. Biashara ya bodaboda
2. Biashara ya mchele
Firstly nimeanza na uchambuz wa hii biashara ya bodaboda ambapo hesabu zangu zinanionyesha kwamba faida yake inayopatikana haiendani na mtaji wake.
Hesabu zangu ni kama ifuatavyo;
1. Tuchukulie bodaboda ya mkataba wa elfu kumi kila siku then after mwaka mmoja(siku 365)dereva inakuwa yake
NB: Hapa naondoa hesabu za service, traffic, ajali maana hayo yanakuwa juu ya dereva according to mkataba
MTAJI
Bei ya manunuz + vibali + bima ni takrIbani 2,400,000/=
MAPATO
10,000 *365 days= 3,650,000
FAIDA
3,650,000 - 2,400,000=1,250,000
FAIDA KWA SIKU
1,250,000/365 = 3425
So kwa biashara hii ya mtaji wa mil 2.4 ina uwezo wa kukuingizia sh 3400 tu kwa siku kama faida!!
2. Tuchukulie hesabu ya 7000 kwa siku na bila ya makubaliano ya dereva kwamba itakuja kuwa yake
Hapa nimechukulia siku 360 kama mwaka,siku 65 zilizobaki hesabu yake nimefidia kwenye risk mbalimbali kama trafic, services, ajali etc
MAPATO
7000*300 days=2,100,000
Thamani ya bodaboda baada ya mwaka 1,500,000
2,100,000+1,500,000=3,600,000
FAIDA
3,600,000-2,400,000=1,200,000
FAIDA KWA SIKU
1,200,000/365=3200
Hapa inakua inakuingizia kiasi cha 3200 kwa siku
Nimepiga hizo hesabu kwa uelewa wangu binafsi na sio mjuzi wa kupiga hizi calculation za profit and loss kwa hiyo kama faida kwenye biashara haziwi calculated kama hivyo naomba mnisahihishe